katima
Member
- Aug 22, 2012
- 96
- 58
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Hospital hii kubwa na ya kisasa inayojengwa huko Chanika nashauri mamlaka husika ziiite MAKONDA HOSPITAL.
WHY?
1. Ndie alie tengeneza proposal ya mradi huu mkubwa kwa ajili ya kina mama wapate sehemu nzuri ya kujifungulia.
2. Ndie alie wafuata Balozi wa Korea kuwaomba waweze kuujenga mradi huu kwa ufadhili wao.
3. Ndie alie buni muonekano wa hospital ufananaje na kisha kuwapa wachoraji waweze kuichora vizuri.
4. Ndie aliependekeza mradi huu ujengwe Chanika na sio kwingine maana amejua shida za wanachamanzi na Watanzania kwa ujumla.
5. Ndie aliehakikisha pesa iliyotengwa karibu Billion 8.8 inatumika vizuri bila kuachia mchwa au wapiga dili kuitafuna. Pesa imefanya kazi iliyokusudiwa.
6. Ndie aliehakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati tena kwa miezi michache tu hospital kubwa na ya kisasa.
7. Mpaka sasa ndie anaehakikisha vifaa vya kisasa vinakuwepo katika hospital hii ya kisasa ya kina mama.
Mh Paul C. Makonda unastahili pongezi maana weye ni mtendaji na sio mwanasiasa mtu wa kupiga maneno matupu bila Vitendo. Nakupongeza binafsi na niombee Mamlaka husika ziiite hospital hii kwa jina la MAKONDA HOSPITAL maana kijana huyu ndie mwenye Wazo hili na ndie alieombea PESA kuhakikisha HOSPITAL hii ya kisasa na kubwa inajengwa katika Mkoa anaoungoza Mkoa wa Dar es Salaam.
Niwashauri baadhi ya kakundi kadogo kanako pambana na Mh MAKONDA hebu muacheni apige kazi jembe kama hili huwezi litupa kirahisi rahisi kama mnavyofikiri. Waheshimiwa wabunge baadhi hawajafanya lolote toka wachaguliwe na wapiga kura wao kazi kubwa ni maneno na kelele nyingi. Niwashauri igeni mfano huu. Tuijenge Tanzania yetu pendwa sote kwa pamoja.
TANZANIA KWANZA.
By copy &Pest