Nape nnauye kijana hodari wa kughushi

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
Nape Nnauye ambaye ni katibu mwenezi wa CCM amekuwa hodari wa kughushi katika maisha yake. Kijana huyu alighushi kuwa CCM wakati akiwa na mbinu za kuanzisha chama cha CCJ huku akitumia nyaraka za kitapeli, vile vile alighushi kadi za CCM ili aweze kushinda kura za maoni CCM. Hivi sasa amedandia kombati za CDM.

Kijana huyu ameghushi barua akidai ni za CDM. Huwa anasema uongo, haaminiki, hayuko makini. Alidanganya umma kuwa ndani ya siku tisini mafisadi watatoka au wataondolewa. Ameshindwa kueleza sera za chama chake, zaidi ya wananchi kushuhudia giza na hali mbaya ya uchumi. Amefanywa domokaya na kuwa mpayukaji siku hadi siku. Pamoja na tafauti za kiitikadi tulitegemea vijana wenye damu changa na kujua mahitaji ya wakati wangeweza kuleta mwanga kwenye dunia ya leo hasa kukuza na kuwa na mbinu mpya za kiuchumi.

Tumechoka siasa za majukwaani kutoka chama tawala. Kazi kubwa ya chama tawala ni vitendo sio ahadi. CCM walishatoa ahadi zaidi ya 70, wanatakiwa kuzitekeleza sio kutuahidi kila asubuhi.

Tumechoka na lugha za kughushi.

Ni mimi
Chief Mkwawa wa Kalenga
 
Hadi sasa Nape anaongoza kwa kula posho za safari nyingi kuliko kiongozi yeyote wa Magamba. Anakusanya pesa za kumng'oa Mnyika
 
Naona Chadema mnamgwaya sana Nape,mnampa umaarufu wa bure kila siku hapa JF post nyingi Nape Nape Nape! Mnamuogopa wa nini? Mnampa Umaarufu tu wa bure au anawatisha kwa lipi? Acheni mambo ya kumpa mtu umaarufu wa bure
 
Back
Top Bottom