Nasaha

Nasaha

chew

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
229
Reaction score
143
*MASIKINI HIVI PUNDE TU TULIKUWA NAE.*
.
[emoji733]...Alikuwa ni mtu mwema na mwenye bashasha na kila mtu..
Nani ambae alikuwa hamjui kwa ukarimu wake..alikuwa ni mtu nadhifu na kipenzi cha watu wengi..

[emoji733]Imam Ghazal ra anasema kuwa mauti yanatisha sana lakini wengi tumeghafilika nayo.
Wengi wetu hatuyaongelei mauti huku nyoyo zetu zinafikiri mengine..na hilo halitusaidii sana..

[emoji733]Yampasa mtu atenge muda kutafakari mauti kwamba yanamkabili..mtu anapaswa kuwafikiria rafiki zake aliowazika azikumbuke sura zao na malengo yao mengi waliyokuwa nayo..

[emoji733]Mtu yampasa kutafakari jinsi wake zao walivyokuwa vizuka..watoto wao walivyokuwa Yatima..mali zao zilivyogawiwa.na nguo zao walizoziacha bila kuzivaa...

[emoji733]Yampasa mtu kufikiria mauti kwamba wakati wowote nae yatamfika kama hayo yaliowafika rafiki zao..

[emoji733]..Ghafla sauti inasikika..kwa masikitiko...
...masikini masikini.
..fulani amejifia

Watu wanashona sanda
Upo juu ya kitanda..

Wanalia wanalia
Jerani na baadia...

[emoji733]Msafara wako katika Ulimwengu wa Barzak ..unaandaliwa huku..watu wakisemezana...
..Ah...
MASIKINI HIVI PUNDE TULIKUWA NAE...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom