Napinga kwa nguvu zote CHADEMA kutokata rufaa

Wellsaid mkuu jinsi hiyo issue ilivyokaa ni kweli jaji alijichanganya wakati wa majumuisho kosa alilopatikana nalo lema ni illegal campaign na siyo illiegal practice.
Mytake:Wakili wa Lema inabidi awasiliane na jaji iliaclarify kuwa huo mkanganyiko wa vifungu alikosea au lah! Lengo la magamba ilikuwa ni lema akate rufaa ambayo ingemuweza kuendelea kuwa mbunge kitu ambacho kingepeleke delidali na hukumu ingetoka mwakani na kama bado mahaka ya rufaa ingemtia lema hatiani jimbo la arusha lingebaki wazi mpaka 2015 coz sheria ya uchaguzi inasema kama jimbo litaachwa wazi miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu hakutakuwa na ujazwaji wa hiyo nafasi.
Wanasheria mtanirekebisha kama nimekosea.

Jamani huyo jaji ajajichanganya bali ndivyo alivyoelekezwa kufanya! huo ni mtego jamani angalieni kwa jicho la tatu! Nguza viking na wanae walikata rufaa mara ngapi??? na ilikuwaje! JK anakisasi kisichokuwa na mwisho na inaonyesha hatakufa ataanguka tu! so kukata rufaa hiyo ni mpaka 2015 na atakuwa katoka ndo rufaa itasikilizwa
 
1:Naunga mkono hoja zako zote,maana ni hoja nzito(Bila kujali usahihi wako)
2:Baada ya kuchanganya akili zangu,zako na za great thnkers wengine,nitarudi hapo ku suggest whether you are right or wrong na kumshauri Kamanda Lema na viongozi wa CHADEMA.
 
Hukumu hii iko kimtego ili tu Lema asigombee na wala CDM wasichukue jimbo likae patupu hadi 2015. Haiingii akilini jaji aliyebobea kutoa hukumu kama hiyo. Hata kama ni kuchanganyikiwa kwa jaji lakini alikua na muda wa kutosha wa kutoa hikumu. Kesi ya wizi wa kuku UHUKUMIWE KUNYONGWA wapi kwa wapi. Istoshe wanajua kbs katika maamu yote mawili ni kwamba ukiitishwa uchaguzi mwingine na wakimsimamisha Lema mbele ya safari wataweka pingamizi na CDM hawataruhusiwa kugombea kutokana na kifungu alichohukumiwa nacho Lema. Nia yao hawataki Lema arudi tena bungeni ni borawamsimamishe mtu mwingine.
 
Mpaka sasa sielewi nani mkweli na nani ananipotosha, wengine ooooooh Lema haruhusiwi kugombea, wengine oooooh Lema anaruhusiwa kugombea, kipi ni kipi hapa?

Kinachopotosha ni hukumu yenyewe. Lema katiwa hatiani kwa kifungu ambacho anaruhusiwa kugombea tena bali kahukumiwa kwa kifungu ambacho haruhusiwi kugombea. Ajabu ya mwaka.
 
kwanza...
Lema asikate rufaa na uchaguzi uitishwe Chadema wasimamishe mtu mwingine... wakati mambo ya uchaguzi yanaendelea , Lema au mtu mwingine kwa niaba yake binafsi, chadema au kwa manufaa ya wanachin wote wa Tanzania afungue kezi mpya ya kikatiba kwa kunyimwa haki yake ya kikatiba kushiriki kwenye uchaguzi either kupiga au kupigiwa kura...maana katiba haijasema kwamba kosa alilofanya lema ni kunyimwa haki ya kuchaguliwa au kupiga na kupigiwa kura... makosa ya jinai ndo pekee yanayoweza kumnyima mtu haki hiyo...na katiba mama haiwezi pingana na vipengere vya uchaguzi, na vikipingana.. katiba mama inakuwa precedent.. pia si lazima lema afungue kesi mpya, chadema pia wanaweza kutumia mtindo wa ki-ccm kwa wanachama wao kupinga maamuzi ya mahakama hiyo iliyotengua maamuzi ya Lema...

Pili.. serikali iseme wazi kama pia inafurahia kulipa gharama za kesi hiyo maana si Lema pekee alishtakiwa... tangu lini serikali ikaona ni jambo la furaha na fahari kubwagwa katika kesi...? au haina uchungu na kodi zetu? wao wanafikiria tu ulaji utakao tolewa na uchaguzi mpya...

Serikali (Tume ya uchaguzi) pia inafaa ifunguliwe kesi mpya kwa kutowajibika wakati wa kampeni hizo za Lema pia akina Lusinde maana polisi hawawezi kuona mtu anatukana au kukashfu na wasimamizi wa sheria (polisi) wanakaa kimya bila kumkamata wakati vifungu hivyo alivyovitumia jaji kumtia Lema hatiani vilikuwa vinajulikana kwao...

Either polisi, tume ya uchaguzi, au serikali iliyokuwepo wakati wa uchaguzi inafaa vifikishwe mahakamani kwa lapse of duties wakati hizo kasha za Lema au Lusinde zikifanyika ....haya mambi yasiishe tu kwa uchaguzi mpya... lazima na wale walioshindwa kufanya kazi zao ipasavyo nao wawajibike...

ni hayo kwa leo
 
NNE: kuna wapiganaji watatu waliuwawa na polisi kwa kushiriki maandamano ya kupinga CCM kubaka Demokrasia na kujipitishia MEYA kibabe, Marehemu hawa waliandamana na kupoteza maisha yao sababu ya kusimamia HAKI na walikufa wakiamini CDM wanasimamia HAKI kwa gharama yoyote. Sasa leo inakuwaje CDM wanashindwakuwaENZI marehemu hao kwa kuendelea kusimamia HAKI kwa gharama yeyote hata kwa kupoteza jimno la LEMA ili HAKI dhidi ya LEMA yaani HAKIA ya kugombea arejeshewe?

Umeeleza mambo mengi ya msingi katika thread yako, lakini nadhani ingekuwa vizuri zaidi kama ungesubiri kwanza mkutano wa kesho, ambao naamini kabsa utaeleza hatua ambazo uongozi wa CDM umepanga kuchukua. Naamini kabsa tangu kutolewa kwa hukumu hiyo ya Lema, uongozi upo busy kwa vikao vya hapa na pale, ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na wadau mbalimbali hatua muafaka za kuchukua (kukata rufaaa au kutokata). Then baada ya mkutano wa kesho wa CDM, nadhani tutakuwa na uwanja mpana zaidi wa kujadili hoja hii.

Hapo kwenye nyekundu sina uhakika kama ni kweli.
 
WANA-ARUSHA KAMA ARUMERU MASHARIKI:
BAADA YA MAFISADI 'KUSHINDA KESI' KWA MTAJI WA HELA ZAO KATIKA MAHAKAMA YA CCM MAJUZI, HIVI SASA SISI 'MAHAKAMA YA RUFAA YA WAPIGA KURA' TUNASUBIRI KWA HAMU KURUDISHA KAMANDA LEMA BUNGENI FASTA FASTA

WaTanzania tumeshaamua, mambo yote ni kwa CHADEMA;

Hivi sasa Mahakama ya CCM imeshatoa hukumu yake ya ki-itikadi kwa Jembe la CHADEMA Mhe Godbless Lema sasa kinachofuata ni CHADEMA mkatuletee hiyo Rufaa sisi WAHESHIMIWA WAPIGA KURA na kumrejesha FASTA Kamanda huyu bungeni kuendelea na kazi zake.

Kwa kuwa walalahoi tumeshaamua kwamba CCM basi hata wangemsimamisha nani Arusha, je ni nani tena wa kutuzuia???

Enyi Machalii wooote jijini Arusha, tuanze mapema kunoa kura zetu kukata nazo FITINA ZOTE ZA MAFISADI dhidi ya Kamanda Lema mpaka waumbuke na roho zao.

CHADEMA msijisumbue kukata rufaa katika mahakama ya CCM ni kupoteza muda, tuleteeni hoja zenu na sisi wananchi tutatoa hukumu murua kuliko hata ile ya Arumeru Mashariki.

Mipango ya SIRI kukidhoofisha CHADEMA kwa kumuondoa Kamanda Lema ubunge, Mhe Tundu Lissu pamoja na Mhe John Mnyika tayari tunazo hadi kitu gani kimepangwa kufuatia mara baada ya mazoezi hayo kukamilika kwa jina CCM dhaifu kinavyokusudia kufanya hivi sasa.

Sasa ni jukumu letu sisi sote Nguvu ya Umma kushirikiana na CHADEMA kwa dhati kabisa kuwalinda viongozi wetu hawa wanaolengwa na MAFISADI kwa kushirikiana na KIRUSI chao tulionaye katikati yetu hivi sasa. Silaha murua hapa ni kutumia nguvu ya kura zetu.

Kila Mwana-CHADEMA kauli mbiu yetu tangu sasa ni PIGA KURA LINDA ILI WALALAHOI TUPATE AHUENI!!

Utaifa mbeeele kama tai katika kukomboa taifa letu toka katika mikono ya MAFISADI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 
Hivi hakuna adhabu kwa Jaji endapo itaonekana hukumu yake ilikuwa na hila? Au akishaamua inakuwa ni kauli ya mwisho? Hivi Mahakama ya juu iki-review hukumu na kugundua Jaji "alipotoka" adhabu yake ni nini? Upuuzi huu usiporekebishwa, wanasiasa watachezea mahakama kadiri wanavyotaka.
 
Umejitahidi sana kuandika na kuweka wazi nawazo yako.Lakini kumbuka kuwa kesi hii mi ya kisiasa. Kesi za kisiasa mara nyingi za haki, kwa maana kuwa haki huwa haifuatwi bali hufuatwa matakwa ya aliye juu.
Kwa hili la Arusha mjini ni kuwa kama Chadema wakikata rufaa basi huenda ikawa hakuna uchaguzi hadi ule wa 2015.Kazi hapa ya mahakama itakuwa ni kuahirisha kesi hadi uchaguzi mkuu ujao.
Kwa hiyo ni heri kupambana tena ksms kuna uhakika wa kushinda tena.

wewe kweli ni great thinker nimekukubali make huyu ndugu yetu hakulijua kabisa hili la kesi kuzungushwa hadi 2015.CDM Wako sawa muno, na hapo kitakachofanyika nikufungua kesi ya kupinga hukumu baada ya uchaguzi mdogo kuisha.
 
Ikulu imemshauri mh lema kama anaona hakutendewa haki, akate rufaa! Wait a minute...! Chadema/ Lema wameanza lini kushauriwa na ikulu? Tutashuhudia mengi mwaka huu.
 
Umeeleza vyema kabisa, ila ukweli ulioko ni kwamba watu wa Arusha wanataka kupiga kura za hasira yaani huu uchaguzi ukifanyika ccm wakipata kura 500 wakatambikie watu wamekasirishwa sana na hili tukio, pia ufahamu kwamba mfumo mzima wa kimahakama umeonyesha kwamba hukumu yenyewe imetolewa kimtego hivyo kukata rufaa kunaweza kuwapa ccm kile wanachotaka kila mtu Arusha anataka Lema agombee lakini tusubiri tuone maelezo ya wanasheria kama Lema ataweza kuwa cleared ili kuruhusiwa kugombea. Ku base kwenye somo kwamba lazime lema akate rufaa na chama kisubiri inamaanisha arusha itakosa muwakilishi na hili linaweza kukidhohofisha chama.
hivyo basi kama Lema asiporuhusiwa kugombea, chama kichague mgombea mwingine ambaye atawakilisha Arusha kwenye uchaguzi mdogo. Alafu Lema afungue kesi upya kushirikiana na chama kuomba kesi yake ipitiwe upya ili kifungu kinachombana asigombee kiondolewe ili aweze kushiriki 2015. Napenda kusema kwamba Arusha tunamuunga mkono Lema na tutakuwa nae hatua kwa hatua kuhakikisha haki inatendeka


haya ndio maoni yangu.
 
Kwa kifungu alichokieleza mleta mada ni kweli hawezi gombea.

Judge amepitiwa maana hakuna ushahidi kuhusu rushwa ambao ulielekezwa katika mwenendndo mzima.

Hivyo the only way nikupeleka maombi Mahakama Kuu ili iweze yenyewe ku rectify error on judgment au vinginevyo kuomba marejeo "Revision" Mahakama ya Rufaa, lakini kama kuna kamchizo kanachezwa utasikia Mahakama haina fungu mara hooo sijui ..... kibao mara 2015.

hakukosea huyo jaji waliompa pesa zao ndio moja ya masharti waliyompa hicho kipengele amekitafuta ili kukidhi moja ya masharti ya wale waliompa pesa zao na ndio maana ningependa kaka Lema akate rufaa na mungu jaalia kesi hii ikifika mikononi mwa jaji ambaye ni mkweli atatupilia mbali kipengele hicho pia na makosa ya kashfa yote kwa sababu wahusika hawakuweza kuwakilisha chochote si tape wala video kuthibitisha madai yao kwahiyo jaji ameamini maneno yao bila ya wao kuyathibitisha.
 
Kwa kifungu alichokieleza mleta mada ni kweli hawezi gombea.

Judge amepitiwa maana hakuna ushahidi kuhusu rushwa ambao ulielekezwa katika mwenendndo mzima.

Hivyo the only way nikupeleka maombi Mahakama Kuu ili iweze yenyewe ku rectify error on judgment au vinginevyo kuomba marejeo "Revision" Mahakama ya Rufaa, lakini kama kuna kamchizo kanachezwa utasikia Mahakama haina fungu mara hooo sijui ..... kibao mara 2015.
Ni kweli haki haikutendeka na Jaji kwa sababu anazozielewa vema amechomekea kipengele cha Lema kutogombea kwa makusudi ili akikata rufaa izunguushwe hadi uchaguzi Mkuu. Kesi hii ina mkono wa siasa na kama tetesi zilivyo licha kukanusha vikali ikulu inahusika kikamilifu katika kutengeneza hukumu ya kesi hii kwa hiyo kukata rufaa kutawapa wahujumu hawa nafuu na uchochoro wa kuficha madhambi yao, ambapo wataingilia kati tena kushinikiza isiishe mapema hadi karibu na uchaguzi wa 2015. Dawa ya hujuma hii ni CHADEMA kuikubali hukumu,ili jimbo litangazwe wazi na CCM wasulubiwe vilivyo katika uchaguzi unaofuatia ambao hata hivyo matokeo yake yanatabirika. Natamani huyo Biriyani wao aje tena kugombea ili safari hii apewe doze ya kustaafu kabisa siasa. Vyovyote ilivyo hukumu hii inaiweka pabaya tashwira ya Mahakama katika nchi hii sawa na ile kesi ya Mtikila ya mgombea Binafsi iliyomalizwa kihuni. Historia itamhukumu Jaji huyu na kumfanya ajute.
Kuhusu Lema, yeye ni mwanaharakati na ni mpambanaji mwenye uwezo wa kuendeleza harakati za ukombozi hata akiwa nje ya Bunge.
 
Sasa ndugu yangu kwa kuwa ni hukumu ya kisiasa tukubali kumtelekeza LEMA asigombee kwa miaka mitano kwakosa ambalo hajatenda ila CCM na Mafisadi wamemtengenezea kwa kumuamuru Jaji aliweke katika hukumu?
Mdogo wangu, ni vizuri sana kuwa una roho ya kutaka mabadiliko katika nchi hii. Uko sawa kabisa. Lakini kwa Chadema kukata rufaa inategemea msimamo wa mahakam kama utaisikiza rufaa hiyo tuseme ndani ya siku 60 na kutoa maamuzi. Lakini kama ikiwa inaendeshwa kwa rimoti kama ilivoonekana huenda Chadema ikakosa bara na pwani kwa kuahirishwa kwa rufaa hiyo hadi 2015.
Kilicho cha maana ni kurufisha mpira uwanjani baada ya siku 90 tokea jana na kuwaonesha kuwa Chadema ni ya wana Arusha na Wana Arusha ni Chadema. Waachie wao washinde mezani lakini wana Arusha washinde uwanjani. Siku zote ushindi wa mezani si mtamu.
 
CDM hawatkiwi kufanya uamuzi wa papara kwani kunataarifa huu ni mpango mahususi uliopangwa na kimkakati ni kumtegea lema agombee wamuekee pingamizi.
 
Wana JF (Great Thinkers) wenzangu, naomba sisi tujipambanue na wadau wengine walioko Facebook.
Mimi naona hapa tutatoka povu bure na kupata sugu kwenye vidole vyetu kwa kugomabana na keyboard. Naweza kusema hii kesi imeamuliwa ki-mtego na kisiasa zaidi, hivyo basi inatubid sisi tusiingie kichwa kichwa katika mtego huo wa pumba. Kwa style hii, jinsi majadiliano yanavyoendeshwa hapa ni kama vile tunatumia ushabiki, Hisia na ghadhabu zaidi kuliko gemu yenyewe inavyotakiwa kuchezwa. Kuna vitu viwili hapa inabd tujiulize:


i). Je, Jaji kafanya makosa ya makusudi kuchanganya vifungu (Na. 108 na 114) katika kufikia maamuzi yake? au (Mimi naamini kwenye hili)


ii) Je, Jaji kapitiwa (kajichanganya) kwa kuvichanganya vifungu viwili vya Sheria?! (mimi siamini kwenye hili).


Na kama kafanya kwa makusudi kuchanganya vifungu vya Sheria, na hapa ndo kwenye mtego wenyewe. Ili kujibu swali hili, hapa tunahitaji angala tuweze kusoma Hukumu yenyewe, tuafuatilie kwa karibu tuweze kujua kuwa Jaji katumia reasoning gani katika kufikia maamuzi yake, na sio ku-base katika mistari miwili ya Hukumu hiyo iliyoandikwa katika Gazeti la mwananchi.
 
Nimeufuatilia mtiririko wa mawazo yako, naanza kubadili msimamo wangu nilokuwa nao kuwa cdm wasikate rufaa na kwasasa naweza kuwashauri cdm wakate rufaa.

Natumaini baada ya kushauriana na wanasheria wao, CDM watatoka na uamuzi makini na wa busara ambao utakuwa na tija si kwa cdm tu bali zaidi kwa taifa zima la Tanganyika!
 
Kwa kifungu alichokieleza mleta mada ni kweli hawezi gombea.

Binafsi na kwa dhati kabisa naomba na nina shauri CDM wakate rufani ili hukumu itakayofuata baada ya rufaa hiyo itumike na umma wa watanzania wote kujua na kujiridhisha pamoja na mambo mengine kuwa mahakama zetu zinasimamia haki kweli ama zipo hapo zilipo ili kulinda na kusimamia dhuluma, unyonyaji, uonevu & ukandamizaji dhidi ya umma na taifa zima la watanzania!
 
haki ya mungu haipotei arusha tutaweka hata jiwe tu tutashinda cha kusikitisha kodi za warara hoi hawa zinaliwa hebu tumogope sar good ira hata kama kunauchaguzi chochote kile kitakacho wekwa hata ng'ombe tunatoka
 
Back
Top Bottom