Nape Nnauye: Kwa kazi nzuri ya Rais Magufuli, CHADEMA waache Siasa za enzi za Kikwete la sivyo watakimbiwa na wanachama wao wote.

Huyu jimboni kwake tu maji hakuna anapanua panua mdomo kwenye majimbo ya watu na kusifia ujinga
 
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, jana akihutubia Mkutano wa Kampeni za Ubunge katika Kijiji cha Mbizi, Jimbo la Buyungu, wilayani Kakonko, alidai kuwa, CCM ilimpitisha Dk. John Pombe Magufuli mwaka 2015 kuwania urais kwa kuwa, walimtaka mtu ambaye angeweza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali.Vilevile, mtu asiyewachekea wezi na pia kubana mianya yote ya rushwa.
Aliwaonya Wapinzani kuwa, kutokana na kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais Magufuli, Wapinzani wanatakiwa kuacha Siasa zao za kipindi kilichopita kwani wakiendelea watakimbiwa na wanachama wote.
Alidai wanaoilalamikia Serikali ya Awamu ya Tano, ni wale waliozoea kuiba fedha za wananchi ambao kwa sasa wamebanwa. Huyu ndiye Kiongozi anayehitajika.... hakuna jambo ambalo Watanzania wanaweza kumsema vibaya Rais Magufuli.
Aliwaonya Wapinzani kuwa, lengo la kuwepo kwa Mfumo wa Vyama vingi ni kuikosoa Serikali, siyo kuipinga inapofanya maendeleo.

View attachment 828430

Asante kwa ushahuri....
 
nimeamini wansiasa ni wanafiki. huyu juzi tu alitoka povu bungeni hadi akatishiwa na magu
 
Nape ni mnafiki namba moja. katika wanasiasa wenye uwezo mdogo ila wamejaa mipasho na umbeya ni Nape
 
Huyo naye anaongea tu kwa sababu ni siasa lakini moyoni kuna kitu kinamuumiza sana kuhusu huyo huyo mtu anayemfagilia

Ndiyo keshaongea sasa.Moyoni kwake unakujuaje? Niambie yaliyopo moyoni mwa Mbowe kama hutapata uchizi.
 
Puwer politics. Political sciience inasema ukuwa na lengo B huku watu wako wana lengo A basi unaingia na lengo A ili u win support wakishakupa nafasi unarudia lengo lako B. Lakini maneno havunji mfupa japo yaweza kuchekesha au kumliza mtu!
Hao ni opportunists politicians ....!!
 
BONGOLALA, kweli bana afadhali Mbowe ni DJ, Msigwa ni mchungaji; Zitto ni mwanasiasa nk
Mbowe sio DJ wewe,umekuja lini Dar toka kijijini kwenu. Unawajua akina Chris Phabby,Kalikali, et al,ulikuwa bush gani wakati huo.
 
Back
Top Bottom