Nape Nnauye: Alipotoka, alipo na aendapo

FortJeasus

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
603
397
Mwaka 2002,August,nikiwa najisomea nyumbani,majira ya kumi na moja jioni,huku nikifuatilia matokeo ya kura ya Uchaguzi Mkuu wa ndani wa CCM,nilistuka kusikia Nape, akiwa na miaka 24 wakati huo,wakati huo akisoma Chuo Cha Kivukoni,akitajwa kuongoza katika kinyanganyiro cha kutafuta Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM,kupitia kundi la Vijana la watu kumi.

Nilistuka si kwa sababu kijana huyo hakuwa akifaa kuweza kushinda.Nilistuka kwa sababu sikuwahi kumsikia akizungumzia nia yake hiyo hadharani wala kuonyesha mapenzi na masuala ya siasa.

Wakati wote kijana huyo alikuwa akijihusisha zaidi na masuala ya dini katika kanisa lake la wakati huo la Free Pentecostal Church of Tanzania,FPCT,kanisa la Singida Mjini.Mara kwa mara, alikuwa akipata nafasi ya kuhubiri pale kanisani,licha ya umri wake mdogo wakati huo.

Upo ujumbe wa Jumapili moja,ambao hadi leo umenasa katiaka akili yangu ambao kijana huyu alipata kuufundisha pale kanisani mwanzonni mwa mwaka 2002 alioupa jina la 'Jiandae Kufanikiwa'.Kama vile Obama aliyeanza kuonyesha kipaji chake cha uongozi kanisani kwake alikokuwa akisali kama Community Organiser,ndivyo ilivyokuwa pia kwa Nape.

Baadaye,mwaka 2004 kamanda Nape,aligombea Uenyekiti wa UVCCM na kura hazikutosha.Kama kamanda asiyekata tamaa ,mwaka 2008 aliwania nafasi hiyo tena , na sote tunajua kilichotokea.Kama mpiganaji asiyechoka ,mwaka 2010 aliomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kugombea Ubunge jimbo la Ubungo lakini hakutimiza ndoto yake hiyo.

Baadaye mwaka 2010, aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya MASASI kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama.
Katika CCM, kutokana na hila ,ghiliba,mizengwe na uhuni, mara zote Nape alizogombea ameambulia patupu isipokuwa ,kutokana na sababau wanazofahamu vyema wateuzi,Nape hajawahi kusahaulikahata mara moja.

Manenno na kauli zake za hivi karibuni zinaashiria kuwa kwake yeye UONGO,GHILIBA zinaweza kuruhusiwa iwapo tu zinafanywa katika ulingo wa siasa.Na sidhani kama Mungu wa Mbinguni ana adhabu tofauti kwa uongo unaotendwa katika siasa na ule unaofanywa katika maeneo mengine.

CCM inaelekea sasa mwisho wake.Nini hatma ya kisiasa ya Nape.Mimi sijui, huenda yupo miongoni mwetu anayejua.
Nimesema kweli yote kadiri ninavyoijua,na kamwe uongo na fitna kwangu ni mwiko maana ni DHAMBI.
 
Asante mkuu kwa uchambuzi mzuri, ila kaa ukujua kuwa ukishakuwa kwenye mfumo wa ccm(mfumo fisadi) basi hata kama ulikuwa mweupe kama theluji utabadilika kuwa mweusi kama mkaa, tukisema ccm chafu tunamaanisha wote wanaounda ccm ni wachafu bila kumbakiza hata mmoja yeyote yule ajionae kuwa yeye si mchafu ndani ya ccm na basi ajitoe sasa vinginevyo mimi binafsi sitomkubali kuwa msafi. Just a charcoal don't expect anything white
 
Nape na wengine wengi ndani ya CCM ni sawa na maji ya kunywa kwenye ndoo ya chooni! Kwanza Mwoga wa kusema ukweli na pia ni bingwa wa siasa maji-taka, hvo basi ka' kijana mwenzangu namkataa maili100!
 
Pamoja na dhambi zote za CCM na udhaifu wa Nape mwenyewe kama binadamu wengine, Nape ni mpaganaji na mpambanaji mzuri. Ni mvumilivu, anajituma, kimsingi ni mwanasiasa. Tatizo ni moja tu, mahali alipo "CCM" si muafaka sana kwake kwa sasa. Kwa mfano hivi sasa Nape angekuwa Chadema, kwa haiba na jitihada zake angekuwa chachu kubwa sana ya mabadiliko na nyota yake kisiasa hasa kwa kundi la vijana ingekuwa juu zaidi. Anyway, fungu alilochagua ni CCM, ngoja tuone atakavyochanga karata zake. Ila naamini kwamba, kwa mtiririko wa mambo ulivyo sasa, CCM inabidi ianguke kwanza kama sio kufa kabisa, ndipo mambo mengine ya maendeleo ya taifa letu yafuate. Haya ni mawazo yangu na naamini ni neutral kabisa.
 
Nape na wengine wengi ndani ya CCM ni sawa na maji ya kunywa kwenye ndoo ya chooni! Kwanza Mwoga wa kusema ukweli na pia ni bingwa wa siasa maji-taka, hvo basi ka' kijana mwenzangu namkataa maili100!

CCM ni chama cha kimafia; mambo yao mengi wanafanya kwa kisirisiri na kuapizana. Mfano ni maamuzi wanayofanya wanapoteua wagombea wao katika chaguzi mbali mbali huwa wanatangaza wanachama wao wajitokeze kuwania nafasi fulani lakini wakati huo huo huwa wamekwisha kaa na kuamua nani wanamtaka!! Tunaposema wanaamua mara nyingi tunafikiri kuwa maamuzi ni by consensus, hapana kwenye vikao vyao neno la Mwenyekiti ndio final hakuna kubisha! Ukikosana na mwenyekiti ndani ya ccm huna haki hata siku moja hata kama ugonvi wenu ni wa mabibi! Nape hana mwisho mzuri pale ccm kwani wenzie ambao mwenyekiti anawaamini kama wakinaNchimbi wanamuangalia tu anapayuka payuka huku wakimlia timing; wakati muafaka ukifika watammaliza na safari hii hapatakuwepo mtu kama Mangula wa kumuokoa!!
 
:disapointed::disapointed:hapa tanzania tunakabiliwa na matatizo chungu nzima lakini si vibaya kuyaainisha baadhi tu kama UFISADI,ELIMU MBOVU,MUKAMA NA NAPE, EL NA HIS ALLIES NA MWISHO KABISA JAPO SI HITIMISHO UDINI
 
Dawa ya Nape ipo jikoni inachemka ila hana maisha marefu kwenye kile kiti chake lazima afanyiwe kitu mbaya. Chanzo mimi mwenyewe,

Atafanyiwa nini stay tuned.
 
Asante mkuu kwa uchambuzi mzuri, ila kaa ukujua kuwa ukishakuwa kwenye mfumo wa ccm(mfumo fisadi) basi hata kama ulikuwa mweupe kama theluji utabadilika kuwa mweusi kama mkaa, tukisema ccm chafu tunamaanisha wote wanaounda ccm ni wachafu bila kumbakiza hata mmoja yeyote yule ajionae kuwa yeye si mchafu ndani ya ccm na basi ajitoe sasa vinginevyo mimi binafsi sitomkubali kuwa msafi. Just a charcowal don't expect anything white
Wewe tu umenena vema. labda ushauri wa bure kwa Nape ni huu. ikiwa anaipenda hatima yake kisiasa ni lazima sasa afikirie kuhamia Chadema. Hii haina ubishi kwa wakati huu kwamba ukiwa ni mmagwanda unakuwa na ihakika wa kunivunia siasa kuliko kuwa mmagamba. wakati ni ukuta.
 
Nape anatumikia tumbo lake, anajua fika kuwa siasa za ccm ni za majitaka, lakini kwasababu uhai na heshima ya mtu inatokana na kula na mapene hana budi kutulia ndani ya chama cha magamba.
 
Back
Top Bottom