Napenda utumbuaji majipu lakini sipendi demokrasia ikikandamizwa nchini

Mjasiriamali1

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
891
237
Mkuu wa kaya sisi maboss zako tuliokupa tiketi tunafurahia nia yako na utendaji wako. Nia yako ni njema! Na kila mtu anaipenda kwa kweli! Ni wajibu wetu kutoa ushauri kuliko kulaumu. kwa kuwa walioko chini yako wanakandamiza demokrasia kwenye kaya please act and do something mwisho wa siku watakuharibia sifa kubwa uliyojitengenezea! Ongea na walio chini yako waache viongozi wa upinzani waongee! Wakiongea wewe unatenda mkuu! Action speaks louder more than words! You give them credits unnecessary! kwa wapinzani Sababu ukiwanyamazia walio chini yako kutumia nguvu vibaya kuwanyamazisha wadau kwa nguvu. Ninajua hata huku unapita mkuu wa kaya. Do something! Ivyo nimea ndika makusudi. Mzee wetu aliyeenda kuwa mkulima, aliyokuachia kaya aliruusu demokrasia! Hawa watu wakiongea mkuu wanazuia vip speed 360 yako! Tubishane hoja kwa hoja! Sio hoja kwa misuli, Jinsi watu wako wanavyotumia nguvu vibaya kuwakandamiza upinzani ndivyo mnavyowapa credit! Na mwisho wa siku hakuna fair competition, kama hawa wameongea nyie kazi yenu kujibu kutolea maelekezo, lakini SIO KUWANYAMAZISHA! Kwa misuli bana. MKUU WA KAYA SISI MABOSS WAKO! tunakushauri ili 2020 usije ingia na wabunge wa chama chako chini zaidi ya sasa! Ujue macho yetu yanaona mkuu.
 
Amesema yeye sio rais wa matajiri ni rais wa masikini.
Atahakikisha wanaoishi kama malaika waishi kama mashetani.
Ila bajeti yake inadhihirisha tofauti.
 
Mkuu wa kaya sisi tunafurahia nia yako na utendaji wako. waache viongozi wa upinzani waongee! lakini SIO KUWANYAMAZISHA!.
You can't eat your cake and have it!. Huwezi kupenda utumbuaji majipu, lakini yakitumbuliwa majipu ya demokasia ndipo unapiga kelele!. Mtu akiwa ni dikiteta, ni dikiteta kote kote, anakata kama msumeno. unakata kote kote!, hivyo you just have to take the bitter with the sweet!, sio uchague vitamu tuu ndio umeze halafu vichungu uteme!, hiyo demokrasia yetu yenyewe nalo ni jipu tuu, lazima litumbuliwe!.

Baadhi ya hao wapigania demokrasia ndio madikiteta wakuu ndani ya vyama vyao, wengine wakifanya uchaguzi wa maigizo!, wengine wakinyofoa kinyemela, vipengele vya ukomo wa uongozi ndani ya katiba za vyama vyao ili watawale milele!.

Mimi ni miongoni mwa tuliomshauri mkuu wa kaya kama katiba ni kizingiti, ikibidi aiweke katiba pembeni, ainyooshe hii nchi kwa mkono wa chuma!, ikiisha nyooka ndipo tuirudie katiba!.
Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria

Pasco
 
Mkuu wa kaya sisi maboss zako tuliokupa tiketi tunafurahia nia yako na utendaji wako. Nia yako ni njema! Na kila mtu anaipenda kwa kweli! Ni wajibu wetu kutoa ushauri kuliko kulaumu. kwa kuwa walioko chini yako wanakandamiza demokrasia kwenye kaya please act and do something mwisho wa siku watakuharibia sifa kubwa uliyojitengenezea!... Ujue macho yetu yanaona mkuu.
Mkuu wa kaya, Baba J. anaiona na kuitambua demokrasia kwamba ni jipu kwa utawala wake.
Mkuu huyu wa kaya amebariki na kufanikisha ubakaji wa demokrasia Zanzibar.
Mkuu huyu amemteua Dr. Asiyetulia kuwa mwakilishi wake bungeni.
Mkuu huyu wakati anahutubia sherehe ya maadhimisho ya miaka 39 ya chama chenye hatimiliki ya kuitawala nchi ya wadanganyika alisema anaipenda sare ya chama chake na atahakikisha wadanganyika hata ndoto ya upinzani hawaioti.

Unapoona demokrasia inatumbuliwa elewa mkuu wa kaya anahusika kwa aina moja au nyengine.

Demokrasia inamletea fyokofyoko ni lazima aitumbue. Nimesikia Mkuu wa kaya anaiogopa demokrasia kama anavyoogopa "bungelive". Demokrasia inataka mawazo mbadala na kukosoana. Mkuu wa kaya hapendi kukosolewa vipi atapenda demokrasia?

Mlitaka "Rais" dikteta, sasa furahieni matamko elekezi. Dikteta na demokrasi ni kulinganisha malaika na shetani. Mtaishi kama mashetani na mtalimia meno, mtamalizia kwa kuisoma namba.
Unapotamani kuona Tanzania ya viwanda ni lazima uridhie mkuu wa kaya kuua demokrasi.
Wadanganyika tunataka domokrasi na hilo ndio tutalipata.
 
You can't eat your cake and have it!. Huwezi kupenda utumbuaji majipu, lakini yakitumbuliwa majipu ya demokasia ndipo unapiga kelele!. Mtu akiwa ni dikiteta kote kote!, hivyo you just have to take the bitter with the sweet!, sio uchague vitamu tuu ndio umeze halafu vichungu uteme!, hiyo demokasia yenyewe nalo ni jipu tuu, lazima litumbuliwe!.

Baadhi ya hao wapigania demokrasia ndio madikiteta wakuu ndani ya vyama vyao, wengine wakifanya uchaguzi wa maigizo!, wengine wakinyofoa kinyemela, vipengele vya ukomo wa uongozi ili watawale milele!.

Mimi ni miongoni mwa tuliomshauri mkuu wa kaya aiweke katiba pembeni, ainyooshe nchi hii kwa mkono wa chuma!.
Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria

Pasco
Yours is a very costly joke! Utashi wako ukibarikiwa utachekea choloni jamaa yangu, ogopa lawlessness kama ukoma!
 
Back
Top Bottom