Uchaguzi 2020 Mkutano Mkuu wa CCM 2020 wamchagua John Magufuli kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amteua Samia Suluhu kuwa Mgombea Mwenza

Roving Journalist

JF-Expert Member
Apr 18, 2017
532
1,000
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Jumamosi, Julai 11, 2020 jijini Dodoma, Wajumbe 1,846 wanatarajiwa kushiriki. Mkutano huo unongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

AJENDA:
1. Kufungua Mkutano

2. Marekebisho ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977, Toleo la 2017

3. Taarifa za Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 za SMZ, SMT na CCM

4. Uteuzi wa Mgombea wa CCM wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

5. Kufunga Mkutano.

Magufuli.jpg

UPDATES

Mkutano Mkuu wa CCM unafanyika leo tarehe 11 Julai 2020 ukiwa na lengo kuu la kumpitisha mgombea wa Urais wa JMT.

Mkutano umehudhuriwa na wanachama 1,822 huku wanachama waliokosekana wakiwa 23 sawa na 1% hivyo uko sahihi kikatiba na ajenda zinaweza kujadiliwa.

Katika hotuba yake, Rais Magufuli kama mwenyekiti wa mkutano huo, amewashukuru viongozi wa upinzani waliohudhuria katika mkutano huo

Amemshukuru Lyatonga Mrema, mwenyekiti wa TLP kwa kauli yake ya kusema TLP haina mgombea bali itamuunga mkono mgombea wa CCM

Rais Magufuli:

Mambo yaliyofanyika ni mengi, kila mmoja ni shahidi, hata Viongozi wa Vyama vya upinzani wanafahamu mazuri yaliyofanyika hata Nchi jirani wanafahamu, Ndege 11 kununuliwa kwa mpigo tena kwa cash, Elimu bure,Barabara,vituo vya Afya nyinyi wote ni mashahidi

Tumeipeleka Nchi kwenye uchumi wa kati, tumepambana vizuri na corona na mengine mengi, tumeitengeneza Tanzania, ni mafanikio yetu wote hata ambao hawako CCM na ndio maana Mzeee Mrema mapema kabisa akasema yeye hana mgombea Urais, mgombea wake CCM maendeleo hayana chama.

Nimefurahi kuwaona Marais Wastaafu, nimefurahi kumuona Mama Anna Abdallah huyu Mama alinifundisha Kazi lakini pia alimfundisha kazi Mwinyi akiwa Naibu Waziri wa Afya, nimefurahi kumuona Mzee Kinana, Lowassa, Mzee Sumaye, Maspika Wastaafu na wote.

Nimefurahi kumuona Mzee Mwinyi Mzee wa ruhusa, nimefurahi kumuona Mzee Mkapa Mzee wa uwazi ingawa sijajua ni uwazi upi?, nimefurahi kumuona Mzee Kikwete naona mvi zimeanza uzee unamuwinda, hii ndio Tanzania, nimefurahi kumuona Dr.Bashiru, Mzee Mangula n.k


Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Mhe. Augustino Mrema:

May 04, 2019 sisi TLP tulikaa tukajadili nani atuongoze, H/Kuu TLP ikasema hatuna mbadala wa Magufuli tukasema Magufuli anatosha, tukakutana tena May 08,2020 kura zote zikamuangukia Magufuli

TLP tumesema wewe Magufuli unatosha, tutafanya kampeni Nchi nzima kuhahakisha unachaguliwa tena, ombi langu kwenu CCM tujipange kuhakikisha kwenye Kata na Majimbo yote kuna mgombea wa TLP na CCM, tusing’ang’anie jimbo moja Watu wa CCM 30 ni matumizi mabaya ya rasilimali Watu

Baada ya May 08,2020 Halmashauri Kuu TLP kusema Magufuli anatosha kuwa mgombea wetu, May 09,2020 tukamuita Polepole aje, tukamualika na Msajili aje ashuhudie kuwa kikao cha TLP hakikuwa cha Magumashi na hapo tukapiga kura kisha wote wakasema tena wanamtaka rais Magufuli


Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF

Amesema chama chao katika uchaguzi wa 2020 kinakuja na agenda ya “Furaha kwa Watanzania inawezekana”

Pia Professa Lipumba amewaomba CCM kuwa na siasa za ustaarabu kitapoanza kipindi cha kampeni akisisitiza kupambana kwa hoja


Mzee Kinana

Amewaomba Wajumbe mkutano mkuu wampe mgombea kura zote bila kuharibika bila hapana ili apate nguvu kuliongoza taifa letu.

Amewasihi Wanaccm kufanya kazi kwa bidii kwa kujitolea kutafuta kura za Rais, Wabunge na madiwani. Hakuna uchaguzi rahisi.

Kuna Watia nia na ubunge wengi sana, kuna jimbo la Rorya watia nia wako 60, nawaomba hatimaye watamteua mgombea mmoja wa CCM hivyo wasigawane kura.


Mzee Mwinyi

Nawaomba wenzangu tumekutana hapa na wanatanzania nzima pamoja na wapinzani. Sote tumeshuhudia kuwa mgombea Rais wetu tuliye naye ameshika madaraka kasoro miaka mitatu kama mambo mengi, ya ajabu kama kununua ndege 11. Sijawahi kuona nchi inayosemwa haina pesa inanunua ndege 11 kwa pesa za ndani. Hakika Rais Magufuli amefanya mambo ya ajabu katika sekta zote ikiwemo Umeme na SGR.

Tumekaa miaka mingi na uwezekano wa kupata umeme lakini Rais wetu kalishugulikia suala la umeme kwa kujenga Stiegler's Gorge na karibu tunakuwa mabepari wa umeme.

Nchi yetu inaendeshwa kwa Katiba lazima tuienzi, , tusiingilie lakini tunaweza kuiahirisha kwa muda mfupi ili kumpa Rais wetu kipindi kingine kimoja cha asante. Hichi ni asante na kisha tuendelee vile vile mpaka dunia iishe. Hiki ni maalum kwasababu ana mengi nchi itayakosa.

Rais Magufuli akimjibu Mwinyi kuhusu kuongezewa kipindi kingine

Mbona wewe (Mzee Mwinyi) hukuongeza muda baada ya kumaliza? Au mzee Mkapa hakuongeza? au Mzee Kikwete hakuongeza? Ila nimekuelewa Mzee Mwinyi wewe ni mtani wangu.


Agenda: Uteuzi wa Mgombea Urais kupitia CCM

Rais Magufuli amejivua Uenyekiti ili aweze kupigiwa kura, Uenyekiti umekaimishwa kwa Mzee Sheini.


RAIS MAGUFULI APITISHWA KUWA MGOMBEA WA CCM KWA 100% YA KURA ZA WAJUMBE

Msimamizi wa Uchaguzi, Spika Ndugai anasoma...

Wajumbe walohudhuria ni 1822

Kura zilizopigwa ni 1822

Hakuna kura iliyoharibika kura halali ni 1822. Kura za ndiyo ni kura 1822 sawa na asilimia 100.

Rais John Pombe Magufuli ameteuliwa na CCM kuwa mgombea wa Urais kwa mwaka wa uchaguzi 2020

Kwa kura 1822 zilizopigwa na wajumbe wa kamati kuu, Rais Magufuli amepata kura 1822 ya kura za ndio

Awali katibu mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally alisema, ilibidi wawe na wagombea watatu lakini hakukuwa na mgombea aliyejitokeza kuchukua fomu ya kugombea urais

Hali hiyo ilimfanya Rais Magufuli awe mtu pekee aliyechukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM


Hussein Mwinyi

Nimefanya kazi na Marais watatu ambao ni Mkapa, Kikwete na Magufuli. Ninawashukuru wote kwa kunielekeza lakini kuna Rais ambaye Mstaafu ambaye sijafanya kazi nae ila ndio Mzazi wangu Mzee Mwinyi, amenilea, kama nina tabia njema basi ni malezi yake, namshukuru Mama yangu Mama Sitti tuko nae hapa, mchakato wa Urais umefanya nipungue uzito ila Mama yangu amepungua zaidi.

Namshukuru Mzee Mkapa nikiwa Kijana wa miaka 33 (Mbunge wa Mkuranga) aliniteua kuwa Naibu Waziri Afya,Mzee Mkapa ulinifungulia njia, namshukuru Mstaafu Kikwete katika utawala wake wa miaka 10 yote nilikuwa Waziri, namshukuru JPM pia kwa kuniamini na kunipa Uwaziri.

Katika miaka mitano ya kufanya kazi na wewe, nimejifunza mengi kwako Rais Magufuli . Wapo waliosema mimi ni mpole lakini nimejifunza kuna mambo yanataka uwe mkali, mfano rushwa, uzembe na ubadhirifu, nikichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar nitakuja na style ya Rais Magufuli katika maeneo hayo.


Hotuba ya Dkt. Magufuli (Kwa ufupi)

Namuomba Mwenyenzi Mungu anisaidie kura nilizozipata leo zisinipe kiburi, zisinifanye nijione mimi nafaa sana, bali zikanifanye nikawahudumie Watanzania wote bila kubagua dini zao, makabila na vyama vyao. Ninafahamu kazi hii inahitaji msaada wa Mungu. Kura nilizopata leo zikawe salamu kwa wasaidizi wangu kuwa wana kazi ya kutimiza shauku ya wanachama na wananchi wote, hivyo tukashirikiane kuijenga nchi yetu hii tajiri

Niwaombe Watanzania mkazidi kuniombea ili nikafanye yale mnayoyataka. Wajumbe mmenipa kura kwa 100%, lakini kamwe msitoke hapa mkiamini kuwa tunakwenda kushinda kwa 100%.

Mara nyingi sisi CCM tunapoteza majimbo kwa sababu ya mfarakano ndani yetu. Anapitishwa mtu ambaye hamumtaki halafu mwisho mnashindwa. Wagombea Zanzibar wameonesha mfano mzuri wapo 31 ameshinda mmoja wengine wamekubali, wanamuunga mkono na nina uhakika watazunguka kwenye kampeni kuhakikisha Mwinyi anashinda

Hussein Mwinyi ni tofauti sana na watoto wa wakubwa. Mwinyi [Dkt. Hussein] hakuubeba Urais wa baba yake [Rais Ali Hassan Mwinyi]. Hussein Mwinyi amezaliwa mwaka 1966, mimi nimezaliwa mwaka 1955, mumchague yeye. Msinichagulie mtu ambaye kila siku nitakuwa nasema shikamoo, shikamoo. Mimi ni Rais wa Tanzania, nikija kule (Zanzibar) nianze kusema Shikamoo muheshimiwa Rais, inakera

Nilimteua kuwa Waziri wa Ulinzi. Waziri ambaye unamkabidhi majeshi yote ni lazima uwe unamuamini sana. Nitamshangaa mtu atakayesema Mwinyi hatoshi. Amesimamia mabomu yote na mizinga ashindwe kutawala Zanzibar?

Wanasema tumechagua Masultan. Mwinyi ndio amegombea kwa mara ya kwanza, sasa kati ya yeye na wale wengine kila mwaka ni wao tu nani Sultani? Hussein ni mnyenyekevu, hajaubeba Urais wa Baba yake na mmeona wakati anashukuru hapa hajaanza kumshukuru Baba yake, kamshukuru Mkapa, Kikwete kisha kanishukuru mimi ndio akamaliza na Baba yake.

Nilipomteua Mama Samia kuwa Makamu wa Rais mwaka 2015 sikuujua utendaji kazi wake vizuri lakini ni mchapakazi, anajituma pia ni mzuri, Wasukuma tunapenda weupe, ukiwa na Msaidizi mweupe hata ukiwa na stress zinaisha, nimeamua awe tena Mgombea mwenza wangu

Katika kipindi nilichofanya kazi na Samia nimejifunza mambo mengi sana na kupitia yeye nawahikikishia nitakuwa mtetezi mzuri wa wanawake. Nimekuwa nikimtuma popote hakatai kama na nyie kina Mama mkitumwa hamkatai.

Kwenye uongozi hakuna Urafiki unatanguliza maslahi mapana ya Taifa, Kikwete aliwatwanga Rafiki zake akaniteua, Mkapa aliwatwanga Rafiki zake akamteua Kikwete, Mwinyi na Nyerere hivyo hivyo, Wastaafu wakiona nimefukuza Rafiki zangu kwenye kazi ni kwasababu nimejifunza kwao

Niseme wazi hapa japo sikutakiwa kusema, lakini ukweli ni kwamba mwaka 2015 nilikuwa nimependekeza Hussein Mwinyi na Mama Samia mmoja wao awe Mgombea mwenza, Mama Samia akapita. Mwinyi namwamini sana.

Nitoe wito kwa Vyama vya siasa tusiwe na Wagombea haohao, tubadilishe Sample, sio kila siku Watu walewale, Mungu hajakuumba wewe tu kwamba uwe Kiongozi kila siku, tuwaachie wengine, Mzee Kikwete angeweza kuendelea kuwa Mwenyekiti ila aliniachia na waliotangulia hivyo hivyo,

Oktoba.jpg
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
31,087
2,000
56985613-C82D-43F7-B5C1-6031106F2378.jpg

Hali ya Ukumbi ni Shwari ndani ya ukumbi. Leo kupitia mkutano huu CCM itapitisha(kwa kupiga kura) jina la Mgombea Urais wa JMT.

Pia itapitisha maamuzi mbalimbali yaliyofanywa na ogani mbalimbali za Chama ngazi ya chini. Pia utapitisha Ilani ya CCM.

Mkutano huu utapokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa miaka 5 iliyopita.
Wajumbe tarajiwa ni 1846 kutoka pande zote za Tanzania.
Akidi ya mkutano imetimia kwani zaidi ya wajumbe 1823 wamehudhuria

KARIBUNI DODOMA #KAZI IENDELEE
 

mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,022
2,000
Waambieni hao watangazaji wa tbc hatujaweka hiyo stn kuwasikiliza wao, wakae pembeni tuone na kusikia live sio kuwasikiliza wao. Ujumbe wafikishien
 

G4rpolitics

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
3,760
2,000
Mtu mmoja anapigiwaje kura? fomu ilikuwa ni moja,huo si ni uharibifu wa hela za Chama. wangekiwa na ujasiri wa kufanya kama Sumaye alivyo fanyiwa upande ule sawa, ila sasa hakuna wa kuthubutu!
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,909
2,000
Mngemruhusu na Membe naye achukue fomu ya kupitishwa kugombea huo Urais ndani ya chama chenu halafu matokeo ya kura nayo yangehesabiwa kwa uwazi kama yale ya Urais wa Zanzibar ningewasifu sana!

Nina imani ile jana, Mwenyekiti naye angejigeuza kuwa Jecha wa pili kwa aina ya matokeo ambayo angeyapata kutoka kwa wale Wajumbe waliokuwa wakimshangilia kinafiki.
 

Ngwanashigi Gagaga

Senior Member
Mar 10, 2017
122
225
Ripoti ya utekelezaji iwekwe wazi
Mbona iko wazi siku zote ,kuanzia mimi na wewe tulipo! Katika nyanja zote yaani Huduma za kijamii (Afya, Elimu, maji, umeme, watumishi tumelipwa madeni yetu nk), Miundombinu (barabara, reli, majengo, madaraja, mabwawa), Demokrasia uliona uchaguzi wa mgombea Urais Zanzibar wazi kabisa, Uchumi hata Benki ya Dunia imekubali, uwazi gani zaidi ya huo?!
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
31,087
2,000
Mngemruhusu na Membe naye achukue fomu ya kupitishwa kugombea huo Urais ndani ya chama chenu halafu matokeo ya kura nayo yangehesabiwa kwa uwazi kama yale ya Urais wa Zanzibar ningewasifu sana!

Nina imani ile jana, Mwenyekiti naye angejigeuza kuwa Jecha wa pili kwa aina ya matokeo ambayo angeyapata kutoka kwa wale Wajumbe waliokuwa wakimshangilia kinafiki.
Mwaka 2015 aligombea pia ila Babalao ndio akawa mshindi
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,976
2,000
View attachment 1503520
Hali ya Ukumbi ni Shwari ndani ya ukumbi.
Leo kupitia mkutano huu CCM itapitisha(kwa kupiga kura) jina la Mgombea Urais wa JMT.
Pia itapitisha maamuzi mbalimbali yaliyofanywa na ogani mbalimbali za Chama ngazi ya chini.
Pia utapitisha Ilani ya CCM.
Mkutano huu utapokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa miaka 5 iliyopita.
Wajumbe tarajiwa ni 1886 kutoka pande zote za Tanzania.

KARIBUNI DODOMA #KAZI IENDELEE
Kuteua au kupitisha,unapiga kura na kuandika jina lako,uchague mtu au kivuli jibu ni moja tu ndio.Ukisema sio lzm ushughulikiwe
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,909
2,000
Mwaka 2015 aligombea pia ila Babalao ndio akawa mshindi
Alikuwa mshindi, au alisukumizwa tu ndani kwa bahati mbaya baada ya JK kumgeuka swahiba wake wa siku nyingi ili apite mteule wake Membe!!

Na hivyo busara ya bora tukose wote ikatumika kimakosa kwa kumpa mamlaka mtu ambaye hakuwa sahihi na pia ambaye hakujiandaa kwa majukumu makubwa kabisa katika nchi!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom