Napenda kumtahadharisha mh. Rais kikwete

Napenda kumtahadharisha mh. Rais kikwete

Fred Wk

Member
Joined
Mar 13, 2012
Posts
65
Reaction score
26
NAPENDA KUMTAHADHARISHA MH RAIS KIKWETE
KUHUSU KAULI YAKE!!
Jana akimpokea mgombea kiti cha Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ndg Pombe
Magufuli, wakati akienda kuchukua fomu kutoka
tume ya taifa ya uchaguzi mh Kikwete alijitapa
kuwa wapinzani ktk uchaguzi wa mwaka huu ni
sawa na timu ya mpira na watakua wakisimama tu
huku magoli yakiingia(wakifungwa).
Haikutosha alisema kwamba MWENYE MWALI NI
YEYE na kwamba atahakikisha anamlinda. Au kwa
maneno mengine ataamua yeye kuwa nani ampe
MWALI(Kiti cha Urais)
Kwangu mm naona km Mh Kikwete kwanza
ameonyesha mshutuko mkubwa sana kwa kuwa
hakuwahi kutegemea anayoyaona na kuyasikia
sasa. Hivyo basi anachojaribu kukifanya ni
kuwatisha UKAWA(mgombea wao) kwa kutumia
madaraka yake aliyonayo.
Naomba nimwambie mh Kikwete kwamba jambo la
MUNGU halijawahi kushindwa mahala popote na
kwamba anapotumia madaraka yake kuwatisha
wagombea wa vyama vingine hiyo sio demokrasia
ila pia asisahau kwamba cheo ni dhamana siku
moja anaweza kujikuta yeye ndie akaona cha
"Mtema kuni" badala ya hao anaowaambia.
Ajiulize GHDDAFI NA wanawe wako wapi leo
pamoja na kuwaita WALIBYA "Panya"?
Mtoto mkubwa wa aliekua Rais wa Libya
(marehemu sasa) yupo Gerezani na wiki iliyopita
alihukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa
kosa la kuwaamuru Majeshi kuuwa waandamanaji
waliokuwa wakipinga serikali ya Baba yake.
Inashtusha sana RAIS wa nchi kusema wapinzani
wataona cha mtemakuni na ikiwa hao wapinzani
watashinda je yeye hataona cha mtemakuni?
Mh Rais Siasa sio Uadui hata ifikie mahala utamke
maneno ya vitisho na kukebehi kwa vile tu ww ni
rais. Siku moja historia itakuhukumu kwa kauli na
dharau zako haswa ukiwa km kiongozi mkuu wa
nchi.
Tulidhani kwamba NAPE anavyoropoka ni kichwa
hakiko sawa sawa kumbe ni maagizo kutoka
kwako?
Tanzania ni mali ya kila Mtanzania na kwamba
uongozi wa nchi hauna hati miliki na chama
kimoja, mtu wa dini fulani au Wa kanda fulani.
Ikifikia huko basi tujue hatuna tena nchi isipokuwa
tusubiri vurugu.
Mh Rais nataka nikuhakikishie kwamba mwaka huu
hata km utatumia Majeshi, bunduki, vifaru na
Mabomu ili kumkabidhi MWALI kwa asiestahili kwa
kuwa tu ww ni Rais( mwenye mwali) hakika utajua
kwamba Watanzania wa leo sio wa mwaka 1995
enzi za Lyatonga Mrema.
Rai yangu kwako na kwa chama chako ni kuwa
mkubali kushindana kwa hoja na sio vihoja lakini
pia pale mtakaposhindwa mkubali kuwa
mmeshindwa ili msije ingiza nchi ktk machafuko
pasipo na sababu.
LOWASSA ni Mtanzania ana haki kuwa Rais sawa
na ww kama Watanzania wataona anafaa na kumpa
kura tar 25 October 2015.
Lakini nikukumbushe tena kwamba unachokiwaza
ww sicho anachokiwaza MUNGU. Mara zingine mh
Rais uweke maneno ya akiba na ujitahidi kuwa na
Kumbukumbu.
Ni mwaka huu tu km sikosei ulitwambia
Watanzania kwamba KATIBA MPYA itapatikana na
utahakikisha kuwa unapoenda kuondoka
madarakani utatuachia katiba mpya. .!!! Je pamoja
na kuwabeza wapinzani(UKAWA) km unavyowabeza
na leo mlifanikiwa kupata hiyo Katiba mpya au
imekuwa Hadithi km ambavyo itakuwa baada ya
tar 25 October?
Mh Rais nchi hii sio mali yako km unavyotaka
kutuaminisha hata leo ifikie mahala uamini
kwamba ww ndie mwenye kuamua au mwenye
mamlaka kusema nani awe na ni nani asiwe Rais
wa Tanzania
Huko ni kujipa matumaini ambayo siku moja
unaweza kujikuta unajuta na kujilaumu kwa
yatakayoenda kutokea.Cheo ni dhamana!!
MARA ZINGINE NI BORA KUWEKA AKIBA YA
MANENO...

Mwisho
Mh. Kikwete jiandaeni kisaikolojia kukabithi nchi kwa amani chini ya Chadema na Ukawa.
"Ukitaka kuzuia mabadiliko yatakubadili"
 
Kwa kweli hata mie.nilimshangaa sana kusikia kauli zile za "adui ni adui", cha mtemakuni, lazima tutashinda, mwali n.k. kwa kiongozi na.heshima yake hakupaswa kutoa hizo.
 
"Tuna uzoefu, tumejipanga, lazima tutashinda"
Na maneno mengine yafananayo na haya.
Kiukweli napata ukakasi!
 
Huyo mwali atamficha tu na hatomtoa nje na shughuli ataiona
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema enzi za uhai wake nanukuu"Ulevi wa madaraka" ndio huu tunaoushuhudia.
 
Mnajidanganya hivi bado mnajiaminisha hilo jizi mlilo lisujudia litakuwa rais! labda rais wa arusha na si tz never
 
Tatizo la baadhi kujiona wana hati miliki ya kuongoza nchi na wengine hawafai. Maamuzi ya wananchi itabidi yaheshimiwe na yeye akapumzike msoga
 
lazima tuwavuruge oct 25, na kauli zake atazijutia
 
Pia ni ushamba na udhaif Wa hali ya juu sana, Mh. Rais kikwete kumpigia kampeni mgombea Wa kutoka chama chake, na maneno ya kejeli kiasi hicho, ni aibu sana,, nimebahatika kuliona hili kwa nchi ya Tanzania tu, nchi zingine sijaona,, Rais hatakiwi kupendelea upande wowote ule,,, huu ni ushamba tu, hii nchi ni ya watanzania wote, hakuna mwenye hati miliki..
 
NAPENDA KUMTAHADHARISHA MH RAIS KIKWETE
KUHUSU KAULI YAKE!!
Jana akimpokea mgombea kiti cha Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ndg Pombe
Magufuli, wakati akienda kuchukua fomu kutoka
tume ya taifa ya uchaguzi mh Kikwete alijitapa
kuwa wapinzani ktk uchaguzi wa mwaka huu ni
sawa na timu ya mpira na watakua wakisimama tu
huku magoli yakiingia(wakifungwa).
Haikutosha alisema kwamba MWENYE MWALI NI
YEYE na kwamba atahakikisha anamlinda. Au kwa
maneno mengine ataamua yeye kuwa nani ampe
MWALI(Kiti cha Urais)
Kwangu mm naona km Mh Kikwete kwanza
ameonyesha mshutuko mkubwa sana kwa kuwa
hakuwahi kutegemea anayoyaona na kuyasikia
sasa. Hivyo basi anachojaribu kukifanya ni
kuwatisha UKAWA(mgombea wao) kwa kutumia
madaraka yake aliyonayo
Naomba nimwambie mh Kikwete kwamba jambo la
MUNGU halijawahi kushindwa mahala popote na
kwamba anapotumia madaraka yake kuwatisha
wagombea wa vyama vingine hiyo sio demokrasia
ila pia asisahau kwamba cheo ni dhamana siku
moja anaweza kujikuta yeye ndie akaona cha
"Mtema kuni" badala ya hao anaowaambia.
Ajiulize GHDDAFI NA wanawe wako wapi leo
pamoja na kuwaita WALIBYA "Panya"?
Mtoto mkubwa wa aliekua Rais wa Libya
(marehemu sasa) yupo Gerezani na wiki iliyopita
alihukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa
kosa la kuwaamuru Majeshi kuuwa waandamanaji
waliokuwa wakipinga serikali ya Baba yake.
Inashtusha sana RAIS wa nchi kusema wapinzani
wataona cha mtemakuni na ikiwa hao wapinzani
watashinda je yeye hataona cha mtemakuni?
Mh Rais Siasa sio Uadui hata ifikie mahala utamke
maneno ya vitisho na kukebehi kwa vile tu ww ni
rais. Siku moja historia itakuhukumu kwa kauli na
dharau zako haswa ukiwa km kiongozi mkuu wa
nchi.
Tulidhani kwamba NAPE anavyoropoka ni kichwa
hakiko sawa sawa kumbe ni maagizo kutoka
kwako?
Tanzania ni mali ya kila Mtanzania na kwamba
uongozi wa nchi hauna hati miliki na chama
kimoja, mtu wa dini fulani au Wa kanda fulani.
Ikifikia huko basi tujue hatuna tena nchi isipokuwa
tusubiri vurugu.
Mh Rais nataka nikuhakikishie kwamba mwaka huu
hata km utatumia Majeshi, bunduki, vifaru na
Mabomu ili kumkabidhi MWALI kwa asiestahili kwa
kuwa tu ww ni Rais( mwenye mwali) hakika utajua
kwamba Watanzania wa leo sio wa mwaka 1995
enzi za Lyatonga Mrema.
Rai yangu kwako na kwa chama chako ni kuwa
mkubali kushindana kwa hoja na sio vihoja lakini
pia pale mtakaposhindwa mkubali kuwa
mmeshindwa ili msije ingiza nchi ktk machafuko
pasipo na sababu.
LOWASSA ni Mtanzania ana haki kuwa Rais sawa
na ww kama Watanzania wataona anafaa na kumpa
kura tar 25 October 2015.
Lakini nikukumbushe tena kwamba unachokiwaza
ww sicho anachokiwaza MUNGU. Mara zingine mh
Rais uweke maneno ya akiba na ujitahidi kuwa na
Kumbukumbu.
Ni mwaka huu tu km sikosei ulitwambia
Watanzania kwamba KATIBA MPYA itapatikana na
utahakikisha kuwa unapoenda kuondoka
madarakani utatuachia katiba mpya. .!!! Je pamoja
na kuwabeza wapinzani(UKAWA) km unavyowabeza
na leo mlifanikiwa kupata hiyo Katiba mpya au
imekuwa Hadithi km ambavyo itakuwa baada ya
tar 25 October?
Mh Rais nchi hii sio mali yako km unavyotaka
kutuaminisha hata leo ifikie mahala uamini
kwamba ww ndie mwenye kuamua au mwenye
mamlaka kusema nani awe na ni nani asiwe Rais
wa Tanzania
Huko ni kujipa matumaini ambayo siku moja
unaweza kujikuta unajuta na kujilaumu kwa
yatakayoenda kutokea.Cheo ni dhamana!!
MARA ZINGINE NI BORA KUWEKA AKIBA YA
MANENO...

Mwisho
Mh. Kikwete jiandaeni kisaikolojia kukabithi nchi kwa amani chini ya Chadema na Ukawa.
"Ukitaka kuzuia mabadiliko yatakubadili"

Umepoteza mda kuandika utumbo!!
 
Hata mimi nilistaajabu sana kumuona JK akibubujikwa povu mithili ya mtu aliyetafuna majani ya mapapai.
In short mwenyekiti wa CCM amepanic.
 
Huyu Mzee amelewa madaraka lkn akumbuke Tanzania sio mali yke, awetayari kuheshimu maamuzi ya watanzania..
 
kwa kweli ni ukosefu wa fikira kudhani kuna kundi la watu flani tu ndo wanahaki ya kuongoza nchi, hakuna mwenye dhamana na nchi mpaka uone ni wewe tu au ni ukoo wa flani au familia kadhaa tu ndo zenye haki ya kuongoza, kila mtu anayohaki ya kuomba kuongoza na ni lazma tuwaache watanzania wao ndo waamue nn wanachokitaka, kuanza kutoa lugha za jumla jumla ya kwamba huyu ndo mshindi si haki na si democrasia maana huwezi ukawa ww ndo mpiga kura wa wagombea wote kwa naiaba ya watanzania wote, tuacheni watanzania tuwasikilize wagombea na sera zao harafu wananchi wataamua nani anafaa kwa wakati huu, ingekuwa hivyo hakuna haja ya kuendelea na huu mfumi wa vyama vingi tuingie tu sasa kwenye mfumo wa kifalme tuanze kuachina vigoda.
 
Hata mimi nilistaajabu sana kumuona JK akibubujikwa povu mithili ya mtu aliyetafuna majani ya mapapai.
In short mwenyekiti wa CCM amepanic.
Mimi sikushangaa kabisa. Hii ndiyo mindset ya Kikwete. Mnakumbuka Ridhiwani aliposema rais hatoki kaskazini?
Alikuwa anawakilisha walichozunguza na baba yake.
 
Mnajidanganya hivi bado mnajiaminisha hilo jizi mlilo lisujudia litakuwa rais! labda rais wa arusha na si tz never

Mwizi mmmma maaaaa koooo, we tulia povuu unalotoa hutaweza fulia hata dekio, nenda Lumumbaaa
 
Very good, JK kapotoka...anapiga kampeni kwani tunamchagua yeye..? As well, Rais sio wa CCM tu, it is totally illegal and unfair kwa Rais yuko madarakani kupiga kampeni, kwani sio haki....

As well, maneno yake ya jana, ni dalili tosha KAOGOPA SANA na Kaona UKAWA kupitia Lowassa wanachukua nchi....!!!
 
Back
Top Bottom