Nashauri ubunge uwe na kikomo kama vile urais ulivyo na kikomo,tumechoka kuona mbunge anaukalia ubunge zaidi ya miaka 15

craq

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
859
1,864
Watu wengi hawapendezwi na suala la urais kuongezwa miaka au mgombea wa urais kizidisha ukomo wa miaka 10 hilo suala halina taabu wala shida


Lakini kuna jambo linatatiza kama sio kutia shaka kwanini ubungo hauna kikomo ,binafsi hili suala linanisikitisha utamkuta mtu amekuwa mbunge kwa takriban miaka 20 lakini kazi yake kubwa ni kupokea posho tu huku jimboni kwake maendeleo hayaonekani au maendeleo unaenda kwa mwendo wa kinyonga


Itungwe sheria ukomo wa ubunge uwe miaka 10 tu baada ya hapo damu mpya iingie na kuleta changamoto ,mtu amekalia jimbo miaka 25 obvious hakutakuwa na jambo jipya ,baada ya miaka 15-10 tupate sura ngeni huenda ikaleta changamoto mpya mawazo na sura zilezile miaka nenda rudi huchosha na kila kitu kina ukomo



Kama vile urais una ukomo basi na ubunge pia uwe na ukomo ,haki sawa kwa wote
 
Back
Top Bottom