Napenda sana upweke

Napenda sana upweke

Tape measure

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2015
Posts
1,988
Reaction score
3,688
Zamani nilikuwa napenda sana kutuma message, ikafika kipindi nikaona message ni kupotezeana muda mtu akinitumia meseji mimi sijibu nampigia. Ukafika muda ata nikiwa na dakika za kupiga simu Sipigi simu. Pia nikikuta meseji na missed call isiyo na umuhimu ama namba mpya sipigi kabisa. Ikitokea nikipiga sitaki maneno mengi kabisa.

Siku zinavozidi ndio namimi nazidi kupenda upweke. Kuna muda natamani kuzima simu kwa muda mrefu nisiwasiliane na watu mpaka Mimi nitakapohitaji kufanya hivyo.

Maisha yangu ni ya ukimya kuongea kidogo sana, Nina marafiki wachache na sijawahi mkaribisha yeyote anaenijua kwangu. Ni kawaida yangu tokea nikiwa Mdogo nilikuwa naenda kucheza nyumbani kwa wenzangu lakini kwetu. Hapana na siku marafiki wakija nyumbani nawatoa nawaambia twendeni tukachezee nyumbani kwa Fulani.

Sasa nimekua mtu mzima najishangaa muda mwingine ata ukiniambia upo karibu na kwangu nitakuelekeza nisubiri sehemu Fulani imenifanya niishi maisha ya siri sana sipendagi kutoa ABC zangu.

Kuna muda naweza kutofautiana na wife akinilaumu kwa nini usimkaribishe tu huyo rafiki yako nyumbani namkatalia, akiniambia rafiki zake wanakuja lazima nitoke home nakuwa sitaki tu wanione shemeji yao japo wananijua napenda tu kuwa scarcity.

Ukinidadisi sana nitakudanganya kulingana na unavyoweza nizania wewe. Nafurahi sana kuishi maisha ya watu kutonifahamu nafanya biashara lakini sipendi kufanya na majirani sijui ata kwanini lakini napenda tu iwe ivo. Napenda sana kujua mambo ya wengine ila mambo yangu ni Siri sana ata mtaa ninaoishi hawanifahamu kwa jina langu halisi zaidi ya Balozi na M/Kit wangu, sipendi mtu wa mtaa ajue ndugu zangu kwa namna yeyote ile.

Sipendi kabisa kukaa na watu wanaonifahamu kwa namna yeyote ile mimi ukinijua tu wazazi, nilikokulia na mambo mengine ya nyuma urafiki na wewe unakuwa mashakani sana.

Hata watoto wangu nawalea kama agents wa CIA ama KGB, kusoma vitabu sana, mafunzo ya karate na kazi pamoja na study za maisha. Michezo ni shuleni tu wakirudi home ratiba inaanza SAA 9:30 usiku wanalala

Jirani akinizoea sana sipendi kabisa mzoea huwa sijisifu kwa chochote napenda kupita njia tofauti tofauti, Mara zote huwa naishi kama vile Nina RB. Lakini sina tatizo kabisa na mtu . Ni mazoea tu.

Sipendi kuzoeeleka popote iwe bar ama club's. Sipendi kukaa eneo moja muda mrefu mfano bar lazima nibadili ata sehemu tatu kwa muda machache APA nazani sababu napenda kutembea.

Napenda sana kuelimisha watu kuhusu maisha na mengineyo angalau waweze kubadili mboga ila sio jambo rahisi kwani kuna muda ata Mimi nashindwa kubadili mboga na kadhalika.

Kuna muda I wish ningekuwa OCD / CID ila sijui kama wanatakaga loneness creature kama Mimi. Sipendi kabisa usumbufu naweza kukubali yes yes yes tu ili uondoke, sipendi kuongea sana na nikinywa pombe naongea kiasi ila vyote nitakavosema ni propaganda tu, stories, fictions ambazo haziusiani na Mimi kabisa na hufanya hivyo tu kusudi wasinitenge na kuniona mimi ni mkimya sana hapo nakuwa najilazimisha kuongea kuchangansha Genge.

I do enjoying being alone and in state of unknown for no reason hii imepelekea kuzaniwa Mimi labda nipo usalama wa taifa kwangu sioni kama ni sifa mbaya sana.

Mbaya sasa napenda sana siasa nafuatiliaga kila tukio la habari kwa kina za ndani na nje ya nchi. Kwa sasa natafuta pesa nikipata nyingi nitagombea ubunge mwaka 2035 Niwagawiapo na wananchi wangu kidogo wafurahi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
In short wewe Ni mchoyo na mbinafsi!! Zipo tabia ambazo hata ukiwa nazo inakua c tatzo sana kama tukokuongea sana sina shda na hlo, mambo yako meng kua secure hlo Galina shda lakn hili la kutokutaka hata marafk zako wafaham kwako?? Hlo Ni mbaya zaid
 
Mshurutishe mkeo atumie uzazi wa mpango otherwise utamzalisha kila baada ya miezi 7. Watu wa kujifungia tu ndani mda wote mnakuwaga juu ya vifua vya wake zenu maana ndo starehe pekee mliyobaki nayo
 
Hupendi upweke ila you are not outgoing (you are an introvert). Simply you like to keep to yourself like. Hapa jukwaani tu ndio natamba ila in reality sina mbwembwe mkimya sana wala sipendi kuongea napenda sana kusikiliza na kumsoma mtu zaidi.

Naweza kukaa mahali kuna mjadala lakini nikawa nasikiliza tu sichangii. In short kuna siku naweza kushinda penye watu kibao lakini nisiongee hata maneno 200 siku nzima.
 
Una dalili zote za kuwa muathirika wa bangi si bure! Though kuna wengine ni wanazaliwa na hali hio kama sisi wengine tusivyoweza ku-fake!/
Bangi sijawahi kuitumia direct labda indirect kwa moshi tu wa vijiweni na ziwani ila siichukii kama sigara huwa nashauri vijana kitaalamu Bangi ni nzuri kuliko sigara
Na Soda ni mbaya kuliko Pombe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya vitu vilivyonishinda maishan mwangu ni
1.Kuwa na rafiki ambae sina issue nae kama vile biashara, kaz n.k
2.Kutaja jina langu full
3.Kutaja kwetu nlikotokea
4.Kutaja kazi nnayoifanya
5.Kupiga smu kwa mtu ili kumsalimia yaan siwez n lazma kuwe na issue tunaizungumzia
6.Kuanzisha story itakayonihitaji mm nitoe taarifa zangu kama vile jina,dini,chimbuko langu,n.k
7.Staki mtu ajue mahali nnapoishi
8.Mtu akija hom kwangu najiskia sna amani yaan kama nimebanwa vile
9.Kupiga story za umbea no no No....ukinpigia smu ili ulete umbea ntakuskiizaaaa afu tunaagana
10.Maishani mwangu sjawahi kuwa na rafiki wa kudumu yan kama tunafanya kazi/biashara bas tutakua marafiki kwa mda huo baada ya hapo kila mtu afate yake mm siez pga smu wala sms (japo mara moja moja twaweza kuwasiliana)
11.Sna mazoea na ndugu zangu hata kdogo yaan nna urafiki na dadangu na kaka angu bhaaaasi.
12.Mambo mengi napenda kuyafanya kwa siri ktu knachofanya watu kuhsi mm sio mtu wa kawaida.
13.Nkiwa na tatzo spend mtu yyte ajue
14.Ninabadilika badilika sana yaan hata tukikubaliana jambo fulani bado huwa siridhiki,naendelea kulifikiria je hili jambo/biashara lina maslahi ???
15.mda mwingne ukinkuta naongea saanaaa lakn ukinikuta npo cool mkimyaaaa mpaka sio poa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom