Alwatan kamba
Member
- Nov 16, 2020
- 70
- 236
Leo kwenye uzinduzi wa ofisi ya makao makuu ya wilaya ya kahama, mbunge wa jimbo hilo mh. Kishimba ameiomba serikali kupiga marufuku wanafunzi kulazimishwa kununua madaftari aina ya 'counter book'. Pia ameiomba serikali kuruhusu wanafunzi kuvaa viatu vya rangi yoyote kwakuwa viatu havisaidii chochote kwenye elimu isipokuwa maarifa wanayopata shuleni.
Kwanza nianze kumpongeza mheshimiwa kishimba kwa kuwa kinara wa kuibua mambo mbali mbali ya kielimu na kuishauri serikali hatua za kuchukua.
Pili nakubaliana na mheshimiwa kishimba ya kwamba ni kweli viatu havisaidii chochote kwenye elimu ya mwanafunzi isipokuwa maarifa anayofundishwa na walimu wake.
Pamoja na kukubaliana na hoja hiyo, nampinga mheshimiwa mbunge kwa mambo yafuatayo;
HOJA YA VIATU VYEUSI
(i) viatu vyeusi ni sehemu ya sare za shule. Sare hizi husaidia kumtambulisha mwanafunzi pamoja na shule.
(ii) viatu vyeusi vinasaidia kupunguza utoro shuleni. Kwakuwa viatu vya rangi nyeusi havishiki uchafu kwa wepesi tofauti na rangi zingine mf. rangi nyeupe ni rahisi kwa wanafunzi kuhudhuria vipindi shuleni bila kusingizia kwamba viatu ni vichafu.
(iii) Rangi nyeusi ndio rangi inayopatika kwa wingi kuliko rangi nyingine kwenye viatu. Hivyo hata upatikanaji wake ni rahisi.
(iv) viatu rangi nyeusi husaidia kupunguza matabaka kwa wanafunzi. Kama nilivyotangulia kusema viatu ni sehemu ya sare 'uniform' hivyo vikiwa vya rangi ya kufanana kwa wanafunzi wote husaidia kupunguza tabaka kati ya mwanafunzi anayetoka kwenye familia ya wenye nacho na wasio nacho.
(v) viatu vyeusi ni sehemu ya mafundisho kwa wanafunzi kuhusu namna ya uvaaji wa kihaiba 'smart' na hivyo kuwafanya wawe na mwonekano nadhifu pindi wawapo shuleni na wamalizapo masomo.
(vi) kwakuwa hoja ya mheshimiwa mbunge imejikita kwenye kuwapunguzia wazazi gharama na endapo hoja hiyo ikafanyiwa kazi tusitegemee itaishia hapo.
Endapo hoja hiyo itatatuliwa tutarajie wazazi kwenda mbali zaidi kudai na uniform zingine ziondolewe kwa sababu nazo ni gharama hivyo mwisho wa siku kila kitu kitafanyike nje ya utaratibu na matabaka kwa wanafunzi yataongezeka.
HOJA YA MADAFTARI AINA YA COUNTER BOOK
Mheshimiwa mbunge amelalamika kuwa daftari aina ya counter book zinauzwa bei kubwa hivyo zinawaongezea wazazi gharama. Kwa mtazamo wangu naona ni sahihi wanafunzi kutumia counter books kwa sababu;
(i) daftari zinazouzwa kati ya 250 - 300 ni ndogo sana kiasi kwamba mwanafunzi akiandikia kipande kidogo cha mada 'sub topic' linaisha hivyo ni sahihi kabisa wanafunzi kutumia counter books kwakuwa zina nafasi 'space' kubwa na kurasa 'pages' nyingi na haziishi mapema.
(ii) counter books zinasaidia kupunguza usumbufu kwa wazazi kununua madaftari kila wakati kwakuwa zinachukua muda mrefu aghalabu mwaka mmoja na ushee bila kuisha lakini daftari ndogo ndani ya week 2-3 au hata week moja haizimalizi hivyo kufanya wazazi kununua daftari kila wakati.
(iii) counter books zinasaidia kupunguza migogoro ya kifamilia kati ya mwanafunzi na wazazi. Kwakuwa daftari ndogo hujaa mapema kuna wakati wazazi wanakuwa 'reluctant' na kuwashutumu watoto wao kwa matumizi mabaya ya madaftari jambo ambalo hupelekea baadhi ya wazazi kuacha kabisa kuwanunulia. Ikumbukwe migogoro kama hii ikitokea hata 'performance' ya mwanafunzi shuleni hushuka kwa sababu ya ukosefu wa nyenzo muhimu 'madaftari' ya kujifunzia.
(iv) kwakuwa counter books hununuliwa kwa gharama kubwa hata utunzaji wake wanafunzi huuzingatia sana tofauti na daftari ndogo ndogo.
(v) kutokana na daftari ndogo ndogo kujaa haraka, hulazimu wazazi kununua nyingi kwa mwaka ambapo kimahesabu gharama inayotumika kuzinunulia inakuwa sawa au hata kuzidi kabisa gharama iliyotumika kununulia counter book moja.
HOJA YA MABEGI
Mheshimiwa mbunge pia amedai ni gharama wazazi kuwanunulia wanafunzi mabegi ya shule.
Yamkini inaweza kuwa hoja nzuri lakini mheshimiwa mbunge akumbuke kuwa mabegi ni kwaajili ya usalama wa vifaa vya mwanafunzi mwenyewe na vifaa au mali anazo azima mwanafunzi shuleni kama vile vitabu. Ili kuhakikisha vifaa hivyo vinakuwa salama muda wote hasa kwa vipindi korofi kama vipindi vya mvua au hatari yoyote ya upotevu na uharibifu ni vyema vikahifadhiwa kwenye begi.
Ushauri wangu: kufuatia hoja zilizotolewa na mheshimiwa mbunge na kwakuwa hoja zake zote zimelenga eneo moja la gharama nikiwa kama mdau wa elimu nashauri serikali iweke mikakati madhubuti ya kudhibiti upandaji holela wa bei za vifaa vya shule hasa nyakati vipindi vya shule vinapokaribia kwakuwa ndio chanzo cha gharama kuwa juu. Namaanisha tabia ya baadhi ya wafanya biashara wachache ambao sio waaminifu kuuza vifaa vya shule kwa bei kubwa pindi shule zinapokaribia kufunguliwa ikomeshwe.