Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Ni aibu kwa taaluma nzima ya usalama,kwa mwanausalama kumvamia kiongozi bila ya kujitambulisha na kuonyesha kitambulisho na kuanza kumtisha kwa bastola ili atii amri yako.

Nakushauri kamanda Sirro umrudishe uyu kijana akasome vizuri sheria za usalama kuliko kulitia aibu jeshi la polisi.

Haapa alivyotolewa bastola, Msanii Harmorapa naye alikuwepo hapo ila alitimua mbiop baada ya Bastola kuonyeshwa.

Dah!

Mimi si mpenzi wa CCM na si shabiki wa Nape ila hicho nilichokiona kwenye hiyo video sijakifurahia.

Kwangu haki ni haki tu.

Ni nini hasa kilipelekea yote hayo?

Kuna anayejua humu anieleweshe zaidi?
Hapa alikuwa anaingia viwanja vya Protea Hotel kwa ajili ya kuingia ukumbini kuanza mkutano, ndipo hawa vijana walipomfuata na kumtaka asishuke kwenye gari badala yake aondoke...ila mwishoni alweza kuendelea na mkutano japo kwa mbinde!
 
Askari ni binadamu ambao unaweza ukawatuma utakavyo na wakafanya bila kuhoji hata ukiwaambia nendeni mkaue basi watatenda na yakiharibika unawakataa wanabaki wenyewe bado wataogopa kusema walitumwa heeeeee heeee narudia tena Alhamdullilah namshukuru Mungu sikutumbukia kwenye kazi hii na kwenye kizazi chetu hakuna aliekumbwa na balaa hili sijui wanalishwa nini maana baba zima ila linaweza kutumwa na Bashite na likaenda bila kuhoji
Uyo askari hapo ukimuuliza kwa nini alikua anatumia nguvu zote hizo hata mwenyewe atashangaa na anaweza kukataa kua sio yeye heee heeee
 
FB_20170323_16_38_26_Saved_Picture.jpg
 
Tunapotaka Jeshi la Polisi liboreshwe na liachane na kasumba za mkoloni tunataka kuepukana na ubabaishaji kama huu wa kuamrisha kufanya kitu hata kama hakina msingi wa kisheria. Kuna wapuuzi wanadhani hili jeshi ni poa tu maana linashughulikia zaidi wapinzani(Lissu na Lema), lakini upuuzi huu unajengeka ndani ya jeshi na matokeo yake watakaoumia zaidi ni wanyonge ambao hata elfu tano ya kumhonga askari amuachie hana.

Haya mambo hayana mwenyewe. Hata rais anaweza kuwa victim wa jeshi kama hili-maana kuna kustaafu. Kuna ndugu na jamaa ambao wanaweza wakaangukia ktk mikono ya jeshi hili babaishaji. Hata askari wenyewe hawako salama ndani ya jeshi hili. Fikiria mtu anakutuma wewe askari ukaue wakati yeye amekaa na mke wake nyumbani. Kumbuka unaua mtu-sio kuku na hivyo damu ya mtu huyo inakuandama maisha yako yote. Mshahara mnaopata enyi askari hautoshi kuua raia wema wanaotumia haki yao ya kikatiba kuwa na mawazo tofauti na watawala.
 
Askari ni binadamu ambao unaweza ukawatuma utakavyo na wakafanya bila kuhoji hata ukiwaambia nendeni mkaue basi watatenda na yakiharibika unawakataa wanabaki wenyewe bado wataogopa kusema walitumwa heeeeee heeee narudia tena Alhamdullilah namshukuru Mungu sikutumbukia kwenye kazi hii na kwenye kizazi chetu hakuna aliekumbwa na balaa hili sijui wanalishwa nini maana baba zima ila linaweza kutumwa na Bashite na likaenda bila kuhoji
Uyo askari hapo ukimuuliza kwa nini alikua anatumia nguvu zote hizo hata mwenyewe atashangaa na anaweza kukataa kua sio yeye heee heeee
huku kwetu tunawapiga na mawe m
 
Back
Top Bottom