Nash Emcee anatualika tumpokee 'shujaa'. Ni shujaa gani huyo?

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
5,417
8,820
Nash.JPG

Nash emcee, msanii wa hipHop.


‘‘Shujaa ndo amefika, na ameshinda vita,
Nami nawaalika kumpokea shujaa… ’’

Hiyo ni mistari kwenye chorus ya pini iliyotoka hivi karibuni ya Nash emcee. Track inakwenda kwa jina la ‘Shujaa’, kamshirikisha binti fulani hivi mwenye sauti tamu sana isiyochosha kutegea sikio.

Ukitia maguu ‘in ze hood’ kwenye mitaa ya Temeke, Nash emcee ana umaarufu mkubwa sana kwa watu wengi, zaidi ya ule umaarufu wa Juma Kiroboto aliyekosa Nature kwa sasa. Mitaa ya Temeke wanamfahamu kwa majina mengi kama vile Maalim Nash, Zuzu, Emcee mwenye V.V.U (Vina Vikali Usipime), na majina mengine kadhaa wa kadhaa basi ilimradi burudani tu. Ni emcee ambaye ana zaidi ya ‘HASI 15’ down the line kwenye game, tangu enzi zileee za Jay Moe akilalamika Majukumu! So, Zuzu anaielewa mitaa, analielewa sanaa. Maalim anafanya hipHop for fun & fans, not fame.

Sio Temeke pekee, bali Nash anajulikana kwa wengi in hip hop community countrywide and beyond borders mpaka jijini Nai. Kwa jijini DarSlum, goers wa kilingeni Msasani wanamnyaka vyema huyu ‘Maalim’. Machalii wa Ara pia wanampata vizuri kwenye harakati za SUA.

Hivi karibuni, Maalim Nash amepakua jiwe… ‘SHUJAA’. Ni track ambayo haichoshi kusikiliza, na katumia fasihi iliyotukuka kwenye nyimbo hiyo. Leo mishale ya jioni hivi wakati nikiwa masikani na wana kubadilishana mawili matatu ya kimaisha na kupeana ‘ramani’ za town, basi nikaplay hiyo track. Nyimbo ilipoisha, wana wote pale masikani walipata tafsiri tofauti tofauti kuhusu maudhui ya nyimbo hiyo, eventually swali likarushwa santakarawe: ‘‘Nash kamaanisha shujaa nani hasa?’’. Nikawaambia ebana eeh... hipHop usikivu, kama hamuielewi basi fuatilieni sebene. Mara ghafla wana wakaanza kujadili habari za Bashite, dakika sifuri mbele... ''Fulola Mbasha 'kaoa' kiserengetiBoy'' ikawa topic. Ile kuona ushilawadu unaanza kuteki-ova pale, aaarrgh mie nikala mguu wa kuku.

My fellow hip-hop fans, hebu sikilizeni hilo pini, kisha toa maoni yako… Je, huyo SHUJAA ni nani hasa? na ameshinda vita gani? Track yenyewe hii hapo chini attached.

HIP HOP... The good music I like most.

-Kaveli-
 

Attachments

  • Nash Mc - Shujaa.mp3
    4.3 MB · Views: 95
  • blob.jpg
    blob.jpg
    11.3 KB · Views: 81
Nash misimamo/Nash Kaskazini.

"Mc usijiite nigga...nigga kashaliwa na Mamba"


Tayari tumeshalivaa Jukwaa Mkuu.


''Ndogo zao ndogo sana, bomba yake haipiti''. hahahaa ama kweli Maalim Nash ni zuzu.

Nash IS.

Karibu jukwaani mkuu .

-Kaveli-
 
''...wachezaji hoi, yani chama langu awamu hii hatuna kocha,
Benchi lake la ufundi kila mmoja analopoka,
Nani wa kuyasema na wenzio wanaogopa kambini weshatoroka... ''

hahahaa Emcee Nash a.k.a Zuzu

-Kaveli-
 
''Ndogo zao ndogo sana, bomba yake haipiti''. hahahaa ama kweli Maalim Nash ni zuzu.

Nash IS.

Karibu jukwaani mkuu .

-Kaveli-
"Wanyonge wakichoka wanageuka waasi bila wasiwasi wanazama msituni na vita ya kudai haki"
-Oya kaka suma wachaa UPUMBAVU wako-

"Pele mchawi wa Soka Nash mchawi wa mistari"


Mkuu hapo juu ni utangulizi kwanza.

Wacha tukae Sasa mkao wa kuchambua "Shujaa wetu"
 
Nitaachaje kwa Mfano..?
Haha Nazo ngoma kibao za Nash Mc mpaka Kero!!!


Hii ngoma nimeshaisikia vilivyo ila inachangamoto kuing'amua.


Mkuu, hii ngoma nilikuwa masikani na wana, tumeachana pale bila kuing'amua. Kila mmoja kasepa na tafsiri yake.

I like this kind of hipHop. Unasikiiza nyimbo unarudia mara mbili mbili ili kunasa maudhui yake.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom