figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Heshima Kwenu wakuu,
Leo nmeamua kuwaletea update kutoka kwenye mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Michezo wa awamu ya tano Nape Nnauye.
Karibuni.
=======
UPDATES;
=======
13:08hrs: Nipo hapa Protea hotel, Mheshimiwa Nape bado hajafika. Ntamsubiri hapa hapa.
Ametokea mtu anayeitwa Iddi Suleiman ambae ni meneja wa Protea na kudai mkutano hautakuwepo na waandishi walipombana nani kazuia, alisema akaulizwe RPC wa Kinondoni.
1415hrs: Nape amekuja lakini akazuiliwa na Askari(Wanausalama(?) ili asifike sehemu ya tukio, akaamua kushuka ili aje kwa mguu, wakaanza kumvuta kumrudisha kwenye gari. Walikua maasikari kama wanne. Ilikuwa sio mbali kutoka Sehemu waandishi wa habari walipokuwa, Sema walikuwa kwa ndani.
Aliyewajulisha Wandishi wa habari kwamba Nape kazuiliwa nje ni dereva wa Nape aliyeanza kupiga honi ya gari kwa nguvu kitu kilichowastua waandishi wa habari na kuwafanya watoke nje. Walipotoka nje wakakuta nape anavutwa aingie ndani ya gari ila Waandishi walipofika Askari wakapunguza kasi
1428hrs: Nape anaongea na waandishi wa habari nje ya Hoteli akiwa juu ya gari.
Nape: Wapuuzi, nimekuja hapa wananitolea bastola eti rudi kwenye gari, nimepigana kuiweka CCM madarakani anakuja mpuuzi eti usishuke kwenye gari, mimi nape sina kinyongo na uamzi wa rais wangu, kama sikumshawishikunichagua hivyo hata kuniacha ni sawa.
Nimejitahidikutimiza wajibu wangu, tusihangaike na Nape tuhangaike na Tanzania inapokwenda nimekuwa mzalendo na muungwana, nimekuwa ninatimiza wajibu wangu
Mimi ndo nimekuwa mzalendo kwa CCM, ambayo niliikuta ikiingia kwenye shimo inakwenda, nitasemakweli daima na fitina kwangu mwiko, na nilichokisiamamia juzi ni kusema kweli, kinachotukutanisha sio magwanda ya kijani, ni imani, nimefundisha na mzee Nnauye kusema kweli na kusimamia ninachokiamini, kamaninachokiamini kitaleta matatizo mimi nlishawahikufukuzwa CCM
Usipopita kwenye matatizoya kisiasa hutakomaa, Ili mbegu iote shuti ioze, nimepanda mbegu ya kupigania haki hakika itaota, Tanzania ni yetu nchini yetu. Vijana hamna la kuogopa simamieni mnachokiamini Mwalimu, Kawawa waliondoka na sisi tutaondoka.
Sisi pia tutaondoka suala la kujiuliza tutaawaachia watoto wetu nchi ya aina gani, hilo ndio kubwa,uamuzi ni wa kwetu wenyewe
Lengo la kuja hapa ni kumshukuru Rais kwa alichokifanya, namshukuru kwa kuniamini kwa mwaka mmoja, nampongeza Mwakyembe naye ni mwanahabari.
Nimefurahi kufanya kazi na nyie, muungeni mkono Mwakyembe na Rais Magufuli ndiye rais tuliyenaye na kudumisha umoja na mshikamano.
Tumefanya kazi pamoja na nimefurahi sana kufanya kazi na nyie
Tudumishe amani na upendo wa nchi yetu, Nape ni mdogo kuliko nchi, wakati wa aliyeniteua ameniondoa mimi nitaendelea kuwatumikia.
Niliomba kazi ya Ubunge na sio uwaziri, sasa narudi kuwatumikia wananchi wangu wa Mtama
Polisi wamezuia gari ya Nape isiondoke, ameshuka kwenye gari anamsikiliza kamanda wa polisi Kinondoni
Nape anawataka waandishi wa habari waondoke, anadai hakuna la kuwaambia tena
View attachment 485512