Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Nape Nnauye ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuwa ukipata nafasi ya kufanya kazi vijijini ndiyo unaweza kuona utofauti mkubwa uliopo.
"Ukikaa na kufanya kazi huku vijijini, utaona utofauti mkubwa uliopo kati ya Dar es salaam na Tanzania, wapiga kelele wengi hawajui maisha haya", alisema Nape Nnauye.
Mbunge huyo ambaye sasa yupo kwenye ziara mbalimbali ndani ya jimbo lake amekuwa akikutana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi wake ambao wengi wao ni watu wa maisha ya kawaida.
Nape alipokutana na wakulima waliweza kuishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuweza kuwapelekea mbolea ya Sulpha ya bure kwa ajili ya mikorosho yao lakini alidai kuwa wakulima hao walilalamika kwa mbolea hiyo kutokuja kwa wakati na kwa kiasi cha kutosha.