Nasalimu amri, watoto wangu nawarudisha shule za serikali

mandokwa

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
620
865
updates...
Asante Georgina kwakukubali... but kuna mambo nitaendelea kuwa makini hasa kuhusu tabia zako.... tulianza wote...lazima tumalize wote
============================================

Kwako Mke wangu Georgina,

Nashukuru kwa upendo wako ambao siku zote umenionesha. Nikweli nilikuahidi maisha ya amani na upendo, lakini pia nilikuahidi watoto wetu watasoma elimu ya english mediam ili wasipate taabu kujua lugha japokuwa sisi wenyewe tumesoma shule za serikali.

Georgina samahani nilikudanganya mambo mengi sana kuhusu uwezo wangu binafsi. Hii yote kwakua wazazi wako na wewe mwenyewe mlinidanganya mkajiweka juu sana kumbe hali tunafanana tu.

Kiukweli sikuwa na investiment zozote hapa mjini bali wafanyabiashara wengi walikuwa wananilipa fidia kwa kuwaunganisha kwenye tenda kadhaa. Kulingana na cheo changu nilikuwa na power ya kuamua nani apewe mkataba fulani kwani boss wangu alichojali ni kumpatia fungu lake unakumbuka tulipoamia Mwanza nilimnunulia boss gari toyota harrier new model, pesa zile hazikuwa zangu ni gawio lake.

Naomba unisamehe kwani tangu mwaka huu uanze nilichukua mkopo ili kukidhi matakwa ya taswira yangu hapa mtaani na kwako kwasababu ofisini mianya imefinywa nilitarajia itafunguka baada ya nguvu ya soda ya mkulu wetu lakini kulingana na hali inavyokwenda naona uelekeo huo ni mdogo na makato ya mkopo yananiua zaidi. Napata uchungu kukuambia kwamba sitaweza kuhimili mikiki mikiki ya mjini na naamua kufanya yafuatayo:-

1. Kuanzia leo tutashare usafiri kwenda na kurudi kazini

2. Watoto wakirudi likizo ya term hii tunawahamishia shule ya serikali...nimeongea na mwalimu kumbe shule mzuri tu inafaulisha na kuna walimu wa kutosha... by the way english ni lugha kama lugha zingine tu.

3. naomba tujilimit michango ya mchungaji... kwanza jiulize hii michango anaifanyia nini? kama ni baraka mbona jesus hakuchangisha kalamu?

4. Tujibidishe kujichanganya na jamii maana lolote likitufika hawa ndio watakao tuokoa.

Haya niliyoandika sio mtazamo ni maamuzi. Kama uliolewa kwa mapenzi nitashuhudia utekelezaji wako. Nakuahidi tutavuka tu baada ya miaka mitano ya mpito...

Nasisitiza watoto hakikisha unatafuta majibu mazuri kwa watoto kwani sipendi waathirike katika hili.

Najua umeelewa mambo mengine tutaongea jioni nikirudi..

With love and care,

Mandokwa
 
Georgina kuja haraka sana hapa, mme wako ameamua kuanika maisha yenu hapa jukwaani amehisi hapa ndio kuna suluhisho, ila kamkumbushe kuwa yeye ni mwanaume hapaswi kuanika anika apambane.
 
CK ALIYEKUWA WA WEMA SEPETU ANAUZA CHIPS SASA ACCORDING TO SHIGONGO. JIANDAE VIZURI MKUU.
 
Mmmh Magu Kweli kiboko. Mimi nilisoma shule Ya serikali na sasa nina position nzuri tu. Kikubwa
Ni kuwahimiza watoto kuwa elimu ndio
Kila kitu either waipate chini Ya mtu wa
Muembe au IST.
Asante Mkuu nimeliona hilo ndio maana nimeanza mapema maana tunakoelekea...nikiendekeza sifa zakijinga nahisi balaa.
 
Kwako Mke wangu Georgina,

Nashukuru kwa upendo wako ambao siku zote umenionesha. Nikweli nilikuahidi maisha ya amani na upendo, lakini pia nilikuahidi watoto wetu watasoma elimu ya english mediam ili wasipate taabu kujua lugha japokuwa sisi wenyewe tumesoma shule za serikali.

Georgina samahani nilikudanganya mambo mengi sana kuhusu uwezo wangu binafsi. Hii yote kwakua wazazi wako na wewe mwenyewe mlinidanganya mkajiweka juu sana kumbe hali tunafanana tu.

Kiukweli sikuwa na investiment zozote hapa mjini bali wafanyabiashara wengi walikuwa wananilipa fidia kwa kuwaunganisha kwenye tenda kadhaa. Kulingana na cheo changu nilikuwa na power ya kuamua nani apewe mkataba fulani kwani boss wangu alichojali ni kumpatia fungu lake unakumbuka tulipoamia Mwanza nilimnunulia boss gari toyota harrier new model, pesa zile hazikuwa zangu ni gawio lake.

Naomba unisamehe kwani tangu mwaka huu uanze nilichukua mkopo ili kukidhi matakwa ya taswira yangu hapa mtaani na kwako kwasababu ofisini mianya imefinywa nilitarajia itafunguka baada ya nguvu ya soda ya mkulu wetu lakini kulingana na hali inavyokwenda naona uelekeo huo ni mdogo na makato ya mkopo yananiua zaidi. Napata uchungu kukuambia kwamba sitaweza kuhimili mikiki mikiki ya mjini na naamua kufanya yafuatayo:-

1. Kuanzia leo tutashare usafiri kwenda na kurudi kazini

2. Watoto wakirudi likizo ya term hii tunawahamishia shule ya serikali...nimeongea na mwalimu kumbe shule mzuri tu inafaulisha na kuna walimu wa kutosha... by the way english ni lugha kama lugha zingine tu.

3. naomba tujilimit michango ya mchungaji... kwanza jiulize hii michango anaifanyia nini? kama ni baraka mbona jesus hakuchangisha kalamu?

4. Tujibidishe kujichanganya na jamii maana lolote likitufika hawa ndio watakao tuokoa.

Haya niliyoandika sio mtazamo ni maamuzi. Kama uliolewa kwa mapenzi nitashuhudia utekelezaji wako. Nakuahidi tutavuka tu baada ya miaka mitano ya mpito...

Nasisitiza watoto hakikisha unatafuta majibu mazuri kwa watoto kwani sipendi waathirike katika hili.

Najua umeelewa mambo mengine tutaongea jioni nikirudi..

With love and care,

Mandokwa
221afea04327f5b7dd19d5b9044c16d7.jpg
 
Umeandika kama wewe lakini nakuapia umewakilisha mawazo yetu wengi hapa hata kama hawatakiri hivyo.
Watumishi wa umma walioko mawizarani na kwenye halmashauri na taasis nyingine za umma wote wanaguswa na posti ya huyu jamaan. Sasa hivi kuwalipia ada watoto huko english medium ni ishuuuu. English medium itabidi zipunguze ada laa sivyo zitafungwa
 
Back
Top Bottom