Nilisoma kuhusu symbolism na numerical patterns katika Biblia na mojawapo ya texts nilizofanyia utafiti ni Ufunuo wa Yohane 13:16-18.
Lugha na misemo ya kitabu cha Ufunuo (Greek, apokalypsis; English, revelation) inafanana na ile ya kitabu Daniel. Hivyo, kuna school of thought inayosema kuwa huenda author wa vitabu hivi viwili ni mmoja.
School of thought nyingine inasema kitabu cha Ufunuo wa Yohanne kiliandikwa wakati ambao Kanisa (wanakanisa, Wakristo) lilipata mateso makubwa - persecutions na ujumbe wa kitabu hicho ilikuwa kuwatia moyo Wakristo waliokuwa wakiteswa kwa ajili ya imani yao wasikate tamaa na waamini kuwa Mungu yupo pamoja nao muda wote na kwamba yeye ndiye mwanzo na mwisho wa yote. Hivyo, mateso ya hapa duniani siyo mwisho wa yote.
Ndiyo maana katika mateso yote hayo kuna ujumbe wa matumaini Mungu atawaokoa watu wake na kuwafanya waishi naye milele katika maisha mapya na atafuta kila chozi walilo nalo. Kitabu hiki kiliandikwa mwishoni mwa utawala wa Domitian (81-97 AD).
Kulingana na lugha na ujumbe wa kitabu chenyewe, inaaminika kuwa kiliandikwa wakati wa persecutions. Kwa hiyo, lugha na misemo iliyotumika, lazima isomwe sambamba na lugha ya zamani Greek. Katika Greek number kama 1,2,3,4,6,7 na 12 au multiples zake zina maana fulani. Namba 6 ni namba ya uovu au mwovu na hivyo namba 6 tatu (666) ni alama ya mwovu hasa (kusisitiza zaidi) mwovu wa waovu evil forces.
Kwa wakati ule, ujumbe uliwahusu first addressees - wale waliokuwa wanatesa Kanisa kwa ajili ya imani yake na hasa Emperor Nero kwani kwa Greek helufi za jina hilo zinafanya 666 au mtawala yeyote ambaye alitawala kimabavu (kinyama) na kuwatesa watu na pia Wakristo wenyewe ili wasikate tamaa. Hiyo, 666 ilikuwa kama code name ya mtu mkatiri (anti-Christ) aliyekuwa anawatesa na kuwaua Wakristo (Wafuasi wa Yesu Kristo).
Kwa mazingira yetu ya leo second addresses inarefer pia kwa watu au watawala ambao hawatawali kwa haki bali wanaishia kumwaga damu za watu kama wakati wa persecutions hasa wakati wa utawala wa Nero na Domitian.
Yaani, watu ambao wanasababisa vita na umwagaji damu, wanaoua maalbino kwa sababu ya tamaa ya mali, mafisadi au watu wasio waadilifu kwa maneno na matendo yao.
Kwa kifupi, 666 ni MTU au WATU WAOVU.
NB: Epukana na wale wanaoforce meneno ya Latin VICARIUS FILI DEI (maneno yaliyoandikwa kwenye kofia ya papa) kuwa namba 666 na kusema eti inasimama badala ya Papa (Baba Mtakatifu). Sasa jiulize ni papa mmoja tu au wote (ili mradi uwe papa tayari unakuwa 666)?
Hii siyo kweli kwa sababu kuu mbili: 1. Kitabu cha Ufunuo hakikuandikwa kwa lugha ya Latin na hivyo kisingeweza kutumia literature na numerical patterns za Latin. 2. Ujumbe wake haumhusu mtu mmoja as such bali yeyote yule mwenye characteristics za uovu ingawa anaweza kuwa papa pia (kama ni mtu mwovu).
Wanaotafisiri hivyo wanajumlisha V+I+C(A wanairuka kwa vile haipo)+I (U wanaifanya V ili iwe 5 na S wanairuka)(F wanairuka)+I+L+D (E wanairuka)+I. Ukijumlisha hizo namba utakuta siyo 666 lakini wanaziforce na kusema herufi zake zinaleta 666 na kwa hivyo kwa vile hayo maneno yameandikwa kwenye kofia ya papa, wanasema namba 666 ni yeye.
Inawezekana wanaoitumia kwenye bidhaa wanakusudi fulani. Lakini, ilivyotumiwa kwenye Biblia ni kama nilivyoeleza hapo na hata wewe ukisoma Kitabu cha Ufunuo na kukielewa utaona ujumbe wake ni huo wa kuwapa matumaini wanaoteseka kwa kuonewa, kunyanyaswa, kubaguliwa au kuuawa. Last edited by Magobe T; 1st December 2008 at 08:38 PM.