Nasa wanaendelea na ujenzi wa gateway ya mwezini

Nasa wanaendelea na ujenzi wa gateway ya mwezini

Mzawa_G

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
669
Reaction score
1,479
Tunahitaji kituo kidogo mwezini ambacho kitakachotusaidia au kuwasaidia wanaanga katika mission mbalimbali za mwezini ambapo pia kituo hicho kitakuwa kikipokea wageni mbalimbali wenye lengo la kufanya chunguzi za kisayansi kutokea mwezini.

Gateway itasaidia katika suala kubwa la mawasiliano ambapo kwa muda mrefu mwezini kumekuwa kukikosa kiunganishi baina yake na dunia kitachopelekea muda mwengine tuweze kukosa data mbalimbali za vyombo vilivyopo mwezini huko.

Gateway itatuwezesha haswa kufanya chunguzi za dunia yetu na jua letu kwakuwa tutaweza kuona magimba hayo kutokea mbali na pia itakuwa ni fursa nzuri kuweza kusoma aina mbalimbali za miyonzi inayopokea dunia yetu kutokea katika jua letu.

Kama dunia yetu imekuwa na kituo chake basi hata mwezi wetu unahutaji kituo chake kwakuwa katika siku za usoni itakuwa ni eneo linalotembelewa na wanadamu kwa wingi sana , Gateway itacheka kama checkpoint ya kuelekea katika ardhi ya mwezini.

Katika siku za usoni ujenzi wa kituo hicho utakuwa umemalizika kabisa na harakati za kupeleka kituo hicho zitaanza katika harakati mama za kuandaa safari kubwa ya kihistoria ya mwezini.

[emoji625] Gerald
[emoji625] geraldchristopher1@gmail.com
FB_IMG_1671903730257.jpg
 
Back
Top Bottom