AMARIDONG
JF-Expert Member
- Jun 24, 2010
- 2,502
- 180
Mwaka 2002,August,nikiwa najisomea nyumbani,majira ya kumi na moja jioni,huku nikifuatilia matokeo ya kura ya Uchaguzi Mkuu wa ndani wa CCM,nilistuka kusikia Nape, akiwa na miaka 24 wakati huo,wakati huo akisoma Chuo Cha Kivukoni,akitajwa kuongoza katika kinyanganyiro cha kutafuta Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM,kupitia kundi la Vijana la watu kumi.
Nilistuka si kwa sababu kijana huyo hakuwa akifaa kuweza kushinda.Nilistuka kwa sababu sikuwahi kumsikia akizungumzia nia yake hiyo hadharani wala kuonyesha mapenzi na masuala ya siasa.
Wakati wote kijana huyo alikuwa akijihusisha zaidi na masuala ya dini katika kanisa lake la wakati huo la Free Pentecostal Church of Tanzania,FPCT,kanisa la Singida Mjini.Mara kwa mara, alikuwa akipata nafasi ya kuhubiri pale kanisani,licha ya umri wake mdogo wakati huo.
Upo ujumbe wa Jumapili moja,ambao hadi leo umenasa katiaka akili yangu ambao kijana huyu alipata kuufundisha pale kanisani mwanzonni mwa mwaka 2002 alioupa jina la 'Jiandae Kufanikiwa'.Kama vile Obama aliyeanza kuonyesha kipaji chake cha uongozi kanisani kwake alikokuwa akisali kama Community Organiser,ndivyo ilivyokuwa pia kwa Nape.
Baadaye,mwaka 2004 kamanda Nape,aligombea Uenyekiti wa UVCCM na kura hazikutosha.Kama kamanda asiyekata tamaa ,mwaka 2008 aliwania nafasi hiyo tena , na sote tunajua kilichotokea.Kama mpiganaji asiyechoka ,mwaka 2010 aliomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kugombea Ubunge jimbo la Ubungo lakini hakutimiza ndoto yake hiyo.
Baadaye mwaka 2010, aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya MASASI kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama.
Katika CCM, kutokana na hila ,ghiliba,mizengwe na uhuni, mara zote Nape alizogombea ameambulia patupu isipokuwa ,kutokana na sababau wanazofahamu vyema wateuzi,Nape hajawahi kusahaulikahata mara moja.
Manenno na kauli zake za hivi karibuni zinaashiria kuwa kwake yeye UONGO,GHILIBA zinaweza kuruhusiwa iwapo tu zinafanywa katika ulingo wa siasa.Na sidhani kama Mungu wa Mbinguni ana adhabu tofauti kwa uongo unaotendwa katika siasa na ule unaofanywa katika maeneo mengine.
CCM inaelekea sasa mwisho wake.Nini hatma ya kisiasa ya Nape.Mimi sijui, huenda yupo miongoni mwetu anayejua.
Nimesema kweli yote kadiri ninavyoijua,na kamwe uongo na fitna kwangu ni mwiko maana ni DHAMBI.
HONGERA NAPE KWA KUJIELEZA,KUMBE UNAJITAMBUA VIZUrI