Pole sana, Mrejee Mungu kwa maombi ya hitaji lako na amani ya moyo, Sali sana na fanya kazi au tafuta fursa kwa bidii
na usione haya kuomba msaada unapokwama hata kama unaona aibu, ni bora uombe uonekane zoba au mvivu mbele ya macho ya wanadamu lakini alie juu anajua yaliyo ndani yako kwa namna unavyojibidiisha katika kutafuta,
kuliko kufanya maovu kwa minajili ya kujikwamua na hali ngumu ya kiuchumi ilhali unaumiza wengine.
Mwisho wa siku Mungu humjaalia riziki mja wake kwa wakati wake ambao ni sahihi daima. Kumbuka riziki ni mvua inawanyeshea wote, na wakati wako utakapofika usisahau kurejesha shukrani kwa aliyekupatia ambae ni Mungu.