Napingana na Aloyce Nyanda kwenye hoja ya "Wembe uleule" ya Mdude Nyagali

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Kwanza, Alloyce Nyanda kwa nafasi yake katika jamii apaswi kuwa mtu wakuhubir au hata kujaribu kuutukuza ukabila. Yeye Sasa ameshakuwa zao la jamii.

Pili, kauli ya Mdude nyangali kwamba Atatumia Wembe uleule aliotumia kumnyoa mtanguliz wa Rais aliyepo kumnyoa aliyepo ni kauli thabiti na ambayo Mdude anaiishi kwa matendo. Alimkosoa mtangulizi wa Rais aliyepo na bado anaendelea kumkosoa Rais aliyepo kitu ambacho ni Cha kikatiba na kisheria. Wembe ni ule ule Ni kauli ya wote, inapotumika na viongozi dhidi yetu isionekeane Kama ni sahihi lakini wananchi wakiitumia wakahukumiwa. Tukubali kwamba sheria haijakataza kiongozi kunyolewa kwa wembe ule ule hasa katika medani za kisiasa.

Tatu, Nyanda anauvaa uzazi kwenye jukwaa la siasa kitu ambacho hakipo. Kwenye jukwaa la siasa kwenye taaluma hakuna mkubwa na mdogo wote mnashawishi kwa lugha na hoja. Kuendelea kutoa maneno kwa kujifanya wewe ni mkubwa au mdogo ukaacha kusimamia hoja nikukosa hoja. Lazima tukubali kuadhibiwa kwa kadri tunavyocheza na jukwaa. Rejeeni kauli za mama kwenye kampeni alizungumziaje hoja ya risasi, wapi tumewahi kumkosoa? Usawa uzaliwa kwa nidhamu kutoka juu kwenda chini na kutoka chini kwenda juu.

Nne, Nyanda kabla yakuandika maoni yake alipaswa kumhoji mtoa hoja. Yeye anapaswa kuwa neutral person, muda wa kusimama Instagram kwa maoni binafsi nakutoa hukumu umeisha pale alipojipambanua kama mwana habari. Alitaka kuwa na upande aondoke kwenye uandishi na akitaka atoe maoni yake basi akubali kuhojiwa ili atakapokuwa anajibu hoja kwenye mahojiano aweze kujibu anayopenda na asiyopenda kusikia.

Mdude Nyangali chapa kazi ila usilewe sifa.
 
Ukimuandika hapa JF unampa mileage ambayo hastahili ni mwandishi fake, kichwani hajaiva, hajapata mentorship ya kutosha, mkaidi anaona ameiva wakati bado, thinking yake iko low sana muache huko huko usimlete huku.
 
Mbona hamkuwahi kujadili kauli za Magufuli, aliwahi kusema wasiropokee bungeni na wakiropoka mtaani ata deal nao. Tuliyaona matokeo
 
Mdude katoa kauli ya kawaida tu kwenye nchi ya kidemokrasia mnaona ajabu, Je kwenye nchi zawenzetu huko wabunge wanapozichapa waziwazi, maraisi kurushiwa viatu, kutemewa mate?

Na mimi naiunga mkobno kauli ya mdude kuwa kama Samia kifuata njia za kidikteta basi wembe uleule tuliomyoa nao Magufuli naye tutamnyoa pia
 
Back
Top Bottom