Nasema hivi, Mume anauma!

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,981
5,438
Nimemulika mwizi!!! Fakeni kabisa

Miaka yote nasikia mume anauma mume anauma nikawa nasema wanaume hawa walivyo wengi anauma nini bwana?? Leo yamenikuta.

Kama mwezi umepita nilikuwa nahisi naibiwa. Kuna ile female intuition tu unajua hapa tuko watatu kwenye huu uhusiano.

Sasa mi si ndio mtaalamu wa IT, nikafanya timing karibu wiki 2 hadi nikafanikiwa kuweka mtego wangu. Lahaula nimekutana na mke mwenzangu mtoto wa 2000.

My analysis of the situation;

Binti sio mtaalamu wa masuala ya kula waume za watu. Sio kwamba namu-underestimate, najua ana power yake. Ila nashukuru Mungu hayuko at war, anatreat huu uhusiano kama mwingine wowote yaani anamuona kama mpenzi wake peke yake. She is at ease.

Nilichofanya ni sijataka mambo yawe mengi, nimemtafuta ex wangu mmoja anapenda chini, anapenda watoto wenye rangi za Mtume maana hata mi alinifatiaga hicho hicho. Nimempa namba, jina, anapopatikana na nimempa pesa (kwa hasira nimemuomba huyu huyu anayenitia hekaheka) amuachanishe huyu mtoto kwa my wangu. Nimemwambia amchanganye apeleke hata posa mi nitagharamia.

Ubaya wa issue hizi bwana yaani tangu nimejua kama wiki 2 zilizopita kila anachoniambia naona uongo. Akijifanya kutaka kukulana namwambia niko period. Hadi jana kauliza “period haiishi?” Nikamwambia “nina stress labda imesababisha”. Akale huko huko nje aache uroho, alaaa…

Sometimes nikioga nalia sio utani. Mume anauma kweli!
 
Kwa kuwa umesema, huyo dada sio mtu wa kukwapua wanaume za watu, na kwa mumeo imetokea kibahati mbaya na hajui km baba ni mume wa mtu.

Basi muitee huyo dada na umpe onyoo kalii, naamini atamuacha chibaba wako.

Hiyo njia unayotaka kutumia, uta fail na uta fail haswaa, niamini mie.

Usijesema hukuambiwaa. Poleeeee sanaa.
 
Kosa unalo fanya ni kuficha Mali.
Toa Mali tena kipindi hiki ungeitoa kwa mwamba kiukweli kweli kama paka shume la bar.

Ila naona mwamba ndio anashinda maana kwako kalamba na huko anaenda kulamba, akimaliza anarudi kwako anakulamba tena, ukikataa atasema ataweka Siri kwa mwamba.
 
Kwa kuwa umesema, huyo dada sio mtu wa kukwapua wanaume za watu, na kwa mumeo imetokea kibahati mbaya na hajui km baba ni mume wa mtu.

Basi muitee huyo dada na umpe onyoo kalii, naamini atamuacha chibaba wako.

Hiyo njia unayotaka kutumia, uta fail na uta fail haswaa, niamini mie.

Usijesema hukuambiwaa. Poleeeee sanaa.
Anajua kuwa ni mume wa mtu. Anajua vizuri tu.

Ila kwa mawasiliano yao, sio mwanamke aliye na nia ya kuvunja ndoa au ambaye yuko na mume wa mtu kikazi zaidi. Yuko tu kutaka faraja na mapenzi kama mahusiano mengine yalivyo.

Kwanini nitafeli cocastic?? 😭
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom