Nashauri serikali Ifute michezo ya Mipira Live

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
3,302
6,115
Kama ilivyokuwa kwenye kuonyesha bunge live, vijana wengi na nguvu kazi nyingi wanakesha kwenye Bar, club na sehemu zingine za starehe kuangalia mechi mbali mbali za mpira. Mara EPL, Bundersliga, VPL, n.k Hii inafanya vijana wengi wanaacha kufanya kazi zao na kuangalia mpira kila kukicha. Hii ni mwaka mzima achilia mbali michezo kama olympics, kumbe la dunia, NBA

Sio hiyo tu hata usiku vijana kwa wazee wameacha kuhudumia ndoa zao kwa visingizio vya kuangalia mechi live. Hivyo kupelekea kuongezeka kwa wachepukaji, madada poa mtaani kwa sababu vijana na wanandoa kutotekeleza wajibu.

Utafiti bubu uliofanyika umeonesha vijana wanapoangalia mpira hushushia na vinywaji mbali mbali vingine vimewafanya kuwa kama vijana wa "ROMBO" warudipo nyumbani na kina mama kuanza kuimport waume kama "wamama wa Rombo".

Hivyo kupitia wizara ile na mamlaka yale yale tunaomba mechi zote zinazochezwa live zisitishwe badala ya yake wananchi waruhusiwe kuangalia highlight za Mchezo tu ili nguvu kazi za taifa ziweze kutumika kujenga nchi

TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA
 
Sielewi kwanini mipira ya nje inashabikiwa sana na watu?
Tofauti na kuichezea kamali,nini sababu ya watu wengi
kushabikia mipira ya nje kuliko kitu kingine chochote.
Mwenye jawabu tafadhali.
 
Sielewi kwanini mipira ya nje inashabikiwa sana na watu?
Tofauti na kuichezea kamali,nini sababu ya watu wengi
kushabikia mipira ya nje kuliko kitu kingine chochote.
Mwenye jawabu tafadhali.

KAmari zimekuja juzi juzi tu hapa...kama sio mshabiki kamwe hautaweza kuelewa sababu
 
Sielewi kwanini mipira ya nje inashabikiwa sana na watu?
Tofauti na kuichezea kamali,nini sababu ya watu wengi
kushabikia mipira ya nje kuliko kitu kingine chochote.
Mwenye jawabu tafadhali.
Mpira wa ndani unaboa, Tim ya taifa haijawahi fika hata robo ya robo final katika mchezo wowote duniani, na tunalipa makocha mabilioni
 
Back
Top Bottom