Nape soma madudu ya chama chako ukawaeleze wenzio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape soma madudu ya chama chako ukawaeleze wenzio

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ebaeban, Apr 20, 2012.

 1. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  NAPE SOMA MADUDU YA CHAMA CHAKO UKAWAELEZE WENZIO>  CCM na anguko lao wamejitakia wenyewe,( mlimbua inchi ni mwanainchi wenyewe) kusimamia uweledi ni jukumu lao viongozi. Kuna kamati kuu, haslimashauri kuu, mkutano mkuu mwisho wanachama. Nyakati Fulani mwanachma wa kawaida husaidiwa kujitambua na hasa kufikia maamuzi sahihi. Enzi za mwalimu chombo kama kamati kuu kilikuwa na uwezo wa kuwashauri wanachama wao kwamba chaguo lao kwenye kura ya mapendekezo siyo sahihi hivyo jina halitarudi. Msamiati wa kama jina halitarudi jimbo litapotelea kwa wapinzani enzi hizo ilikuwa ni potelea mbali jimbo wacha lipotee heshima yachama ibaki, heri lawama uliko fedheha oneni sasa CCM Arusha watabaki na Mery Chatanda tu wanachama wote watawakimbia


  Sasa kuna faida gani mtu kama Rostram Aziz, Aden Rage, Mohammed Dewji, Murji, Shabib, Abood, na wengine kama hao wabaki kwenye chama halafu wanachama wengine wote wahamie kwenye vyama vya upinzani.


  Ni nani hajui kwamba wote hao enzi za mwalimu majina yao yalikuwa hayarudi walikuwa wanakatwa juu kwa juu? Wao kuwa CCM ni mavuno , thread ilipita jana eti nani anajitolea kama mbunge huyu (Mohamed Dewji) eti ametolea jimbo lake Billion 6. Mimi nawasaidia watu wenye kuamini amelitolea jimbo kwamba hawapo sahihi kwa sababu tuhuma zinazomkabili Waziri Mustafa Mkullo ni pamoja na kumwuzia huyo ambae pia anajulikana kama Mohammed Enterprise viwanja kwa bei ya kutupa, sasa swali ardhi na pesa kipi chenye samani? Wewe upate pesa hizo billion 6 yeye achukue ardhi naomba mnipe jibu, wenzetu walisema _ There is no free lunch under the sun. Mtu kama Murji alianza kuwahonga wanainchi wa Mtwara mjini miaka miwili kabla ya uchaguzi, mala basi kwenye mazishi, mala kahawa ya bure kwenye vijiwe vya kahawa, mala sadaka na rambirambi kwa wafiwa, kuja kura za maoni wamakonde walikuwa wanafukuzwa kama mbwa.


  CCM BADO MNA NAFASI YA KUJISAHIHISHA. REJEENI ENZI ZA MALIMU
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Blayi, siamini hata kama wanaelewa kosa lao (I mean ccm) na wanaoelewa wanapuuzwa. Sioni kiongozi ndani ya ccm anaeweza kusimamia uadilifu sasa hivi halafu akapewa nafasi. Lazima atachafuliwa tu na kuundiwa mizengwe lukuki.
   
Loading...