Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,027
- 20,414
NASAHA NA TARATIBU ZA UKEWENZA
1. Ukiwa katika ukewenza kumbuka kuwa hiyo ni ibada. Chunga adabu za ibada hiyo.
2. Chukua lililo haki kwako na jiepushe na kudhulumu haki za wenzako
3. Usiibe zamu ya mwenzako, usimtumie mume siku ya zamu ya mwenzako. Tafadhali, tumia siku za zamu yako vizuri na mwachie mwenzio aitumie zamu yake.
4. Usiwasiliane na mumeo akiwa kwa mwenzio hususan kuanzia maghrib, ila pakiwa na dharura. Simu na messages za mapenzi zitume mchana au muda wa zamu yako. Unapozituma usiku unamhamisha mume kiakili hivyo anakufikirie wewe tu. Huu ni wizi wa zamu
5. Usimlishe mumeo chakula cha kushiba, usimuogeshe au kumpa massage au singo mumeo siku isiyo zamu yako. Mwache mwenye zamu ayafanye hayo, naye ana haki nayo.
6. Ondoa athari zako kwenye mwili wa mumeo akiwa anakwenda kwa mwenzio mfano nywele zako. Jitahidi.
7. Usijisifie juu ya uyapatayo kwa mumeo au umfanyiayo mumeo mbele ya mke mwenzio au watu wa karibu yake
8. Usifurahie madhaifu, makosa na mapungufu ya mkemwenza. Utakuja kujaribiwa na wewe na kwa hayo hayo.
9. Usiruhusu mumeo akupendelee jambo, hiyo ni dhulma. Ukiruhusu hilo jiandae nawe kushuhudia mwenzio akipendelewa hivyo hivyo au zaidi
10. Usimruhusu mumeo ataje habari za mke mwenzio iwe ni mazuri au mabaya. Jua kuwa habari zako pia atazitaja akiwa na mke mwenzio.
11. Usichunguze maisha ya mke mwenzio, kisha usishindane naye. Ishi maisha yako kama kawaida yako.🌹pokea