Nape Umeonyesha Upendo Mkubwa leo

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
Wadau

Leo mida ya mchana Mh. Nape Nnauye alipita maeneo ya soko kuu Arusha karibu na kijiwe cha kahawa maarufu kwa makada wa CHADEMA.

Kilichonifurahisha akiwa ndani ya gari lake makada hao wa CHADEMA bila uoga walimfuata kumsalimia na kisha kumuomba Kada huyo wa CCM angalau awapatie hela kidogo kwa ajili kahawa na kashata.

Bila kusita wala kujali itikadi tena kwa moyo wa ubinadamu na kuzingatia hali zao Mh.Nape aliwapatia vijana hao hela kidogo kisha kuendelea na safari yake. Naamini Mh. Nape alikuwa kwenye majukumu mazito ya kichama lakini aliona ni vema tena kwa busara kubwa atumie muda huo mfupi angalao kuwasikiliza na kuwasaidia makada hao wa CHADEMA.

Ukweli jambo hili ulilolifanya limenifurahisha sana kwani limeonyesha kuwa kwa CCM siasa sio Uadui bali Maendeleo. Kwa siku ya leo kumekuwa na utulivu eneo hilo na upendo umetawala.

Hongera sana Kada wa Chama cha Mapinduzi na Mbunge wa Mtama.

Karibuni.
 
Makarai yamechacha. Vyuma vimekaza.
 
Dont be cheap to that extend!....fanya analysis ya mambo mabaya ambayo kawafanyia upizan kwa kipindi chote kwanza..... usiwe kama mwanamke ambaye hata akimfumaia mmewe kwenye kitanda chake akishikwa kiuno kidogo na mmewe husema nimekusamehe!
 
Hata angekuwa mm ningefanya kama alivyofanya Nape ili safari yangu iwe ya heri. Hata mm nikikuta mateja kwenye kijiwe chao wakiniomba hela kidogo lazima niwape ili kuepusha Shari ya Kuvunjiwa vioo vya gari
 
Sijaona cha maana,kama anaubavu akemee wanaccm wenzake wanaohubiri chuki na kuadvocate chuki na mauaji.
 
Kwa hiyo mtu kutoa hela ya kashata ww ndo umeona jambo kubwa mpaka uje kuanzisha uzi humu?
 
Hii nayo ni issue?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…