Nashauri serikali ifanye haya kumaliza tatizo la ajira kwa vijana

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Kiukweli serikali ya awamu ya tano chini ya JPM imefanya mambo makubwa sana katika nyanja ya kuboresha miundombinu na huduma za afya kitu ambacho kila mwananchi anatambua hilo bila ubishi.

Ila bado vijana wanaonekana kama kundi lililosahaulika ,japo ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inasema itashughulikia swala la ukosefu wa ajira kwa vijana lakini haionyeshi kama kuna matumaini mpaka sasa.

Kutokana na takwimu za kati ya mwaka 2013 hadi 2035 yaliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), yanaonyesha kuwa idadi ya vijana walio na umri wa miaka 15-35 mwaka 2019 itakuwa asilimia 34.6 ya watu wote nchini na inataongezeka hadi kufikia asilimia 35.6 mwaka 2025.

Ongezeko kubwa la vijana tena wasio na ajira ni tishio kubwa kwa taifa linalokua kwa kasi kwa technolojia na wingi wa wasomi wakiwapo mitaani.

Ila serikali inaweza kuamua kufanya kitu maana vijana ni takribani asilimia 35 ya wa Tz wote let say Tz ina watu 50Milion vijana wanakadiliwa kuwa 15Mil ukiwaweka kwenye mafungu wale graduates wasio na ajira watakuwa chini ya 15Milioni

Wazo #1:
Ss kama serikali imekuwa na mpango wa kuzinasibu kaya masikini kupitia mpango wake wa Tasaf ,nashauri mpango kama huo uanzishwe pia kwa vijana graduates wanaomaliza vyuo wasio na ajira wawe wanapata posho kama wale wa Tasaf.

Wazo namba #2
Kama serikali yetu imekuwa ikitoa billions za pesa papo papo kupitia mheshimiwa rais kujenga mahospital na ma barabara marefu nashauri itolewe japo billion moja tu yaani moja tu then wahesabiwe graduates wote wapewe semina ya biashara na ujasiriamali kutoka kwenye mabank then wakaparanganyike mitaani.

Hii ideology nadhani inatumika sana kwa nchi za wenzetu ndio maana wao wanajeuri ya biashara sabau serikali zao zinawa support kwa mikopo kama hii.

Wazo#3
Kila kaya yenye graduates hasiye na ajira ipatiwe ng'ombe wa maziwa au jike mmoja then serikali iwe inafanya follow kuhakikisha anaendelezwa.

Au nasema uongo wadau,je kuna atakayelalamika hapo?
Maana humu Jf watu wanalia kwa kukosa ajira mpaka huruma,haistaajabishi kuona graduate natafuta ajira mshaara chakula.
 
Kweli man, pia selikali ijitaidi kuangalia na vijana walio single iwapatie pisi Kali hii itasaidia kuwapunguzia msongo wa mawazo na watawasaidia kupunguza kutuonea wivu sisi wenye pisi Kali zaidi ya moja wakati wengine wanaishia kudownload tu picha za pisi Kali
Pia ikiwezekana kila kijana apewe vile vigari vya million tano pia parking kwenye mabaa Nazo ziongezwe
 
Daah
 
Mimi naona wazo la mbunge Msukuma lingefanyiwa kazi,kwamba kama serikali inaweza kuwakopesha vijana wa chuo ambao hawana vyeti,inashindwa vipi kuwasaidia vijana ambao wameshamaliza na wana vyeti mkononi?,Hivyo vyeti vya elimu zao ndiyo ingekuwa dhamana.
 
Kweli man, pia selikali ijitaidi kuangalia na vijana walio single iwapatie pisi Kali hii itasaidia kuwapunguzia msongo wa mawazo na watawasaidia kupunguza kutuonea wivu sisi wenye pisi Kali zaidi ya moja wakati wengine wanaishia kudownload tu picha za pisi Kali
Pia ikiwezekana kila kijana apewe vile vigari vya million tano pia parking kwenye mabaa Nazo ziongezwe
Ukishapata pesa au chaneli za pesa pisi kali zitakuja tu automatically😂😂😂😂
 
namba moja itawafanya wazeekee nyumbani pia namba 3 ni impractable kwa maeneo ya mijini
Europe mbona wanatumia namba moja vijana wasio na ajira wanalipwa na hawazeekei nyumbani.

Ww haunatofauti na wazazi wanyima lift watoto wao wakiwataka watembee kwa miguu kwenda shule sababu wao walipigwa na umande nyakati zao😂😂😂

Namba tatu inawezekana tu ,ukishapewa ng'ombe utajiongeza tu .
 
Serikali iwekeze kwenye kilimo.

Vijana wa kutoka vyuo vya kilimo serikali iwakopeshe Mabilioni ya fedha kuwekeza kwenye kilimo Cha kisasa. Wawe na matrekta na visima.

Hizo kampuni zitajiri wanafunzi wenzao wanaotoka vyuoni.

Serikali iruhusu soko huria na iwezeshe masoko ya nje.

Ndani ya miaka mitano tutashuhudia mabadiriko makubwa sana.

Nchi zote zinazotuzunguka hazijazitosheleza na chakula Kama TANZANIA. Badala serikali itumie fursa hiyo kuokoa vijana wao wamekaa kupiga siasa.

Anyway acha niendelee na Mambo yangu
 
Euroe mbona wanatumia namba moja vijana wasio na ajira wanalipwa na hawazeekei nyumbani.

Ww haunatofauti na wazazi wanyima lift watoto wao wakiwataka watembee kwa miguu kwenda shule sababu wao walipigwa na umande nyakati zao😂😂😂

Namba tatu inawezekana tu ,ukishapewa ng'ombe utajiongeza tu .
🤣 🤣kwa tanzania hii bado sana
 
Back
Top Bottom