Napenda mnyukano huu uendelee(wizara nishati na wafanyabiashara

mseseve

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
511
89
KUNA MALUMBANO YANAENDELEA KATI YA VIGOGO WA BIASHARA NCHINI WAKIWEMO MADALALI NA MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUHUSU SWALA LA GESI. Kilichopo ni kuwa kauli aliyoitoa waziri husika kuwa watanzania hawawezi kuwekeza kwenye swala la utafutaji mafuta imeonekana kuwachefua wafanyabiashara ambao ni wazawa/wazalendo kwani walitaka na wao wapewe fursa.
SWALA HILI LIMEPELEKEA MPAKA KUIBULIWA KWA MAMBO MENGINE YALIYOPO CHINI YA KAPETI KUHUSU WAFANYABIASHARA WANAOIHUJUMU WIZARA hasa KWA UPANDE WA TANESCO NA MADINI.
WAZIRI MWENYE DHAMANA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI ALISEMA MUDA WA KUCHEZEWA UMEKWISHA NITAWEKA WAZI WALE WOTE WANAOHUJUMU WIZARA(TANESCO NA MADINI) SIKU YA KUSOMWA KWA BAJETI YA WIZARA.
FAIDA YA HAYA MALUMBANO
1. Wananchi kuijua kweli kuhusu matatizo ya tanesco na hiyo kweli ituweke huru(tuchukue hatua)
2. malumbano yatapelekea kama kuna baadhi ya madalali na wafanyabiashara walio na wanaotaka kulihujumu shirika kuogopa na kukimbia au kujiondoa na mwisho kutapunguza idadi ya mchwa wala tanesco....faida kwa shirika.
3.Malumbano yatasababisha wafanyabiashara wanamtuhumu waziri kwa kubana..wahangaike kutafuta pesa ya kuwekeza pindi watakapo pewa nafasi hata kama walikuwa wanataka udalali kwenye mradi, ili wasijefedheheka kwa kauli zao, maana wakiwekeza ajira zitapatikana. na sio kudalalia.
4.Kama watawekeza kutaongeza fursa na udhubutu kwa watanzania wazalendo kujitokeza kwa wingi kwenye sekta ya gesi.(sio kudalalia kuwekeza)
FAIDA ZIPO NYINGI MALUMBANO YAENDELEE TUJUE MENGI KAMA KWENYE SAKATA LA EPA hata mimi nilieko TANDAHIMBA NAJUA KUHUSU EPA.
NB UDALALI HAUNA FAIDA KWA WANANCHI NI KWA MTU MMOJA MMOJA UKULINGANISHA NA UWEKEZAJI.
 
Back
Top Bottom