Nape Nnauye anawasili asubuhi hii Missenyi Kagera Kunusuru CCM!

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
Taarifa ni kuwa atakutana kwa faragha na vijana wa CCM wa wilaya hiyo ,kikubwa ni kuwa katika mji mdogo wa kyaka ambao ni mji wa wilaya hiyo kumekuwepo na ongezeko la vijana na makada wa CCM kujiunga CHADEMA na hivi karibuni serikali nzima ya kijiji iliyochaguliwa ni CDM.sasa anafika hapa kusafisha hali ya hewa.

Afya yangu si nzuri hivyo sikwenda huko kujua ataongea nini lakini waandishi wenzangu kadhaa wamekwEnda , hivyo nitwajuza kila kitu kupitia kwao.

lakini pia taarifa ni kwamba atawasili bk mjni kw ndege ya kukodi kutoka mwanza.

"...................."
Byabato
 
Lazima afike kusalimia ukweni kwa Makamba kwa Babu zake na January hapo Kyaka.
 
MImi nadhani ziara yake ni kwa ajiri ya Mazishi Kesho ya Dr Kyaruzi...wala si vinginevyo. Nadhania tuuuu!!!
 
Hivi kuna mtu anayemkubali huyu dogo kweli.
najua huko atakwenda kuharibu zaidi.
 
vijana maneno sio vitendo!yatupasa kuwa makini kifikra na utendaji pia kwa mtu mmoja mmoja na vikundi ikibidi!tujifunze kwa yaliyopita tupate dira kamili ya kuinusuru nchi hii?vizazi vijavyo vitukumbuke kwa mema sio hoo!waliingia mikataba laghai ...mpaka lini?
 
Nape huyu tunaemfahamu aiokoe ccm??? Wee ndugu una vituko, Nape keshajivua gamba siku nyingi nyie hamjagundua tu! Ile project yake ya kuwavua magamba alituambia kuwa ina deadline ya siku 90, zikaisha na hakuna tulichokiona zaidi ya kushadidiwa msamiati wa "siasa za majitaka" na yeye kukanusha deadline ya siku 90! Hapo alipo anajua kuwa CCM ya Nyerere na baba yake imegeuka ccm ya kisanii (kindly note my uses of upper and lower cases kwa mlio na akili) na ushahidi ni nguvu alizotumia akidhani ccm inaweza kugeuka kuwa CCM tena. Alipo kajikatia tamaa I tell you!
 
Back
Top Bottom