Nashauri serikali ianzishe Mfuko wa Maendeleo ya Huduma za Jamii, (Social Services Development Fund)

Nashauri serikali ianzishe Mfuko wa Maendeleo ya Huduma za Jamii, (Social Services Development Fund)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,481
Reaction score
89,898
Somo tajwa hapo juu lahusika.

Naishauri serikali ianzishe Mfuko wa Maendeleo ya Huduma za Jamii (Social Services Development Fund), mfuko huu uwe na jukumu la ku-mobilise funds za kugharamia masuala ya elimu kama kujenga shule za msingi, vyumba vya madarasa, vyoo nk

Pili, mfuko uwe unatoa pesa za kujenga vituo vya afya na zahanati pamoja na kutoa ruzuku ya gharama za bima ya afya kwa wananchi. Tukiweza hili tutaondokana na utegemezi wa mabeberu kwenye vitu vidogo kama kujengewa zahanati au vyoo au madawati kwa watoto wetu.

Serikali inaweza kuweka tozo kwenye huduma za mawasiliano, miamala ya fedha kwenye mabenki au kampuni za simu au kuwa na kodi ya kila mwezi angalau elfu 3 kwa kila mtu mzima ili kupata pesa ya kugharamia hizo huduma. Kwa kuwa makato yatakuwa madogo madogo, lakini accumulative hayatakuwa na maumivu makubwa kwa watu.

Uzoefu wa jambo hili tayari upo kupitia mfuko wa barabara, mfuko wa maji, EWURA na REA ambazo zimewezesha kuwa na pesa za uhakika kutekeleza miradi ya barabara, maji na umeme badala ya kutegemea bajeti ambazo huwa hazina uhakika.

Nawasilisha
 
Watu mnaipita hii thread kama hamjaiona,mbona haina mimba?
 
Back
Top Bottom