Naruhusiwa kumuoa?

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
782
1,056
Ndugu ZANGU,

Naitwa Udangu, baba yangu anaitwa Mafudu, baba yangu ana mke aitwaye Salima ambaye ni mama yangu mlezi.

Salima ana dada yake aitwaye Fatima, na huyu Fatima ana mtoto aitwaye Faudhia.
Sasa huyu Faudhia naye ana mtoto aitwaye Asia.

Kwa mahusiano hayo hapo,#Asia ni mjukuu wa dada wa mama yangu mlezi.

Hoja yangu ni kwamba,
Je, Kidini (Ya Kiislam)
Kuna uhalali wa mimi kumuoa Asia?
Pia kijamii, hiyo haina/ina tatizo lolote?

Nawasilisha.
 
Uislamu hauoi ndugu zako wa moja kwa moja, ambao ni dada zako, wengine ruksa! Wataobisha wanafuata taratibu za sisi 'MAKHAFIR' bila kujua!
 
Hapo cha msingi umuulize baba yako, au ndugu zako wa karibu mfano wajomba au baba zako wakubwa! Maana hao ndio wanaifahamu historia ya familia zaid.
 
Unaweza ukamuuliza Salima kwa ushauri mzuri akikwambia inawezekana unaweza ukamuapproach Asia na kama akikubali
UNARUHUSIWA KUMUOA
 
Uislamu hauoi ndugu zako wa moja kwa moja, ambao ni dada zako, wengine ruksa! Wataobisha wanafuata taratibu za sisi 'MAKHAFIR' bila kujua!
NIMEKUELEWA ndugu, ngoja tupate na MICHANGO ya wengine.
 
Back
Top Bottom