Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Mwanasiasa haaminiki hasa katika ulimwengu huu wa tatu, tunataka siasa za hoja,sio majungu, siasa ya uwazi na ukosoaji wa uwazi na uhuru kwa kila anayekosoa kistaarabu. Msamaha wa kweli pale kunapotokea kutofautiana maana wote tunafikiri kwa ajili ya nchi Kwanza sisi baadae
 
Naam,

Mbunge wa Mtama kupitia CCM ndugu Nape Nnauye leo kakutana na Raisi Magufuli Ikulu kujadiliana masuala ya kitaifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo pamoja na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuomba msamaha mara baada ya kuzungumza na wanahabari. Hii ni baada ya mazungumzo yao pamoja na kusamehewa kosa aliliofanya miezi michache iliyopita.

Pia soma;

Mzee Makamba alisema kweli huyu atakuwa anabatiza kwa moto tena mbele ya kamera
 
Sijaelewa kinachoendelea ndani ya jahazi ila tunaweza kusema ni taarifa kwa wale wanaodhani jahazi linaingia maji na linaweza kuzama ilihali maji yanaingia na kutolewa.

Kwa lugha yetu wakongwe huwa tunasema
(mtoto kashika adabu) maana mmoja mmoja anaenda nyumbani na kukiri.

Ila kwa muktadha huu wa kupigwa masnap kutokea juu tena popote unapotokea huku jasho likimwagika sijaelewa mantiki yake!!.


IMG_20190910_144407.jpg


IMG_20190910_144604.jpg


IMG_20190910_144651.jpg


IMG_20190910_144508.jpg
 
Utusamehe sisi wakosefu ndio picha inachojaribu kueleza hapo
 
Katika kinachoonekana ni kuipigia salute njaa baada ya kusota mitaani bila kazi ya kumfanya atembelee magari ya kifahari .

Nape ameanua kujisalimisha rasmi kwa yule anaye toa ridhiki yaani rais Magufuri na kuomba msamaha .Amakweli hakuna mwenye jeuri juu ya njaa.
20190910_145931.jpeg
 
Back
Top Bottom