KWA KUONGEZEA.
Nawashauri wana ccm hasa Nape, Ritz, na Chama wa gongo la mboto wajikumbushe kufanya hesabu za takwimu (statistic) za kidato cha tatu kwa kuchora graph (group bars au line graph) ya matokeo ya kata 29 ambazo zimefanya uchaguzi wa udiwani kwa kuoanisha matokeo ya mwaka 2010 na haya ya 2012 (miaka miwili baadae).
Mstari ulalo (x-axis) waweke majina ya kata na mstari wima (y-axis) wachague skeli itakayo kidhi idadi ya kura kwa miaka husika, baada ya kuchora waeleze taswira ya michoro kwenye graphs zao kwa mahasimu wawili (chadema na ccm). Halafu wawe wakweli wa dhamira kwa kueleza ukweli usio tawaliwa na akili za ki-ccm.
Majibu ya taswira ndio yatawaeleza ukweli kuhusu chama chao kama kinazidi kuporomoka au kinapanda? Na kama kinaporomoka ni chama gani kinapanda siku hadi siku?
HII HAIHITAJI KUWA na PHD (Pure head damage) KAMA BALALI au waziri ambae hatuwezi kumpata akijiZURU. 😀