Mkuu VIKWAZO
Madhara/effect lengwa ya maamuzi ya mahakama yeyote ni kujaribu kumrudisha yule anayeamuliwa kuwa na haki juu ya dai husika, kwenye mahali ambapo atakuwa kama vile hakuwahi kudhurika na mlolongo mzima wa kesi aliyoianzisha ama iliyoanzishwa dhidi yake..
Njia nzuri ya kuhakikisha hili ni kuangalia katika wakati wote wa kusikilizwa hukumu na hata baada ya hukumu, ni haki zipi ambazo mshindi wa kesi alizikosa kwa kuwapo kwa kesi hiyo iliyoisha na ambazo angezipata endapo hiyo kesi isingekuwepo kabisa.
Njia ya kuielewa hii zaidi ni kuchukulia mfano kuwa Bwana Lema alikuwa ameajiriwa kabla ya kuwa mbunge na aliamua kuiacha kazi yake mara tu baada ya kupata ubunge wake. Kazi ya Ubunge ikitegemewa pia kuwa chanzo cha mapato ya yeye na familia yake kujitimizia mahitaji ya kila siku..mahakama haiwezi kujipatia uthibitisho wa moja kwa moja kuwa Lema alikuwa na uwezo wa kuendelea kutimiza mahitaji yake ya kila siku (kama ilivyokuwa kabla ya kupata Ubunge) na pia kutokana na hukumu ya mahakama, haikuwa kosa lake kusimamishwa kuendelea na utekelezaji wa ajira yake mapya...hivyo basi, hapaswi kuadhibiwa kwa kosa ambalo hakulifanya na anastahili kulipwa stahiki zake zote kana kwamba hakuwahi kuwa mbali na ajira yake hata siku moja kutokana na kesi husika.
Kuna watu wanaleta utetezi kisiasa kwa kuzani kila mtu mwanasiasa, sasa hapa watakwamba hata hoja ya kukataa posho za wabunge itakwama, mantiki kuwe na malipo ya haki kama vile mishahara na sio posho wakati ujafanya kazi.
Posho kama ya mafuta wakati hakufanyakazi kwa miezi 8, sio sahihi
Lazima Pro-Chadema watakuambia umetumwa kumchafua Lema, Chadema huwa hawana makosa ni chama cha mitume.
Nakubaliana na wewe 50%
sina tatizo na Lema kulipwa mshahara wake, hiyo ni haki yake ya msingi kabisa, Tatizo langu ni lema kulipwa posho (jimbo, mafuta etc etc) hizo sio haki zake na msingi, ni pesa inayotakiwa kwendana na shughuli ambayo kwa kipindi hiyo ilisimama, ni hakika kwamba Lema alizuiwa na mahakama kundelea kama mbunge wa Arusha na kwa misingi hiyo haya ghalama za mafuta na uendeshaji wa jimbo ( posho ya jimbo) ili koma, hiyo sio pesa ya Lema au mbunge yeyote kujikimu kwa mambo yake binafsi, kwa misingi hiyo hana haki ya kupewa posho hizo kwa sababu akufanya hizo kazi, hizo ni posho unapata ili ufanye kitu furani na sio pesa ya matumizi yako ya kawaida
Kwahiyo makosa ni ya Lema au ni ya kisheria?
Labda la msingi pia zaidi ni sisi kupata mchanganuo wa matumizi ya kila posho anayostahili kulipwa mbunge,..kwa maana ya shllingi ngapi hutakiwa kutolewa kwa ajili ya matumizi ya aina gani, yanayotarajiwa kufanyika wapi na kwa utaratibu upi (i.e kwa mkupuo, kwa kila mwezi, kwa kuthibitishwa na vithibitisho kama risiti na viambatisho vingine vinavyoonesha ushahidi wa matumizi etc..)
Mathalani mfuko wa mbunge wa kusaidia jimbo, unatakiwa kutumikaje??kila mwezi?kila wiki??ama mbunge anaruhusiwa kulimbikiza hizo pesa na hatimaye kuzifanyia matumizi kwa mkupuo wakati fulani hapo mbeleni busara yake itakapoona inafaa??
Je utaratibu ukoje kwa wabunge ambao inadhihirika wazi kuwa walipewa fedha kwa ajili ya matumizi makuu na kama posho wakati (unaotakiwa kuwa) wa utekelezaji wa shughuli zao za kibunge majimboni lakini hawakuzitumia kabisa kwa shughuli hizo??je sheria imeweka kwa nani maamuzi ya kutumia hizo pesa ama la kwa ajili ya shughuli za mbunge jimboni?..je mbunge anaweza kuadhibiwa kwa kutoonesha ushahidi wa kutumia hizi fedha kwa ajili ya shughuli za kibunge?na adhabu yake ni ipi??
Nadhani tukijibu haya maswali kwa ufasaha tutaweza kumhukumu Lema kwa haki zaidi.
yanzo vya kuaminika kutoka ndani ya Bunge na wakiwamo wabunge wa upinzani na wale wa CCM vilisema kwamba malipo ya mbunge kwa mwezi ni Sh10.7 milioni, yakijumuisha Sh2.3 milioni za mshahara, Sh2.5 milioni za mafuta, posho ya jimbo inayokaribia Sh5 milioni na malipo mengineyo.
Kwa muda wa miezi zaidi ya minane ambao amekuwa nje ya Bunge, malimbikizo ya mshahara wake yanafikia Sh18.4 milioni, posho ya jimbo Sh40 milioni, mafuta Sh20 milioni na posho nyingine Sh6.6 milioni.
apewe malimbikizo ya mshahara wake yanafikia Sh18.4 milioni,Ninachopinga mimi ni hii hapa Sh40 milioni, mafuta Sh20 milioni na posho nyingine Sh6.6 milioni.
Mleta uzi ameleta observation nzuri sana ambayo inaonyesha kuna haja ya kuzipitia upya hizi kanuni mfano mzuri hiyo issue ya mafuta maana huwezi kuzirudisha siku nyuma maana mafuta atakayopata kuanzia mwezi huu na kuendelea yatafanya kazi ya kuanzia hapa aliporudishiwa ubunge wake na kuendelea.
Kifupi sioni tatizo la Lema kupewa hizo pesa kwa kuwa hata hao waliopewa hakuna kipengele kinachoonyesha wameyatumia vipi (yaani wanaonyesha Log book alafu kama hawajazimaliza wanarudisha chenji), kanuni zinawapa posho ya mafuta kama zawadi na hakuna ufuatiliaji wa yametumikaje, kama kungekuwa na kanuni ya kufanya retirement hapo kiukweli Lema hastahili lakini kwa kuwa huwa wanapewa tu hizo posho kama karanga iwe unayatumia au unagawa basi acha apewe.
MLETA UZI AMETOA ANGALIZO TU NA UZOEFU WAKE NA NDIO MAANA WAFADHIRI WENGI HUWA WANATUSHANGAA SANA
marejesho, EL anapata kama kawa mafao yake ya ustaafu wa u-Pm kwani hata ukichaguliwa leo na kesho ukastaafu unalipwa
Sh2.3 milioni za mshahara, Sh2.5 milioni za mafuta, posho ya jimbo inayokaribia Sh5 milioni
Alipiga kazi vyema hadi superviser akampa likizo, sasa kuna shida gani alikuwa far ahead of time.Kwa hiyo Lema kapata Excuse kuchukuwa hizo pesa ambazo ajazifanyia kazi.
unfortunately sheria zetu ndivyo zilivyo.... Kwa sasa hakuna tunachoweza kubadilisha ila tuhakikishe tunapa katiba mpya SAFI imbayo tutabainisha mambo yote yenye utata kwa sasa.....
Swali la kizushi... Mheshimiwa wa Monduli bado anapokea posho ya "Waziri Mkuu MSTAAFU?
Ndio hapo kwenye argument mkuu VIKWAZO..je hiyo 5m inatakiwa kutumika na kila mbunge kila mwezi jimboni kwake??je kuna uwezekano wa mbunge kuilimbikiza kwa miezi 12 ikafikia milioni 60 na kuenda basi kufanya hayo maendeleo jimboni??..
Je hii 2.5 million ya mafuta...haya ni mafuta ya kwenda wapi hasa??je ni safari za mbunge kutoka nyumbani kwenda bungeni tu kila siku??je ni mafuta yanayotumika pia kwenye safari za kibunge jimboni??.,..je anaweza kuyalimbikiza na kuyatumia wakati autakao hapo baadaye?vipi asipoyatumia kabisa?tumfanyeje?...hakika ninayo idadi kubwa sana ya wabunge ambao huwa wanafika majimboni baada ya miaka mitano..
na pia katika kazi zetu za kawaida zisizo za kibunge,..wakati mfanyakazi akiwa na mkataba wenye kipengele kinachoruhusu kulipwa masurufu ya mafuta,,mwezi atakaokuwa likizo huwa anastahili kuendelea kulipwa hayo masurufu?..
baada ya kujadili haya nadhani ni vema mjadala wetu ukawa mpana zaidi..unaohusu stahiki wastani za wabunge..je tuweke utaratibu gani wa malipo ili kama taifa tusiingie tu hasara hasa pale wabunge wanapoonekana dhahiri kutotekeleza majukumu yao stahiki??...mfano wa wale waliopata ubunge na kwenda kuishi marekani.....