PostGE2025 Nasaha za Mzee Kamara Kasupa kwa Samia

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
11,811
Reaction score
18,054
KUNA MAMBO YAKIPOTEA HAYAWEZI KUREJESHWA.
“KWANINI SAFARI HII HALIPO TENA GOLI LA MAMA WALA SIMU YAKE?”

Naanza na kuwauliza washabiki wa Simba na Yanga, imekuwaje safari hii kusiweko tena simu itokayo kwa MAMA, inayowatia moyo wachezaji na washabiki na viongozi, ikionyesha kwamba kuna mshikamano kati ya uongozi wa juu wa nchi na wananchi?

Hata kwenye vijiwe vya kahawa sisikii washabiki kutamka goli la mama! Wahenga walisema maji yakimwagika hayazoleki. Hili liwafunze wale waliojitoa ufahamu wakaingiza ushabiki kwenye eneo la siasa na utawala, wakidhani wanaposhabikia upotofu wanamsaidia mtawala.

Kuna mambo ambayo yakipotea hayarejeshwi kwa namna yoyote. Kuna mambo ambayo mwanasiasa akiisha kuyapoteza hawezi kuyarejesha, Waingereza wanaita “reputation” hili ni neno linalobeba maana ya staha, hadhi, heshima, kuaminika na kukubaliwa na jamii. Hao Waingereza waliotutawala na kutuanzishia mfumo wao wa kisiasa na kiutawala mwanasiasa wao akipoteza “reputation” hulazimika kujiuzulu, kumpisha mwingine. Kwasababu kuna gharama nyingi za kuongozwa na mtu aliyepoteza staha na heshima yake kuendelea kukalia kiti cha uongozi huku akiwa haaminiki wala haheshimiki.

Hapo zamani za kale alikuwako mwanamama aliyeitwa Samia Suluhu Hassan, alikubaliwa na wengi akiaminika kwamba kitokacho kinywani mwake ni kweli. Msemaji wake aliyeitwa Gerson Msigwa aliwaunganisha wananchi waliohudhuria uwanjani siku ya mechi muhimu ya kimataifa, kuisikia sauti ya MAMA akiwatakia heri wachezaji na watazamaji, hata waliotazama mechi kupitia Runinga, nao waliyaisikia maneno ya MAMA. Sijui miaka mingapi imepita maana hayo sasa yakikumbukwa na kusimuliwa yanafanana na hadithi za hapo zamani za kale.

Zamani hizo mazingira ya “Harmony” yalikuwa bado hayajaharibiwa, neno hili lina uzito wake ambao Kiswahili hakikidhi, wacha niite mshikamano ama “solidarity”. “Harmony na solidarity” ingawaje hayaonekani, hayashikiki wala hayana umbile bado yanaishi na yana umuhimu wake kwa Taifa linalojitambua. “solidarity” ndiyo iliwezesha Watanzania kushinda vita vya Kagera mwaka 1978, Nyerere alipotangaza kwamba “sasa tunayo kazi moja tu nayo ni ya kumpiga mvamizi ili ajue Tanzania ni ya watu.” Wakulima walichangia maharage yao kwa moyo mweupe wakisema wapelekeeni vijana walio kwenye uwanja wa mapambano. Wafugaji walitoa ng’ombe na mbuzi zao kwa moyo mweupe wakisema ndio mchango wao, mboga kwa wapiganaji. Hakuna aliyechangishwa kinguvu, wapo waliochangia mchele, unga, wengine walitoa jogoo kama mboga kwa wapiganaji wanaoipambania Tanzania yetu. Wapo matajiri waliotoa Malori yao kwa hiari zao Malori yatumike kubeba wapiganaji ama kubeba mahitaji yao, hasa ya chakula. Wananchi walijua ile haikuwa vita ya serikali bali vita ya wote, kwahiyo walitakiwa kufanya kila linalowezekana kumtoa nje mvamizi.

Nyerere hakutawala watu wajinga kama kizazi cha sasa kinavyoaminishishwa na hao waliofeli somo la uongozi. Nyerere alitawala watu waliomwamini na kumheshimu, kwasababu kamwe Nyerere hakuthubutu kucheza “to tamper” na hayo mawili “harmony” na “solidarity”. Nyerere alijua kwamba TANU wakati inapigania uhuru haikuwa na fedha, iliungwa mkono na maskini, kwahiyo alitumia rasimali watu kuzunguka nchi nzima akieneza ujumbe wa TANU kuhusu uhuru wa Tanganyika. Nyerere alipokwenda kila mahali ndani ya Tanganyika, alifikia kwa watu, alilala kwa watu hakulala Guest, wala kula Hotelini, alikula kwa watu na kuketi nao kama ndugu.

Hata baada ya uhuru kupatikana bado Nyerere hakubadilika, hakuthubutu kuwafanya watu waone kwamba madaraka aliyo nayo yamemtenganisha na wananchi, yakimfanya awaone hao wananchi aliowaongoza kuwa maadui wanaomlazimisha aishi kwa kujihami. Hapana! Nyerere aliendelea kuiishi imani ya TANU kwamba “Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.” Nyerere aliendelea kuzunguka nchi nzima mijini na vijijini kwa gharama za dola lakini kushirikiana na wananchi wa vijinini kufanya kazi za mikono. Hapa nimekosa picha ya Nyerere akiendesha Toroli, namwomba kaka Livingstone Ruhere na Muhidin Michuzi wanisaidie kuiweka picha hiyo kwenye ukurasa huu, ili picha ya Mwalimu iendelee kusomesha.

Kwasababu “hapo katikati” eneo letu la utawala limevamiwa na watu wanaofanana na wale waliouza njiwa na kubadilishaji fedha waliofanya biashara Hekaluni. Yesu aliwatoa nje kinguvu, akamwaga fedha zao chini, akiwaambia “mmeigeuza nyumba ya Baba yangu iwe pango la wanyang’anyi”. Hapo katikati IKULU yetu imevamiwa na watu ambao wameondosha kabisa thamani, heshima na utakatifu unaopaswa kuwako IKULU.

Kwasababu wamegeuza madarakani liwe eneo la kukidhi haja za binafsi na kuzima kiu zao. Matokeo ya kutoheshimu UTAKATIFU wa IKULU yamemfanya mtawala kukosa nguvu kutoheshimika wala kutoaminika! Tumekuwa na serikali inayopwaya katika mengi, mwisho wake itahatarisha amani na usalama wa nchi.

Hakuna linalofichika, Samia amezungukwa na washauri wabaya, angalia anavyofanya uteuzi mbaya, akiwateua ndugu zake wa damu na kuwapa nyadhifa kubwa! Binamu yake Yusufu Masauni alimpa Uwaziri wa mambo ya ndani, Mkwewe Mchengerwa naye akampa wizara, hatimaye amemteua mwanawe wa kuzaa Wanu, amekuwa Naibu wizara ya elimu. Eti huyo Wanu akiwa Bungeni awe ndiye anajibu maswali ya wabunge yanayohusu Elimu yetu! Kiuhalisia huyu atakuwa anatoa majibu kutoka kwa mama yake mzazi, yale wanayojadili wakiwa sebuleni! Hii ni dharau ya hali ya juu. Kweli Samia hajawaona Watanganyika wengine wanaoiweza nafasi hiyo hadi ampe mwanawe wa kuzaa? Nyerere hadi anastaafu mwaka 1985 hakuwaacha akina Makongoro wakiwa madarakani wala hakuwapa nyadifa kubwa! Serikali kuu ikivaa sura ya kifamilia kamwe haitaheshimika. Mbaya zaidi hao akina Wanu hawasomeshi watoto wao kwenye shule wanazosoma watoto wa Watanganyika wengine, bali wanawasomesha nje kwasababu wanajua katika Tanzania serikali imeua elimu. Vinginevyo ajitokeze mjukuu wa Samia anayesoma na Watanzania wengine humu nchini?

Watu wanaowaepusha watoto wao na shule wanazosoma Watanzania (wanaotawaliwa), wanaozikwepa Hospitali zilizoko nchini wakienda kutibiwa nje, wasioziamini Benki za Tanzania wakificha dola zao kwenye Benki za nje, hawawezi kuwa na uzito wa kuitwa viongozi wa Watanzania. Kwahiyo nauweka wazi ushauri wangu kimaandishi ili uwe kumbukumbu itakayodumu kwenye Historia ya nchi yetu. Ikiwa wewe Samia utauzingatia utanufaika kwa matunda yake na ukiupuuza pia utaonja matunda yatokanayo na maasi yanayotokota, yanayosubiri kulipuka. Hao wanaotaka ujiuzulu hawawapi Watanzania ushauri mzuri, nitaifafanua kwenye makala nyingine na kuziweka wazi athari zake, lakini pia huo moto wao wanaokutaka ujizulu utakapowaka hakuna atakayeuzimisha. Kwasababu utakuwa endelevu.

Samia irudie historia ya Tanganyika, waulize hao unaowaamini kwanini Nyerere mwaka 1962 alijiuzulu ghafla nafasi ya Uwaziri Mkuu akiwa amekaa madarakani siku 42 tu? Kwa sababu aliukubali ushauri wa Oscar Kambona, walipata taarifa za fukuto la baadhi ya Waislamu wasiomkubali, waliopanga kupitia kuitisha Kamati kuu ya TANU, ifanye kikao cha kumjadili, hatimaye kumfukuza kwenye chama. Kambona akaona Tanganyika nayo ingeingizwa hatarini kuwa na mgogoro kama Congo, akamshauri Nyerere ajiuzulu ili “kuwa – pre empty” hao waislamu wenye hasira naye. Kambona akamwambia ukiniteua mimi bado moto hautazimika, mteue Mwislamu mwenzao Rashid Mfaume Kawawa atajua jinsi ya kuwazimisha. Nami nakushauri ufanye yafuatayo ili kujinusuru wewe na pia kuinusuru nchi. Kwanza vunja Baraza lako la mawaziri, ukifanya ushupavu wa kuendelea nalo, hatimaye maasi yataenea nchi nzima nawe utajikuta umebaki Rais wa IKULU tu, siyo Rais wa nchi.

Pili vunja Bunge kwa kutumia madaraka uliyopewa na katiba, kwasababu wabunge wa sasa siyo wawakilishi halali wa wananchi, maana hawakushinda, kwakuwa walishinda pasipo kushindana.

Tatu ukimaliza hayo unda serikali ya mpito na uwaambie wazi Watanzania na Jumuiya ya kimataifa wasitishe kwanza hayo wanayotaka kuyafanya ili kuipa muda hiyo “transitional Government” kuwaelekeza wananchi kwenye Tanzania mpya. Achana na udanganyifu wa kuunda Tume! Kwasababu hiyo Tume haitaaminika na wananchi wenye hasira na wenye uchungu wa kufiwa na wapendwa wao.

Hujachelewa kati ya leo na “Disemba tisa” kuna siku 14, hizo ni nyingi, zinatosha kuleta NUSRA.
 
IMG-20251125-WA0056.jpg
 
Samuya hawezi kutuundia watanganyika serikali ya mpito. Serokali ya tutaunda wenyewe.
 
Kama hawezi kuzingatia ushauri wenye hekima kama huu, basi hili litakuwa ni lile SIKIO LA KUFA LISILOSIKIA DAWA, yaani lazima life. Atakuwa na mwisho mbaya wa kutisha.
 
Back
Top Bottom