Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi mwenye usikivu mkubwa kwa wakulima wa korosho, akisisitiza kuwa pembejeo za bure alizotoa kupitia serikali yake ni uthibitisho wa dhamira ya kweli ya kuwawezesha wakulima nchini.
Akizungumza Aprili 12, 2025 wilayani Nachingwea mkoani Lindi, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika ziara ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla, Nape amesema kuwa serikali iliyoongozwa na Rais Samia imeleta mageuzi makubwa katika sekta ya korosho kwa kutoa pembejeo bure tangu mwaka 2021.
“Wakati ule tulizozana bungeni mpaka wanajeshi wakaja hapa kukusanya korosho. Baadaye tukajadili, serikali ikatuelewa, tena aliyetuelewa sana ni Rais Samia. Akaamua wakulima wasitoe hela mfukoni, akaleta bilioni 58.4 na tukagawa pembejeo za bure kwa wakulima,” amesema Nape.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mbunge huyo ameongeza kuwa hata baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani waliokuwa wakipinga mfumo wa korosho na kushutumu serikali, walijitokeza kuchukua pembejeo hizo, akisema: “Wakawa wanapanga foleni kuchukua pembejeo ya Samia, kweli au si kweli? Hawaulizwi kadi ya chama. Mama hana ubaguzi.”
Akitetea juhudi za Rais Samia, Nape amesema viongozi wa upinzani hawapaswi kubeza mafanikio yanayoonekana kwani wao na wafuasi wao pia wananufaika na huduma za afya, elimu na kilimo zinazotolewa na serikali ya CCM.