Nasaha kwa binti yangu siku ya send off | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasaha kwa binti yangu siku ya send off

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Magane, Oct 14, 2012.

 1. M

  Magane Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nataraji kumuaga binti yangu natafakari maneno gani yanafaa siku hiyo bila ya kuwachosha na kukwepa boredom kwa wageni kwa hotuba ndefu.Naamini wana jamii mnaweza kunisaidia maneno ya hekima yenye mshiko na msaada kwa binti yangu kwa maisha yake ya ndoa.Tafadhali naomba mchango wenu wa nasaha.
   
 2. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  kiukweli sijui kama naweza kukuekea maneno mdomoni ama kukusemezesha ili uyatoe kama hotuba. to me naamin ili uweze kusema mbele za watu lazima uijue audience uliyo nayo na mwanao ni mtu wa aina gani. ukishajua wageni wako ni wa aina gani basi ili usiwachishe ongea kwa namna ambayo wao wanatazamia wewe uongee hilo usiseme uongo ila sema lile ambalo ni lakweli kwenye maisha basii.

  mfano waweza kwenda na taa ya chemli ukaiwasha kisha ukampa mwanao ukamwambia mwanangu sina meng ya kukueleza ila kama uoanavyo taa hii inavyowaka basi nategemea wewe ukawe nuru huko uendako, kawashe nuru ya uendo, furaha, amani, busara , mafanikio, na ucha mungu. daima kumbuka kwamba watu huangalia matunda kutoka kwako kama hawaoni mataunda basi hawana haja na wewe...........Mungu pekee ndiye anae angalia moyo na daima sisi hatuwez kuusoma moyo wa mtu.

  ukamaliza kisha ukakaa. Pia kumbuka maneno ya ukaumbini si kitu siku zote sema na mwanao chumban hadi akuelewe usimsukume kuhangaika kwa mafundi masaa yote bali mweke ndani sema nae juu ya maisha ya ndoa changa moto na furaha zake ki undani usimwache asijue kitu mweleze aamue yy kusuka ama kunyoa. usimtishe ila mweleze possibilities zote na mwambaie kabisa kuamua ni yy.
   
 3. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,336
  Likes Received: 6,684
  Trophy Points: 280
  maadam ameamua kuolewa awe tayari kulala bila nguo!...ongezea hii kwenye hotuba yako!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Binti yangu, suwasikilize watu wanaosema ndoa ni kuvumilaiana, si kweli. Kuvumilia ina maana kila linapotokea tatizo unavumilia, hiyo haitasaidia kuondoa tatizo. Tatizo likitokea, sema na mumeo ili mlitatue, ukivumilia matatizo yatawazoea na kwua sehemu ya maisha yenu. Ndoa si kuvumilia, bali kuelezana ukweli tatizo linapotokea.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  maneno marefu yanachosha mno

  kuwa short
  nukuu biblia au quraan....

  anza na hiyo nukuuu
  hakikishani dakika tatu tu......

  usimkeemeee.kuwa kind kidoogo

  na umuage kwa maneno matamu hivi....
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mtakie heri tu, na mkumbushe kuendeleza mazuri uliyomfundisha.
   
 7. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Aleleleleeeleeeeeeeeeeeee! Dada huyo!!! Anaolewaaaa! Kwanza nikupongeze kwa kukuza, malezi yamejibu warudishiwa heshima!!!! HAKIKA WASTAILI HONGRA!!!!!
  Mi nakushauri kwanza ufanyie kazi hisia, sabubu chochote ukikisema kwa hisia watu watakikubali, ufike keti ulie kidogo, kigugumizi. (Mbinu za public speech)

  Pili kabla ya wosia hakikisha kwanza UNAMSHUKURU BINTI YAKO KWA HISIA KALI!!! "Mwanangu kabla ya yote napenda nikushukuru kwa kunirudishia heshima mimi kama mama yako, kwa kujitunza mpaka umempata mwenzio kwenye hii dunia yenye vishawishi vingi. Umepambana mpaka mwisho na kunistiri mzazi wako! ( Kimya cha vikwikwi kidogo na chozi la kizushi)

  Tatu mpe wosia mmoja tu wa maana. "Mwangu wewe nimekulea mwenyewe sina shaka lolote na wewe, najua ni binti mzuri, tabia zako nazifahamu ni za kuridhisha, wema na ukarimu uliokuwa nao hapa uende kuuendeleza huko pia, Mshike sana Mungu, lolote likikutatiza au kulifurahia jawabu utalipata kwa biblia!!! (Quote vifungu viwili vitatu) sisi wazazi wako tutakupenda daima!!! baaaaaaaasss

  Ukimaliza hapo wapambe fasta fasta na khanga, huku dj akisababisha kitu cha NANI KAMA MAMA cha Boni Mwaitege, mnapiga na picha ya pamoja na mwanao huku mnafuta vichozi vya kishkaji( japo ulimlamba miko ya kutosha alivokuwa akileta za kuleta jikoni! lol!)
   
 8. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,746
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  mwambie bintiyo kuwa mjenzi wa nyumba alikuwa na akili timamu,ndio maana akaweka mlango wa chumbani,bafuni,sebuleni na hatimaye geti la nje la nyumba,lengo halikuwa jingine bali yasemwayo chumbani huishia kwenye kitasa cha mlango,yakivuka yatakuwa yasebuleni,na yasebuleni lazima yaishie humohumo sebuleni!

  Mwambie ulimi ni hatari,awe na mdogo!
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Nadhani kipindi hiki bado yupo kwako ndio muda wa kumpa Nasaha jinsi ya kuishi vizuri na mume wake, siku ya Send off, mtatakie heri na mafanikio kwenye ndoa yake mungu amjalie kizazi kizazi bora.
   
 10. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,012
  Likes Received: 3,197
  Trophy Points: 280
  Mkwe wako naye yuko humu anasoma. Akiona umebebelea taa tu, tayari kishakujua id yko. Atajaribu kukutongoza kwa pm kutest ka we ni mkwe material.
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  usisahau kumwambia 'ukiolewa hakuna kulala na nguo ' lol
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Lara1 safiii

   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Ushauri mzuri

   
 14. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,078
  Likes Received: 7,295
  Trophy Points: 280
  Kama mumewe atakuwepo basi we chimba biti kali kwa huyo mumewe,

  Mwambie hujamzalia punching bag hivyo ujinga ujinga against mwanao hupendi kabisa.

  Ongea hivyo ukiwa ukekunja ndita na ngumi, halafu uwe pia unamnyooshea kidole huyo jamaa ukiwa.

  Kwa kufanya hivi hutakaa usikie kesi au mashitaka kutoka kwa mwanao baada ya ndoa.
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  mwanamke wewe wafiti angle zote
   
 16. n

  nanasi85 Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bilateral kusahau.... Asante, Samahan, pole ni msaada tosha katika maisha ya kila Siku kwa mumewe na jamii imzungukayo.... asiaahau maneno hayo!
   
 17. n

  nanasi85 Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I min bila hapo bilateral na hapo asiaahau min asisahau.
   
Loading...