Napinga kwa nguvu zote CHADEMA kutokata rufaa

hukumu iliyomtia hatiani mh lema ni katika makosa 6 kati ya 8 sasa msije mkakomalia jaji amejisahau kumbe katika makosa hayo sita yaliyomtia kitanzini yanaingia kwenye kila kifungu cha kumsimamisha kutogombea au kumruhusu kugombea na decision kama hizi maranyingi inatoa mwanya atakayeweka pingamizi lema asigombee na akashinda lema anabanwa mbavu na sheria zaidi ya moja yani sheria ya nchi criminal law ,sheria ya uchaguzi na bila kusahau regulations zake hakuna option itakayomuweka salama mh lema zaidi ya kukata rufaaa ambayo ndiyo mtego uliposetiwa aingie huko ambapo wana CCM lazima wale pilau CDM waki kata rufaa UWEZEKANO WA LEMA KUGOMBEA TENA UBUNGE NI SAWA ILI UIONE AHERA LAZIMA UFE NDIYO UENDE AHERA.sasas lema hana ujanja hizi ni mbinu za kimafya instead of assasination
 
Mie sio mwanasheria wala sizitambui sheria vizuri ila kwa hili la Lema huhitaji Elimu ya juu kujua nini kinachoendelea,Vuta subira tu hutaamini macho yako kitakachotokea,Kifupi jimbo limepotea
 
CCM itapenda uchaguzi urudiwe japokuwa inajua haiwezi kushinda,Lema hatoweza kugombea mpaka 2017! CCM haikutaka mtu kama lema,bora apatikane mbunge mwingine yeyote ambae wanaamin hatokuwa na mvuto kama wa Lema especially katika kipindi hiki cha katiba mpya,chadema itashinda ubunge lakin kwa kumkosa Lema CCM itakuw pia nayo ni mshindi.Tafakari chukua hatua!
 
Hii kitu judge hajajichanganya. Lawyer huwa tunatwist the law but not break the law. Hapo jugde sio kuwa hakuona hicho kifungu,but he errod with reasons.
 
Judicial review mbaya.In myanya ya rushwa. Hapa ni kukata rufaa(Appeal) basi.Tufanye kitu cha uhakika!
 
KWA kwa mujibu wa HUKUMU LEMA haruhusiwi kugombea. Embu soma vizuri kipengele cha kwanza cha post yangu nilicho kiandika MOJA
Sasa naomba nisaidie, umesema huu ni mpango uliopangwa na EL na wafuasi wake, sasa unapata wapi ujasiri kuwa CDM ikiapeal haki itapatikana? Binafsi naona hata mahakama imeshatekwa nyara hasa ukizingatia hukumu ya kesi ya mgombea binafsi na hii ya Ubunge wa Arusha mjini, kwahiyo mie naona haki haiwezi tena kupatikana mahakamani bali ni kuelekea kwenye uchaguzi. Lema apewe majukumu muhimu ktk chama maana ameonesha kuwa ni mpiganaji aliwachanganya hata wale wanaojiona ndio wamiliki wa nchi hii. Anaweza kutumika kama anavyotumika Dr Slaa sasa, iundwe program ya kuelimisha jamii kama vile operation sangara halafu iwe chini ya Lema hapo mtashuhudia enzi mpya ya Godbless Lema mwenye mafanikio ya juu kabisa.
 
Na waambieni kwa mambo yanavyokwenda, wanaweza kujitokeza mamluki fulani hivi wakamkatia rufaa G.Lema, kama mtego ulikuwa Lema akate rufaa ili mahakama icheleweshe kusikiliza rufaa hiyo....kuweni macho. Si bado mna kumbukumbu ya waliofungua kesi iliyosababisha G. Lema avuliwe ubunge ?
 
Kama Chadema wanaamini kwamba mahakama zetu hazitendi haki na hazipo huru kwanini wao hupeleka kesi au mashitaka huko?
 
Kama Chadema wanaamini kwamba mahakama zetu hazitendi haki na hazipo huru kwanini wao hupeleka kesi au mashitaka huko?

Uhuru wa mahakama hauzuii mahakama kutotenda haki na ndio maana kuna utaratibu wa kukata RUFAA katika mfumo huo huo ambao ni 'huru'! Kumbuka 1 + 1 = yaweza kuwa mbili, tatu, hata kumi au 11 katika sheria na siasa!!!!!!
 
Kwa kweli umeandika vyema na hoja zako ziko wazi. CDM mnahitaji utulivu kwani pia adui zenu kupitia hukumu hii watataka kuanza kupenyeza makundi. Endapo mtaacha kukata rufaa na kumtelekeza Lema hao hao wataanza kuwachochoa watu kuwa CDM imemtelekeza Lema ili pawepo mgawanyiko. Hivyo rufaa ni ya muhimu kuliko kukimbilia uchaguzi. RUFAA ITAKILINDA CHAMA chenu. Take my word mitego iko mingi kwenye kila hatua mtakayochukua. Lakini wanataka kuivuruga CDM kupitia hili.
Wanasheria watumike kwani CDM kupitia ushindi wa Lema ina kura 56,000 lazima tufikirie maamuzi yetu juu ya mawazo ya watu 56,000.
Wakilishwa sumu kuwa CDM imemtelekeza mbunge wenu sumu hiyo itakuwa mbaya.
"Wao wana Jaji mahakama kuu, sisi tuna Mungu"
 
Huhitaji kuwa prof wa sheria kung'amua kuwa hukumu ya LEMA ni mtego. Hata Jaji alimwambia akate rufaa. Hata Jaji wa Majaji aka JK kupitia tamko lake walimwambia LEMA akate rufaa. Swali kwanini wote hawa au 'maadui' wako wawe wa kwanza kukushauri namna au njia ya kupata ushindi? Adui mara zote anakuombea njaa

Katika hili CCM wanachotaka ni Lema akate rufaa na kesi iende mwendo wa kinyonga jimbo likose mwakilishe then mwishowe muda uishe na uchaguzi ushindikane kufanyika

Hapa jibu ni moja tu nalo ni HAPANA KUKATA RUFAA. Na kama tunaogopa pingamizi wala hakuna shida kwani CDM watamsimamisha mwingine na Lema kupewa majukumu mengine ya kitaifa/kichama ambapo itakuwa faida zaidi kwa CDM na mwiba mkali zaidi kwa CCM kuliko hata huo ubunge

HAKUNA KUKATA RUFAA
 
Lema tunafahamu hujuma tunayo fanyiwa n ccm pamoja na serikali yao,lakini hili la kusema hukati rufaa halikubaliki kamwe.
wewe mwenyewe uliwahi kusèma hatumkatai meya kwasababu ya kuwa ni ccm,bali ni kutokana na kukiukwa kwa sheria,je vipi wewe haki ili fwatwa?

Hu ni mtego kwako na kwa chama,maana watajenga propaganda na kusema chama kimekutelekeza kwa kutokukata rufaa.

Tafathali kama kweli wewe ni mpigania haki na mfuata sheria tunakuomba kubali maombi yetu.

Furaha ya ccm si kurudiauchaguzibali ni kuhakikisha wewe lema hugombei,sisi wana arusha tunakuomba siwape mwanya huo.ulituambia kosa kubwa kwa bina damu ni woga vìpi kamanda unataka kutuangusha?

NI LAZIMA TUPIGANE VITAHIVI PAMOJA MPAKA MWISHO HUWEZI KUTUACHA MSTUNI KWA KISINGIZIO CHA UCHAGUZI KUCHELEWESHWA,WAMEMWAGA UGALI SISI TUMWAGE MBOGA,MÀPAMBANO LAZIMA YAENDELEE NA WEWE UKIWA FRONT,HAKUNA KURUDI NYUMA KAMWE,

RUFAA NI LAZIMA NA SI OMBI
 
habari toka ndani ya chadema zinasema kuwa wanakwenda arusha kuwapa fulsa wananchi wa jimbo la arusha mjini waamue wao kipi bora kifuate kati ya kukata rufaa au wakubaliane na hukumu uchaguzi urudiwe
naomba kuwasilisha
 
Ni strategy nzuri ya kuwashirikisha wananchi, wananchi wanajiona kuwa wanathaminiwa.
 
habari toka ndani ya chadema zinasema kuwa wanakwenda arusha kuwapa fulsa wananchi wa jimbo la arusha mjini waamue wao kipi bora kifuate kati ya kukata rufaa au wakubaliane na hukumu uchaguzi urudiwe
naomba kuwasilisha

Busara na hekima ya juu kabisa kwenye jambo hili ni kukataa rufaa, maan hii hukumu imetengenezwa kisiasa, kuilazimisha chadema kutafuta suluhisho kupitia mahakama kuliko kurudia uchaguzi, si haki Lema kuzuiliwa kugombea hata kama hatagombea lakini ni muhimu yeye kuondolewa hicho kitanzi cha kisiasa hivyo mimi naunga mkono kukataa rufaa.
 
Naunga mkono hoja! Rufaa ikatwe.Inaoneka Jaji kafanya makusudi katika majumuisho yake na kutumia kifungu cha 114 ili kuwachanganya wafuatiliaji wasiojua sheria.Hii imejidhihirisha wazi kwa kuwa awali alitumia kifunga 108 kutoa hukumu yake kwa kumalizia akatumia kifungu 114.Natumaini katika mkutano wa leo wa CDM ufafanuzi utatolewa ikiwa ni pamoja na maamuzi na utekelezaji, kwani pia na uhakika wakili wa CDM atatoa ufafanuzi wa kisheria.Tumeanza na Mungu na tutamaliza na Mungu:heh:
 
Back
Top Bottom