mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,574
- 9,809
Mkuu nakupa kongole nyingi kwa hoja ulizojenga juu ya ubora unaopaswa kuwepo ktk masuala ya elimu. Kuna kasumba mbaya imejitokeza hivi karibuni kwa viongozi kutoa ushauri wenye fikra za kimaskini na ufukara.
Kumejitokeza kasumba ya kuwataka watu kutokuwajibika ama kukumbatia vitu duni kama sababu ya kujionyesha kuwaonea huruma. Kibaya zaidi ni kutaka kuhadaa tabaka linalotawaliwa ili kuhalalisha "mentality" za kimaskini kuwa ndiyo uzalendo wenyewe.
Kuzaa ni wajibu mpana unaohusisha chakula, malazi, mavazi, elimu, bima na vitu vingime muhimu kwa ajili ya makuzi ya watoto na kujenga familia bora. Kisingizio cha kulalamikia gharama kwa wazazi hukuondoi wajibu huu.