Nape tupia jicho vipindi vya redio na luninga

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,700
1,721
Kwanza nakupa hongera.

Nakusihi utupie jicho majina ya vipindi katika 'radio' na 'television' zetu.

Mie huhuzunika mno kusikia/ kusoma jina la kipindi kwa lugha ya Kiingereza lakini kwenye kipindi hicho hakuna kuzungumza lugha hiyo ila ni 'full' Kiswahili.

Mfano mzuri ni DW na BBC, hawa vipindi vyao vinasomeka kwa lugha husika.
 
Kama majina ya Radio ni ya kiingereza kwa nini vipindi visiwe na majina ya kiingereza?.... Sidhani kama kipindi kuwa na majina ya kiingereza ni tatizo, tatizo ni Maudhui yaliyopo kwenye vipindi hivyo.... Asilimia kubwa ya vipindi vyetu vya Radio na Tv ni kufanana.
 
Mkuu hayo ndo mapungufu ya wizara hii. Yampasa waziri awe na ujasiri wa kuisimamia lugha ya Taifa.
 
Kuna Morning Talks
Kuna Morning Mirror
Kuna Morning Suggestion
Kuna Sunrise Power
HIVYO VYOTE NI VIPINDI ASUBUHI KATIKA RADIO MBALI MBALI...
Pana redio moja inajiita ya Afrika yenyewe saa kumi na moja alfajiri wanakipindi kiitwacho 'good morning Africa' wakati usikivu wake hapa hapa nchini ni wa kubahatisha.
 
Mheshimiwa mzee wa Mtama hebu mulika darubini ktk hii miziki ya kizazi kipya yani ktk runinga ni kero kwa baadhi ya watazamaji.Mfano wakianza na miziki ya milavu lavi ya ni kila kituo utakuta ni nyimbo hizo hizo hakuna hata ujumbe wa maendeleo.Utakuta baby ninakupenda mara honey ninakumisi yani ni masaa yote nyimbo ni hizo hizo.
 
Back
Top Bottom