Napinga kwa nguvu zote CHADEMA kutokata rufaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Napinga kwa nguvu zote CHADEMA kutokata rufaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Naloli, Apr 6, 2012.

 1. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Baada ya hukumu ya kupinga matokeo ya Ubunge Arusha Mjini kutoka na Mh. Godbless Lema kuvuliwa Ubunge, nimesikia kauli ya Mh. Godbless Lema na Viongozi wa CDM kuwa wako tayari kutokata Rufaa ili uchaguzi ufanyike mapema na warejeshe jimbo lao. Kiukweli mimi sihafikiani na Uamuzi huo. Sababu zangu ni kama zifuatazo:-

  MOJA; Kwa mujibu wa hukumu Lema amepatwa na hatia kwa kukiuka kifungu cha108 kifungu kidogo cha pili A (kimsingi anaye kutwa na hatia kwa kiuka kifungu hiki anaruhusiwa kugombea tena UBUNGE) yaani kukutwa na kosa chini ya kifungu hicho uzuhiwi kugombea tena Ubunge. Lakini ajabu ya mwaka Jaji katika majumuisho ya hukumu jaji ametumia kifungu cha 114 cha sheria ya Uchaguzi kumzuia Mh. Lema kugombea tena UBUNGE baada ya kupatikana na hatia. Kwa kifupi kifungu hiki cha 114 utumika kumzuia kugombea Ubunge Mbunge aliyetenguliwa Ubunge wake kwa kukutwa na hatia ya kujihusisha na makosa ya RUSHWA. Kwangu mimi mkanganyiko huu si wa Bahati mbaya bali ulikusudiwa.( kwanini naamini hivyo) Wiki hii nilituma POST hapa JF na kueleza kuwa nimepata taarifa ya Mh. Lema kuvuliwa Ubunge wake na kuwa atazuiwa kugombea Ubunge tena, niliweka wazi kuwa taarifa hizo zimezagaa Arusha na CCM wamepanga hadi sherehe ya kujipongeza, na Mpango huo wa kumvua UBUNGE Lema uliasisiwa na kiusimamiwa na timu nzima ya EL. Na kweli nilichokieleza kimetimia. SWALI. Je kumzuia Lema kugombea tena Ubunge kwa kosa ambalo hajakutwa nalo yaani kosa la RUSHWA ni sahihi? au ndio Jaji alikuwa anatekeleza Maagizo ya MABWANA ZAKE? kwa kuamua KUIBAKA HAKI.
  PILI napinga CDM kukokata Rufaa kwa sababu HUKUMU hii (yaani kipengele cha kumzuia LEMA kugombea Ubunge) kinakiathiri chama kwa upande mmoja lakini ni athari ndogo kwa CDM maana wanaruhusa ya kumsimamisha mtu mwingine isipokuwa Lema tu. Lakini hukumu hiyo ina athari zaidi kwa LEMA maana kwa kusimamishwa miaka mitano kutogombea UBUNGE kuna maanisha hata mwaka 2015 haruhusiwi kugombea. Sasa kwanini CDM na LEMA wakubari LEMA abebe msalaba wa dhulma peke yake? Kwanini CDM wakae kimya wakati wanajua wazi hukumu hiyo si ya haki kwa LEMA? Kwanini CDM imtelekeze LEMA kwa ajili ya kulipata JIMBO la ARRUSHA MJINI?

  TATU; CDM
  iliwavua Uanachama na Udiwani Madiwani wake watano wa kata tofauti Arusha mjini kwa sababu ya kuingia makubaliano na CCM kuhusu UMEYA wa Manispaa ya Arusha bila Ridhaa ya CHAMA. N ukiangalia Idadi ya madiwani wa cdm na ccm ukiweka na wa Tlp ni wazi CDM hata kama UCHAGUZI wa MEYA ungefanyika na wao kuweka mgombea walikuwa na nafasi finyu ya kushinda LAKINIA msimamo wa CDM ulikuwa ni lazima UCHAGUZI urudiwe ili sheria na Haki ziheshimiwe bila kujali wao watashinda au kushindwa cha msingi HAKI ITENDEKE. Kama HAKI nia msimamo na msingi wa CDM hadi kuwatosa Madiwani watano ambao walishindwa kusimamia hilo, Je kwanini wamtose LEMA eti kwakuwa wana uhakika wa kupata Jimbo la Arusha Mjini?

  NNE: kuna wapiganaji watatu waliuwawa na polisi kwa kushiriki maandamano ya kupinga CCM kubaka Demokrasia na kujipitishia MEYA kibabe, Marehemu hawa waliandamana na kupoteza maisha yao sababu ya kusimamia HAKI na walikufa wakiamini CDM wanasimamia HAKI kwa gharama yoyote. Sasa leo inakuwaje CDM wanashindwa kuwaENZI marehemu hao kwa kuendelea kusimamia HAKI kwa gharama yeyote hata kwa kupoteza jimno la LEMA ili HAKI dhidi ya LEMA yaani HAKIA ya kugombea arejeshewe?

  TANO; (Hapa wanasheria watanisaidia) kisheria kuana kitu kinaitwa (RUFAA) APPEAL na JUDICIAL REVIEW, Kwanini CDM wasitumie hiki kipengele cha pili yaani JUDICIAL REVIEW kuiomba mahakama KUU au ya RUFAA kuifanyia REVIEW mwenendo mzima wa kesi ili kuona kama Hukumu ya kumzuia LEMA kugombea ndani ya miaka mitano hipo sahihi au la< kama haipo sahihi imtake Jaji kurekebisha kipengele hicho katika HUKUMU yake?

  MWISHO; Hoja kuwa wananchi wa ARUSHA watakosa muwakilishi BUNGENI kwangu siioni kuwa ya msingi maana ni CDM haohao ambao wanawakosesha haki ya uwakilishi ktk baraza la madiwani wananchi wa ARUSHA wa KATA TANO baada ya kuwavua uanachama kwakuwa madiwani hao hawakuheshimu msimamo wa chama kuhusiana na HAKI. Je ni sahihi wananchi wa ARUSHA wawe na MBUNGE wa kuwawakilisha BUNGENI wakati MBUNGE wao LEMA hakutendewa HAKI kwa kuzuia kugombea? kwanini haki wapewe wanajimbo la ARUSHA Lema anyimwe? Hivi ni sahihi kumnyima mtu haki kwa kigezo kuwa wengi watakosa uwakilishi Bungeni? Mbino kwa miaka 50 wamepata UWAKILISHI lakini hadi leo wanalalamika kuwa Wawakilishi hao hawakuwasaidia na kuwafanyia kazi waliyowatuma? Hivi si kuna majimbo yana WABUNGE lakini uwajibikaji huo wa wabunge hao kwa wananchi ni sawa na JIMBO kuto kuwa na MBUNGE?
   
 2. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Umejitahidi sana kuandika na kuweka wazi nawazo yako.Lakini kumbuka kuwa kesi hii mi ya kisiasa. Kesi za kisiasa mara nyingi za haki, kwa maana kuwa haki huwa haifuatwi bali hufuatwa matakwa ya aliye juu.
  Kwa hili la Arusha mjini ni kuwa kama Chadema wakikata rufaa basi huenda ikawa hakuna uchaguzi hadi ule wa 2015.Kazi hapa ya mahakama itakuwa ni kuahirisha kesi hadi uchaguzi mkuu ujao.
  Kwa hiyo ni heri kupambana tena ksms kuna uhakika wa kushinda tena.
   
 3. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280

  Hebu nisaidie kitu kimoja mkuu ambacho labda mimi sijakipata vizuri, kwa mujibu wa hukumu ya jana, LEMA anaruhusiwa kugombea tena au la??
   
 4. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  KWA kwa mujibu wa HUKUMU LEMA haruhusiwi kugombea. Embu soma vizuri kipengele cha kwanza cha post yangu nilicho kiandika MOJA
   
 5. d

  denilson Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kifungu alichokieleza mleta mada ni kweli hawezi gombea.

  Judge amepitiwa maana hakuna ushahidi kuhusu rushwa ambao ulielekezwa katika mwenendndo mzima.

  Hivyo the only way nikupeleka maombi Mahakama Kuu ili iweze yenyewe ku rectify error on judgment au vinginevyo kuomba marejeo "Revision" Mahakama ya Rufaa, lakini kama kuna kamchizo kanachezwa utasikia Mahakama haina fungu mara hooo sijui ..... kibao mara 2015.
   
 6. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa ndugu yangu kwa kuwa ni hukumu ya kisiasa tukubali kumtelekeza LEMA asigombee kwa miaka mitano kwakosa ambalo hajatenda ila CCM na Mafisadi wamemtengenezea kwa kumuamuru Jaji aliweke katika hukumu?
   
 7. d

  denilson Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kifungu alichokieleza mleta mada ni kweli hawezi gombea.

  Judge amepitiwa maana hakuna ushahidi kuhusu rushwa ambao ulielekezwa katika mwenendndo mzima.

  Hivyo the only way nikupeleka maombi Mahakama Kuu ili iweze yenyewe ku rectify error on judgment au vinginevyo kuomba marejeo "Revision" Mahakama ya Rufaa, lakini kama kuna kamchizo kanachezwa utasikia Mahakama haina fungu mara hooo sijui ..... kibao mara 2015. [​IMG] [​IMG] Edit Post [​IMG] Reply [​IMG] Reply With Quote [​IMG]

  [HR][/HR]  [h=2]JamiiForums Message[/h]


  Cancel Changes


  [h=3]Errors[/h] [h=3]The following errors occurred with your submission[/h]
  Okay


  [h=3][​IMG][/h]
   
 8. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivyo sehemu niliyo iwekea rangi Blue ndio naona ni suluhisho la tatizo hili kuliko lulimbilia katika uchaguzi huku tukimtelekeza Mpiganaji mwenzetu eti tu ARUSHA inaweza kukosa mbunge hadi 2015
   
 9. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  OK, nashukuru kwa hii explanation. Pamoja kamanda.
   
 10. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Umetumwa wewe manake plan zenu ilikuwa si kurudia uchaguzi kwa sababu kwanza hela hamna, mtu wa kumsimamisha ili apambane na cdm lazima atakunya makundi matatu c mawili lakini la muhimu na ambalo lipo wazi ni kushindwa vibaya hivyo ninyi kuaibika zaidi!
  Sasa usituchorenge! pateni mlichotaka sisi tunawasubiri kwenye kura! siku zote mwisho wa ubaya aibu!!
   
 11. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante sana Mkuu kwa maelezo safi kabisa! Natumaini baadhi ya viongozi watapitia hii pia itawasaidia kutoa maamuzi sahihi hapo kesho ila naomba Jamani kama amepigwa stop kugombea naomba chadema wakate rufaa jamani kuliko kumpoteza kamanda wetu hivihivi!
   
 12. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Mpaka sasa sielewi nani mkweli na nani ananipotosha, wengine ooooooh Lema haruhusiwi kugombea, wengine oooooh Lema anaruhusiwa kugombea, kipi ni kipi hapa?
   
 13. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hukumu imekaa kimtegeo jamani! tusirudi mahakamani! haiwezekani uambiwe njia hii kuna chatu usipite wewe unapita! Jaji mkuu wa majaji JK alishajaji kama alivyomjaji babu sea na papii! so hakuna kurudi mahakamni 5 years Lema anakwenda kukijenga chama na sisi wana waarusha tunafungua mfuko wa kulipa mshahara kama wa mbunge wetu finito
   
 14. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yani mzee unategeka haraka! huyu katumwa yupo kazini huyo! we twende kwenye uchaguzi Lema ni mbunge wetu na sisi tutamlipa!
   
 15. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Haruhusiwi mzeee
   
 16. S

  Saitoti Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ilisemekana kwamba , Lema anaruhusiwa kugombea tena , Basi haruhusiwi basi Lema atate rufaa, ili jimbo libaki hadi 2015, Lema atakuwa anahirimalisha Chama , nasi wana Arusha tutakuwa tunamtambua lema kama Aliyekuwa mbuge wa Arusha mjini. ili Ccm wapoteze na CC tupoteze
   
 17. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wellsaid mkuu jinsi hiyo issue ilivyokaa ni kweli jaji alijichanganya wakati wa majumuisho kosa alilopatikana nalo lema ni illegal campaign na siyo illiegal practice.
  Mytake:Wakili wa Lema inabidi awasiliane na jaji iliaclarify kuwa huo mkanganyiko wa vifungu alikosea au lah! Lengo la magamba ilikuwa ni lema akate rufaa ambayo ingemuweza kuendelea kuwa mbunge kitu ambacho kingepeleke delidali na hukumu ingetoka mwakani na kama bado mahaka ya rufaa ingemtia lema hatiani jimbo la arusha lingebaki wazi mpaka 2015 coz sheria ya uchaguzi inasema kama jimbo litaachwa wazi miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu hakutakuwa na ujazwaji wa hiyo nafasi.
  Wanasheria mtanirekebisha kama nimekosea.
   
 18. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  mtoa maada ana mantiki, tusimame katika kutetea hati za jamii na raia mmoja mmoja(lema) anastahili kukata rufaa kwa ajili ya kurekebisha hayo makosa ya kisheria ili haki ya mtu isipotee.
   
 19. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mie nashauri chadema wakate rufaa! Haki tunayoidai kila siku lazima tuendelee kuidai! Mambo ya kusema jaji alijichanganya sio kweli. Hivi mnataka kuniambia kuwa huyo jaji alikaa mezani mwenyewe na kutoa hukumu? Hamuoni kuwa hiki ni kikundi cha watu wasomi wahuni wanaotumiwa na mafisadi? Ninapata hasira sana ninapoona mtu anasema jaji alijichanganya katika hukumu!!!!! Naamini mapambano ya kudai haki ya vyama vya upinzani ni zaidi ya vita yoyote iliyowahi kupiganwa hapa duniani: let fight we will win, if not us our children will find us on the way fighting.
   
 20. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono hoja/mawazo yako 100% sina addition yoyote.
   
Loading...