Napinga ujengaji flyover Dar

Napinga ujengaji flyover Dar

Kijakazi

Platinum Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
9,265
Reaction score
14,912
Napinga ujengwaji wa barabara za juu au flyover Dar, badala yake hizo fedha zipelekwe kwanza Mikoani, Wilayani ambako hamna Barabara, kwa mfano kwenye kuunganisha Mikoa kwa Mikoa kama vile Tabora-Mbeya, Mtwara- Ruvuma, Kondoa-Handeni, Ifakara- Handeni-Lushoto, Arusha- Musoma n.k.
kwa kufanya hivyo kutawezesha pia Watu waishio mikoa mingine kujikomboa kiuchumi, Dar tayari tuko mbali sana kiuchumi ukilinganisha ni mikoa mingine, hivyo haileti maana kuendelea kuwekeza fedha zote hapa Dar!

Halafu isitoshe kabla hata ya kufikiri kujenga hizo flyover kwanza barabara za mitaani zote zijengwe na kupitika kama walivyofanya Barabara za oysterbay,Masaki, ambazo zimewaondelea foleni wakazi wa huko ingawaje uwiano wa watu wenye magali kwa wakazi wa huko ni mkubwa kuliko sehemu yoyote ile ya nchi yetu hivyo basi wajenge kwanza br pia sehemu kama za Sinza, Magomeni, Temeke, Vingunguti, n.k yaani flyover ziwe hatua ya mwisho kabisa.
 
Kwa rejesha mawazo yako kwenye theory ya .....Center - Peripheral relations, halafu jiulize jinsi uchumu wa nchi unavyorudi nyuma kwa watu kukaa kwenye foleni muda mrefu - muda wa kazi na mapumziko kupotelea njiani kwa kuchelewa kufika kazini na kurudi nyumbani, mafuta, vipuri n.
 
Flyover ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi ili kupunguza traffic jam. Unajua ni sh ngap zinapotea kwa siku kwa sababu ya foleni Dar? Pesa itakayookolewa itasaidia kurekebisha huko kwengine.
 
Flyover ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi ili kupunguza traffic jam. Unajua ni sh ngap zinapotea kwa siku kwa sababu ya foleni Dar? Pesa itakayookolewa itasaidia kurekebisha huko kwengine.

Unajua ni fedha kiasi gani kinapotea kusafirisha Mzigo wa Biashara kutoka Mbeya kwenda Tabora kwa wiki mbili?
 
Utafiti umefanyika ya kutosha na ukakidhi haja ya kuwa na hizo barabara za juu. Huko kwingine kutapiga hatua kama Dar itasonga mbele vilevile.
 
Napinga ujengwaji wa barabara za juu au flyover Dar, badala yake hizo fedha zipelekwe kwanza Mikoani, Wilayani ambako hamna Barabara, kwa mfano kwenye kuunganisha Mikoa kwa Mikoa kama vile Tabora-Mbeya, Mtwara- Ruvuma, Kondoa-Handeni, Ifakara- Handeni-Lushoto, Arusha- Musoma n.k kwa kufanya hivyo kutawezesha pia Watu waishio mikoa mingine kujikomboa kiuchumi, Dar tayari tuko mbali sana kiuchumi ukilinganisha ni mikoa mingine, hivyo haileti maana kuendelea kuwekeza fedha zote hapa Dar!

Halafu isitoshe kabla hata ya kufikiri kujenga hizo flyover kwanza barabara za mitaani zote zijengwe na kupitika kama walivyofanya Barabara za oysterbay,Masaki, ambazo zimewaondelea foleni wakazi wa huko ingawaje uwiano wa watu wenye magali kwa wakazi wa huko ni mkubwa kuliko sehemu yoyote ile ya nchi yetu hivyo basi wajenge kwanza br pia sehemu kama za Sinza, Magomeni, Temeke, Vingunguti, n.k yaani flyover ziwe hatua ya mwisho kabisa!

Hakuna flyover inayojengwa Dar,kinachotarajiwa kujengwa kinaitwa Upper passage.
 
Kwa rejesha mawazo yako kwenye theory ya .....Center - Peripheral relations, halafu jiulize jinsi uchumu wa nchi unavyorudi nyuma kwa watu kukaa kwenye foleni muda mrefu - muda wa kazi na mapumziko kupotelea njiani kwa kuchelewa kufika kazini na kurudi nyumbani, mafuta, vipuri n.

Unajua Uchumi unasimama kwa kiasi gani kwa watu Mikoa kwa mikoa kutokuwa na mawasiliano? Unajua Mkulima wa Ifakara anaathirika kwa kiasi gani au angefaidika vipi kama angeweza kusafirisha mazao yake mpaka Tanga au Arusha bila shida? Unaelewa hilo lingechangia ukuaji wa Uchumi kwa kiasi gani?
 
Utafiti umefanyika ya kutosha na ukakidhi haja ya kuwa na hizo barabara za juu. Huko kwingine kutapiga hatua kama Dar itasonga mbele vilevile.

Waliofanya huo Utafiti kama ni Kweli basi ni Vilaza, hakuna nchi iliyoendelea kwa kubeza Mikoani, hata Wazungu walivyokuja kitu cha kwanza walichofanya walijenga Reli inyounganisha Mikoa ya Arusha KLM na Tanga, Dar na Mikoani yaani ktk Kigoma, Mwanza, Tabora mpka Dar sasa ni kwa nini?
Kwa nini hawakujenga tu Dar? Kama unafikiri Dar muhimu kuwa na miundombinu Bora kuliko kwingine? Hizi Barabara zote tunazojenga leo tunarekebisha tu lkn zilijengwa na Wazungu sasa ni kwa nini wao hawakupendelea Dar Tu?
 
Hakuna flyover inayojengwa Dar,kinachotarajiwa kujengwa kinaitwa Upper passage.

Vyovyote vile utakavyoamua kuiita lkn Ukweli ni uleule kwamba itatumia fedha nyingi ambazo zilipaswa zipelekwe sehemu nyingine za Nchi, isitoshe itasaidia nini kuwa na flyover Ubungo wakati br zote zinazochepuka ni mbovu na za mabonde na hazipitiki, sawa utatoka huko kwenye li-fyover lako mbio ukifika kona ya kuingia ndani unakuta foleni kwa Magari yamekwama kwenye mashimo sasa utakuwa umefanya nini?

Wazo lako ni zuri pia ni sahihi!
Dar Es Salaam Haihitaji barabara za juu katika kipndi hiki. Dar inahitaji barabara za mitaa (street roads), Barabara lishi (Feeder Roads) na nyongeza ya barabara tawanyishi (Arterial Roads). kwa mfano hivi Sasa Dar in arterial roads nane tu! wakti zilitakiwa angalau ziwe ishirini kwa uwiano wa safari za magari jijini.
Napinga ujengwaji wa barabara za juu au flyover Dar, badala yake hizo fedha zipelekwe kwanza Mikoani, Wilayani ambako hamna Barabara, kwa mfano kwenye kuunganisha Mikoa kwa Mikoa kama vile Tabora-Mbeya, Mtwara- Ruvuma, Kondoa-Handeni, Ifakara- Handeni-Lushoto, Arusha- Musoma n.k kwa kufanya hivyo kutawezesha pia Watu waishio mikoa mingine kujikomboa kiuchumi, Dar tayari tuko mbali sana kiuchumi ukilinganisha ni mikoa mingine, hivyo haileti maana kuendelea kuwekeza fedha zote hapa Dar!

Halafu isitoshe kabla hata ya kufikiri kujenga hizo flyover kwanza barabara za mitaani zote zijengwe na kupitika kama walivyofanya Barabara za oysterbay,Masaki, ambazo zimewaondelea foleni wakazi wa huko ingawaje uwiano wa watu wenye magali kwa wakazi wa huko ni mkubwa kuliko sehemu yoyote ile ya nchi yetu hivyo basi wajenge kwanza br pia sehemu kama za Sinza, Magomeni, Temeke, Vingunguti, n.k yaani flyover ziwe hatua ya mwisho kabisa!
 
Ungetupa angalau projection ya barabara kilometa ngapi zinaweza kujengwa kwa gharama za fly over moja ya tazara.
 
Kila mji ujitahidi kujijenga kwa pato la ndani kwanza.
 
hata mimi kama gogo la shamba nakubaliana na wazo lako, ziimarishe kwanza barabara za kawaida au za mitaani katika kila mkoa,kwa mfano barabara zote za Ujiji kigoma ziwekwe lami kadhalika kila mkoa kuliko kuangalaia Dar peke yake.
 
Bavicha kwao upinzani ni kupinga kila kitu.
 
Unajua Uchumi unasimama kwa kiasi gani kwa watu Mikoa kwa mikoa kutokuwa na mawasiliano? Unajua Mkulima wa Ifakara anaathirika kwa kiasi gani au angefaidika vipi kama angeweza kusafirisha mazao yake mpaka Tanga au Arusha bila shida? Unaelewa hilo lingechangia ukuaji wa Uchumi kwa kiasi gani?

Songea - Dar ni lami mbona mahindi yanaozea kwenye magala. Aidha, ni gharama gani itakayomika kujenga hayo madaraja inaweza kujenga hizo bara bara za mikoani. Sina uhakika kama kinachojengwa Tazara ni flyover, miye naona ni kama daraja vile. Maana flyover ni barabara zinazoonekana nchi zilizondelea, kwa mfano barabara inapita juu kwa juu kutoka Chalinze mpaka Mbagala.
 
Wazo lako ni zuri lakini hiyo avatar yako ni utata mtupu
Yaani hiyo avatar ilinifanya nirudi tena kuangalia, nilichokiona nisahihi au macho yamwnidanganya. Na je kuna ujumbe gani anatuma kupitia avatwr hiyo.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Hakuna flyover inayojengwa Dar,kinachotarajiwa kujengwa kinaitwa Upper passage.

Mkuu, tofauti yake ni nini? Mi nilidhani ni kitu hicho hicho tu. Moja ni American English na Nyingine British English.
 
Back
Top Bottom