Nasari kupoteza ubunge wake kama Lema

Nasari kupoteza ubunge wake kama Lema

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Posts
6,157
Reaction score
4,454
Tetesi za uhakika kutoka ndani ya CCM ni kwamba kuna timu ya watu Tisa(9) wamepewa kazi ya kutafuta na kukusanya ushahidi wa maneno machafu yaliyotumika wakati wa kampeni, ili ifunguliwe kesi kupinga ushindi wa Nasari kwa madai kwamba mpinzani wake alisingiziwa kwamba ni shoga ilihali si kweli hivyo kupoteza mvuto kwa wapiga kura.

My take. Kama alivyodai mwana CCM mmoja kwamba nia yao kubwa siyo kwamba wanataka uchaguzi urudiwe ili washinde, nia yao kubwa ukiachilia mbali kwamba wanasahaulisha CHADEMA kujipanga namna ya kupambana ipatikane Katiba mpya iliyo bora pia ni kukifanya CHADEMA kiwe busy na masuala ya kesi na kutumia rasilimalizao chache zilizopo kughalamia michakato ya chaguzi ndogo ili ifikapo mwaka 2015 wasiwe na resources za kutosha kukabiliana na CCM.
 
well, u can expect anything from him! ishu ni hao wanaoburuzwa wanakubalije kuburuzwa?
 
hawatapata kitu hapo. nasarri yeye binafsi hajawahi kuongea lugha ya matusi kama ni hilo imekula kwao ccm.
 
Waanze na lusinde na naona ccm wanajichimbia kaburi wenye kwa wanayoyafanya wanatutia sn hasira wananchi
 
hamna kitu. CCM ndo inalikaribia kaburi.

Mkuu lakini hizo mbinu hata mimi naona zitasababisha CHADEMA isijipange vema ku-deal na mambo mengine mda mwingi itautumia kuhangaika masuala ya kesi za uchaguzi na chaguzi ndogo
 
hawatapata kitu hapo. nasarri yeye binafsi hajawahi kuongea lugha ya matusi kama ni hilo imekula kwao ccm.

Hivi ni lazima awe ameongea yeye mwenyewe au hata wapiga debe wake??
 
CDM ni nguvu ya umma tutashinda tu kwa lolote, na bado moto utawaka wataachia ngazi wenyewe!!!
 
Mkuu lakini hizo mbinu hata mimi naona zitasababisha CHADEMA isijipange vema ku-deal na mambo mengine mda mwingi itautumia kuhangaika masuala ya kesi za uchaguzi na chaguzi ndogo

vise versa ni kwamba, wanapelekea CDM ku-buy trust kwa wapiga kura zaidi na zaidi.
Sasa kama wanawapotezea mda kwa kesi while tendo hilo linaongeza mtaji wa kura kwa CDM watakuwa wao ndo wanajipotezea muda na mtaji wa kura.
wanachokifanya CCM ni sawa na kukata tawi la mti walilolikalia wenyewe.
 
Kama matusi yanachangia kushinda, mbona wao hawkuishinda?.Kama kutukama walitukana!!!!
 
Hakuna mafanikio katika maji taka bali ni kuzidi kunuka. Gamba lenyewe limewashinda.

Kinachoniuzi ni maamuzi ya kuamua kukimoa chama bila kujari ghalama za uchaguzi hebu fikiria mabilioni yatakayotumika Arusha kumrudisha tena Lema Bungeni.
 
Back
Top Bottom