mind ur business
JF-Expert Member
- Dec 27, 2018
- 416
- 419
1. Kijana wangu mwanamke naye ana moyo kama wako, usimnyanyase kisa hawezi kupigana na wewe, mpe upendo kwasababu Mungu kasema tupendane.
"Mpige na upendo mwanamke wako na siyo ngumi. Kwasababu upendo hujenga ila ngumi hubomoa."
2 Kijana wangu mwanamke kuwa mnyenyekevu na mwenye heshima kwako siyo ndo iwe tiketi ya kumdharau na kufanya jambo baya huku ukidhania atachukilia poa tu eti kwasababu anakuheshimu, huenda ujinga wako ukaleta mpasuko katika penzi lenu.
"Tumia akili katika kuishi na mwanamke kama Mungu alivyotuagiza."
3. Kijana wangu mwanamke naye huwa anachoka Kwasababu ana mwili Kama wako, muda mwingine msaidie kazi ndogo ndogo au mpe muda apumzike, siyo punda mwenzako, sawa?
"Kuchoka hakuchagui kama wewe unachoka hata mwanamke huchoka pia."
4. Kijana wangu najua wanawaume tamaa yetu ipo machoni na huo ndiyo udhaifu wetu ila hiyo isiwe tiketi ya kufanya ujinga kumbuka uaminifu ni jambo la Maana.
"Tamaa ipo kila siku, ukisema tamaa za mwili zikushinde kila wakati basi fahamu mwisho wako na huyo mwenzako utakuwa mbaya lazima."
5. Kijana wangu ikiwa mwanamke naye ana moyo ina maana pia kuna wakati anaumia, hivyo epuka kumpa maneno machungu na makali, usimtukane, usimfanye aone kwanini alizaliwa mwanamke au kwanini alikubali kuwa na wewe.
"Usimfanyie mwenzako kitu ambacho hupendi kufanyiwa. Kama hupendi kuambiwa vibaya basi na wewe usiwambie wenzako vibaya."
Najua inaweza ikawa ngumu kunielewa kwasababu kila mtu ana mitazamo na misimamo yake, ikiwa unataka kufika mbali na mwenzako na kuwa watu wenye furaha, ishi kwenye nasaha hizo nilizokupa mzee baba.
Nakupenda [emoji3590].
Uwe na usiku mwema.
[emoji2398] December, 2022
------------------------------------------------------------------------