Napendekeza, Serikali yetu itenge Eneo maalumu kulisha Afrika!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Liwe ni kwa ajili ya kulima mazao kama Mahindi kwa ajili ya export kwa nchi za Kiafrika tu zenye uhaba wa chakula kama Kenya, Zimbabwe, Malawi &Co. binafsi imenishtua sana kusikia Nchi ya Kenya inaagiza Mahindi ktk nje ya Afrika!
Tukiweza kufanya hivi hii ni win - win situation kwani tunaweza pia huko mbele ya safari kutumia kama bargaining chip mambo yanapokwenda ndivyo sivyo!

Naamini kabisa Kusini mwa nchi yetu Mikoa ya Ruvuma huko au Umasaini pia hatukosi eneo kubwa ambalo linaweza kutumika kwa ajili hiyo tu, kulisha Afrika, ...
 
Sijawahi kupenda mada/mchango wako wowote kabla ya leo. Kifupi nakuchukia kama ninavyowachukia CCM wengine wengi (sio wote).
Ila leo, mashallah, umekuja na wazo murua sana; multi-billion-dollar idea. Kongole mwana wane. Inahitaji kuwa vizuri kichwani kuja na wazo kama hili.

Tukifanya jambo hilo kwa weleldi walahi watu wetu na taifa kwa ujumla tutaona nuru ya maisha bora. Tuna kila kitu kulitekeleza hilo (ardhi nzuri, maji ya kutosha na nguvu kazi); ni uamuzi tu
 
we can't feed our people how the hell we can manage to feed others!!!!acha bange,njaa bado ipo mikoani huko
 
Ni wazo chanya, ila tatizo ni Viongozi wa Tanzania hawana vipaumbele, hayo mashamba tunaweza kufanikiwa tu ikiwa tuna uhakika wa maji ya kumwagilia kwa sababu kilimo cha kutegemea maji ya Mvua ktk karne hii ni sawa na Mgonjwa anayetegemea nguvu za mganga wa kienyeji kupona ktk karne hii.
 
MIMI NI MKEREKETWA WA MASWALA YA UHIFADHI WA CHAKULA CHA KUTOSHA KWA AJILI YA WANAINCHI WETU.
MARA NYINGI NIMEKUWA NANUKUU MANDIKO MATAKATIFU TOKA KWENYE MISAFU NA HASA NJAA ILITOKEA INCHI YA MISRI KWA KIPINDI CHA MIAKA SABA.
HAYATI MWALIMU NYERERE ALITOA KIPAO MBELE CHA KWANZA KWA AJILI UHIFADHI WA CHAKULA.
ALIJENGA MAGHALA KILA MKOA, WILAYA NA HATA SEHEMU ZINGINE ALIJENGA MAENEO YA VIJIJINI (TRANSIT SHEDS).
ALIHAKIKISHA KILA PUNJE YA ZIADA YA NAFAKA INAYOLIMWA NA MWANAINCHI INANUNULIWA NA SERIKALI KUPITIA MASHIRIKA YAKE.
MAGHALA MENGI YALIUZWA. SASA HIVI HAKUNA CHOMBO MAALUMU CHA KUKUSANYA NAFAKA KWA AJILI YA MATUMIZI YA SASA NA BAADAYE. BEI ZA NAFAKA ZIKO JUU SANA UKILINGANISHA NA BIDHAA ZINGINE.
HAKUNA BEI ELEKEZI YA NAFAKA.
KWA HIYO SWALA LA MSINGI SIYO KUWAZA KULISHA INCHI ZINGINE WAKATI TUNASHINDWA KUJILISHA SISI WENYEWE.
MAHINDI MENGI AMBAYO YALIKUWA YANATUMIKA KUSAGA UNGA KWA KIPINDI ZA MWEZI MACHI NA APRIL 2017 YALIKUWA YANATOKA UGANDA.
KWA MARA YA KWANZA MIKOA YA SINGIDA, SHINYANGA MWANZA N.K. ILIKUWA INATEGEMEA MAHINDI TOKA UGANDA.
TUMSHAURI RAIS WETU KUWA PAMOJA NA KUWEKA KIPAO MBELE KWENYE MASWALA YA MIUNDO MBINU LAKINI INCHI HAITAJUWA NA HESHIMA KAMA HAINA AKIBA YA KUTOSHA YA CHAKULA.
 
Back
Top Bottom