GE2025 Nape: Samia ndiye mgombea original, wengine wasindikizaji

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,397
Reaction score
14,505
Mgombe Ubunge wa jimbo la Mtama kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Moses Nnauye amewasisitiza wananchi wa jimbo la Kilwa Kaskazini kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kumchagua mgombea Urais wa chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan sambamba na Mbunge na Madiwani wake kutokana na kile alichoeleza kuwa mgombea huyo ndio 'Original' na kwamba wengine ni 'photocopy'

Ameeleza hayo Septemba 10.2025. Alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo hilo kama mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo hilo Kinjeketile Ngombale Mwiru, ambapo pia amesema, ambapo amesema Dkt. Samia katika kipindi chake kama Makamu wa Rais na baadaye kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametekeleza majukumu yake kikamilifu

"Sisi Chama cha Mapinduzi, tumemsimamisha Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuna vyama vingine vimesimamisha wagombea wao, mimi sina maneno nao kwa sababu wote wasindikizaji, yupo mmoja mwenye shughuli yake anaitwa Samia, na mtu mwenye akili timamu hawezi kuhangaika na photocopy wakati original ipo" -Nape

‎Ameongeza kuwa mataifa mengi hujikuta katika hali ya machafuko baada kujitokeza kwa mazingira kama yaliyotokea Tanzania mwaka 2021 (ya kufariki Rais aliyekuwa madarakani), lakini hapa Tanzania aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo Dkt. Samia Suluhu Hassan aliapishwa kuwa Rais na amenyesha utayari wa kuiongoza Tanzania licha ya kwamba awali hakujiandaa kushika nafasi hiyo

Aidha, Nape amesisitiza kuwa miradi yote ya maendeleo aliyoipokea Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa mtangulizi wake (Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) imeendelea kiukamilifu zaidi ya ilivyokuwa awali

"Wakina mama wanaweza, na kama tulimjaribu miaka minne (4) hatuna sababu ya kumnyima miaka mingine mitano (5), amethibitisha anaweza" -Nape

‎Ameongeza kuwa licha ya msigano uliokuwepo kwenye siasa hapa nchini lakini Dkt. Samia Suluhu Hassan aliruhusu uhuru kwa wanasiana na mikutano ya hadhara kuendelea licha ya kushambuliwa kwa maneno

‎Aidha, ili kuchagiza maendeleo amesema kiongozi huyo alisisitiza ulipaji kodi wa haki hali iliyopelekea miradi ya maendeleo kukamilika.

Shina waliokata na kulitupa porini limechipua ila vichwani mwao wanadhani limekauka... Ukombozi wa fikra unasambaa Kwa Kasi ya kimbunga katika Kila ufahamu wa mtu timamu.
 
Mjuba Nape hata sisi tunajua hao vikaragosi wenu ni wasindikizaji tu, hakuna upinzani wa kweli pale, wanazuga tu!. Ila mmewapa magari makali na ulinzi wa kufa mtu ili waweze kufanya kampeni za kuhadaa umma kuwa nao wanagombea kumbe ni geresha tu!
 
Ahsante nape umemaliza.samia alikuwa kwenye majaribio na ameonekana anapwaya na hana upinzani kwamana uliokuwepo ni photocopy ya ccm.
 
Huu ni ukweli samia hata kwa mpina hachomoi pamoja tume mbovu achilia mbali lisu
 
Mgombe Ubunge wa jimbo la Mtama kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Moses Nnauye amewasisitiza wananchi wa jimbo la Kilwa Kaskazini kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kumchagua mgombea Urais wa chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan sambamba na Mbunge na Madiwani wake kutokana na kile alichoeleza kuwa mgombea huyo ndio 'Original' na kwamba wengine ni 'photocopy'

Ameeleza hayo Septemba 10.2025. Alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo hilo kama mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo hilo Kinjeketile Ngombale Mwiru, ambapo pia amesema, ambapo amesema Dkt. Samia katika kipindi chake kama Makamu wa Rais na baadaye kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametekeleza majukumu yake kikamilifu

"Sisi Chama cha Mapinduzi, tumemsimamisha Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuna vyama vingine vimesimamisha wagombea wao, mimi sina maneno nao kwa sababu wote wasindikizaji, yupo mmoja mwenye shughuli yake anaitwa Samia, na mtu mwenye akili timamu hawezi kuhangaika na photocopy wakati original ipo" -Nape

‎Ameongeza kuwa mataifa mengi hujikuta katika hali ya machafuko baada kujitokeza kwa mazingira kama yaliyotokea Tanzania mwaka 2021 (ya kufariki Rais aliyekuwa madarakani), lakini hapa Tanzania aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo Dkt. Samia Suluhu Hassan aliapishwa kuwa Rais na amenyesha utayari wa kuiongoza Tanzania licha ya kwamba awali hakujiandaa kushika nafasi hiyo

Aidha, Nape amesisitiza kuwa miradi yote ya maendeleo aliyoipokea Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa mtangulizi wake (Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) imeendelea kiukamilifu zaidi ya ilivyokuwa awali

"Wakina mama wanaweza, na kama tulimjaribu miaka minne (4) hatuna sababu ya kumnyima miaka mingine mitano (5), amethibitisha anaweza" -Nape

‎Ameongeza kuwa licha ya msigano uliokuwepo kwenye siasa hapa nchini lakini Dkt. Samia Suluhu Hassan aliruhusu uhuru kwa wanasiana na mikutano ya hadhara kuendelea licha ya kushambuliwa kwa maneno

‎Aidha, ili kuchagiza maendeleo amesema kiongozi huyo alisisitiza ulipaji kodi wa haki hali iliyopelekea miradi ya maendeleo kukamilika.

Huyo si mnufaika kama wale wa Nepali tu? Au?

Utawala wa haki unapokosekana, kama, roho za chuki na visasi hutawala kama tulivyoona kule Nepal

G0GPBvwXcAAqH2p.jpeg
 
Huu ni ukweli samia hata kwa mpina hachomoi pamoja tume mbovu achilia mbali lisu
mzahamzaha mpina anaweza kumkalisha maza chini hivihivi, wajuvi wa mambo ya siasa wakaona itakuwa taabu, kura zitakombwa zote na mpina, ikabidi mpina awekewe pingamizi la kugombea yule mjuba. Nape kasema ukweli hakuna upinzani, waliopo ni vikaragosi wao wa kunogesha uchaguzi tu
 
Back
Top Bottom