Narudia tena, ni nani wapanga mipango wa Tanzania?

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,313
6,895
2010 tulikuja na Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza. Kwa kiwango fulani ilifanikiwa. Sema changamoto za Masoko kidogo hatukuwa tumejipanga.

2015 tukaja na sera ya Viwanda, hii ikapuuzia kilimo mpaka nchi ikaingia kwenye njaa.

Maswali ya msingi: Ina maana baada ya kila miaka mitano mapinduzi yanapindua sera za awali?

Leo kilimo hakipewi tena kipaumbele as if ni jambo lililofeli. Kilimo kimeajiri 70% ya watanzania ni ajabu kuona kinapewa bajeti sawa na bomberdia moja..

Sera ya viwanda imefeli maana walisema tuna viwanda vya juice sasa tuingie kwenye viwanda kweli kweli ajabu tumerudi kwenye vyerehani vinne..

Wapanga mipango wa nchi wenye dhamana ya kufikiri mipango ya kuipeleka nchi mbele je hamuoni kuna haja ya kupitia kauli mbiu na focus ya serikali?

Je, mlipanga kuwa na uwanja Chato na daraja la Masaki?
 
Mkuu ukiandika inabidi utulie vizuri!

Swali umeuliza nani anapanga mipango ya Tanzania, Halafu ukaongelea kilimo kwanza kama mbiu, ukamalizia na kusema viwanda ni sera!

Mimi napata wakati mgumu nijadili kipi; maana mipango, sera na kauli mbiu ni vitu vitatu tofauti na utekelezaji wake pia uko tofauti!
 
Nimechanganya makusudi maana kama wananchi hatuelewi kipi ni kipi tena nimekosa mahali pa kupachika Ilani ya CCM, maana Taifa halina dira yaani rais kesho anaweza hamia kwenye miundo mbinu kwanza wote tukakimbilia huko tukasahau viwanda
 
Mkuu kwa uchambuzi wako wa kusema njaa imesababishwa na kutelelekezwa sera ya kilimo ni kujitia aibu. Unaangalia taarifa za idara ya hali ya hewa? Unasoma habari mbalimbali na kuangalia taarifa za habari? Umewahi kulima? Tatizo la upungufu wa chakula limetokana na badiliko la hali ya hewa na tabia nchi. Mvua za vuli hazikunyesha za kutosha na sehemu nyingine hazikunyesha kabisa. Na mvua za masika zilichelewa kwa baadhi ya mikoa. Tafadhari fanya tafiti kabla ya kuanza kuandika uongo.
 
Mkuu ukiandika inabidi utulie vizuri!

Swali umeuliza nani anapanga mipango ya Tanzania, Halafu ukaongelea kilimo kwanza kama mbiu, ukamalizia na kusema viwanda ni sera!

Mimi napata wakati mgumu nijadili kipi; maana mipango, sera na kauli mbiu ni vitu vitatu tofauti na utekelezaji wake pia uko tofauti!
Kwa uelewa wako ili kuendana na kasi ya Magufuli. "Tanzania ya Viwanda" ni nini? Sera, Ilani, Kauli mbiu au mpango kazi
 
Sasa tuulizane kitaalamu sio kishabiki. Sema vitu vyote viliyopuuziwa, kuachwa au kufutwa ktk sekta /sera ya kilimo kwanza vikasababisha njaa? Usiseme vile vya bajeti mpya ya 2017/2018 maana hiyo bado haijaanza kutekelezwa hadi tarehe 1 July kwa hivyo haiwezi kuathiri msimu uliopita wa kilimo. Wewe tuwekee hapa hizo takwimu kwa idadi yaani nambari sio maneno tupu tujue tumeumizwa wapi na serikali yetu tuanze kuhoji.
 
Unatakiwa uwe wazi kwanza kwamba unataka tujadili nini kati ya hivyo!

Pia sera, ilani, kauli mbiu na mpango kazi haziwezi kuwa defined kwa mujibu wa uelewa wangu!
 
Mkuu kwa uchambuzi wako wa kusema njaa imesababishwa na kutelelekezwa sera ya kilimo ni kujitia aibu. Unaangalia taarifa za idara ya hali ya hewa? Unasoma habari mbalimbali na kuangalia taarifa za habari? Umewahi kulima? Tatizo la upungufu wa chakula limetokana na badiliko la hali ya hewa na tabia nchi. Mvua za vuli hazikunyesha za kutosha na sehemu nyingine hazikunyesha kabisa. Na mvua za masika zilichelewa kwa baadhi ya mikoa. Tafadhari fanya tafiti kabla ya kuanza kuandika uongo.
Tungelima vizuri maghala yangekuwa yamejaa au unataka paki tokea msimu mmoja wa mavuno kushuka basi turudi kwenye njaa? Ndio maana nilisems changsmoto ni soko serikali kama mnunuzi mkuu iliiishiwa fedha maghala yakajaa mpaka mahindi yakalala nje na kuharibika.
 
Hapa utuletee 2010 - 2015 ilikuwa hivi na 2016 - 2017(sasa) ipo hivi tulinganishe kilicho achwa au kuongezwa. Nenda moja kwa moja kwenye pembejeo, ruzuku na vinginevyo vinavyohusu moja kwa moja uzalishaji shambani. Ukiweza malizia na sera ya masoko ya bidhaa za kutoka shambani namaanisha soko la mazao ya shamba.
 
Mkuu kwa uchambuzi wako wa kusema njaa imesababishwa na kutelelekezwa sera ya kilimo ni kujitia aibu. Unaangalia taarifa za idara ya hali ya hewa? Unasoma habari mbalimbali na kuangalia taarifa za habari? Umewahi kulima? Tatizo la upungufu wa chakula limetokana na badiliko la hali ya hewa na tabia nchi. Mvua za vuli hazikunyesha za kutosha na sehemu nyingine hazikunyesha kabisa. Na mvua za masika zilichelewa kwa baadhi ya mikoa. Tafadhari fanya tafiti kabla ya kuanza kuandika uongo.
Kwahiyo unataka mvua ya msimu mmoja ikikosekana tufe njaa uongo ni upi wakati mvua ilinyesha 2016 umesahau ng'ombe walilishwa nyanya?
 
Tungelima vizuri maghala yangekuwa yamejaa au unataka paki tokea msimu mmoja wa mavuno kushuka basi turudi kwenye njaa? Ndio maana nilisems changsmoto ni soko serikali kama mnunuzi mkuu iliiishiwa fedha maghala yakajaa mpaka mahindi yakalala nje na kuharibika.
Sasa hapa unajichanganya! Kwa hivyo hatukulima vizuri au hatukuwa na sera ya masoko vizuri kwa maana ya serikali haikununua hayo mazao?
Kipi ndio kipi ainisha vizuri?
 
Sasa tuulizane kitaalamu sio kishabiki. Sema vitu vyote viliyopuuziwa, kuachwa au kufutwa ktk sekta /sera ya kilimo kwanza vikasababisha njaa? Usiseme vile vya bajeti mpya ya 2017/2018 maana hiyo bado haijaanza kutekelezwa hadi tarehe 1 July kwa hivyo haiwezi kuathiri msimu uliopita wa kilimo. Wewe tuwekee hapa hizo takwimu kwa idadi yaani nambari sio maneno tupu tujue tumeumizwa wapi na serikali yetu tuanze kuhoji.
Nimesema tunaendelea kupuuza ndo maana nikaweka mfano wa bajeti iliyopangwa. Ni kitu gani kinaleta njaa kama sio kupuuza kilimo? Na mvua za mwaka huu utashangaa bado mvua za vuli zikikosekana mwakani tutarudi kwenye njaa tena kali
 
Tungelima vizuri maghala yangekuwa yamejaa au unataka paki tokea msimu mmoja wa mavuno kushuka basi turudi kwenye njaa? Ndio maana nilisems changsmoto ni soko serikali kama mnunuzi mkuu iliiishiwa fedha maghala yakajaa mpaka mahindi yakalala nje na kuharibika.
Kama hatukulima vizuri serikali ingenunua toka wapi? Wakati huo huo unasema serikali iliishiwa fedha haikununua chakula hivyo maghala yalijaa chakula hadi kikaoza, hiki kilitoka wapi wakati hatukulima vizuri?
Na kama tulilima vizuri ila serikali haikununua chakula kikajaa ktk maghala hadi kingine kikaharibika kwa kulala nje. Swali linakuja hicho kilichojaa ghala kimeenda wapi? Kama kilibaki kwa wakulima kwanini wao sasa wasikiuze bei nzuri kuliko ile ambayo wangeiuzia serikali? Au kwanini sasa wasikitumie hao wananchi hicho chakula ambacho kimebaki kwao baada ya serikali kushindwa kukinunua?
 
Wapanga mipango, Philipo Mipango, Mwakyembe, Bashite, Gumbo, Happy, Mnyeti, J. Mhagama, A. Kairuki, Ndalichako na Kabudi.
 
Kama hatukulima vizuri serikali ingenunua toka wapi? Wakati huo huo unasema serikali iliishiwa fedha haikununua chakula hivyo maghala yalijaa chakula hadi kikaoza, hiki kilitoka wapi wakati hatukulima vizuri?
Na kama tulilima vizuri ila serikali haikununua chakula kikajaa ktk maghala hadi kingine kikaharibika kwa kulala nje. Swali linakuja hicho kilichojaa ghala kimeenda wapi? Kama kilibaki kwa wakulima kwanini wao sasa wasikiuze bei nzuri kuliko ile ambayo wangeiuzia serikali? Au kwanini sasa wasikitumie hao wananchi hicho chakula ambacho kimebaki kwao baada ya serikali kushindwa kukinunua?
Rejea ziara ya bunge kwenye maghala walisema chakula kipo na kinaliwa na wadudu lakini serikali ndio imegoma kukitoa, Japo hakipo kingi kutokana na maghala yetu ni madogo na hayawezi kubeba chakula kinachotutosha hata kwa miezi mi3
 
Sasa hapa unajichanganya! Kwa hivyo hatukulima vizuri au hatukuwa na sera ya masoko vizuri kwa maana ya serikali haikununua hayo mazao?
Kipi ndio kipi ainisha vizuri?
Tulilima vizuri mpaka tukawa na excess sasa badala ya kushughulikia namna ya kutreat kilichozidi unafikiria namna ya kupunguza production ili kitodhe kwenye maghala yako ambacho bado hakitoshi. Dont you see a problem there...really
 
Back
Top Bottom