yegella
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 3,113
- 1,104
CHADEMA wamwanika Nape
*Marando asema alinufaika na pesa za EPA kwa Patel
*Yadaiwa anapata mishahara miwili ya CCM, na U-DC
*Wadai aliomba kugombea ubunge Chadema, akakosa sifa
Na Peter Mwenda
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha vikali tuhuma kuwa Mwenyekiti wake, Bw. Freeman Mbowe ameagiza
chama kununua magari yake matatu aina ya Fuso, kufafanua kuhusu mshahara wa Katibu Mkuu wake, Dkt. Willibrod Slaa na kuibua tuhuma mpya dhidi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA, Bw. Antony Komu alisema tuhuma hizo zinazotolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Wilson Mukama na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye zinalenga kuwachafua viongozi wa chama hicho na kupotosha ukweli juu ya vita inayopiganwa na CHADEMA dhidi ya ufisadi na mafisadi.
"Madai kuwa Dkt. Slaa ameshinikiza kulipwa sh. mil. 7.5 siyo kweli, tunaomba ieleweke kuwa hajawahi kuomba, kushinikiza wala kuchagiza kulipwa kiasi hicho cha fedha kama ambavyo viongozi wa CCM wanavyotaka kuaminisha umma," alisema Bw. Komu.
Akiwa na maofisa wengine wa CHADEMA, Bw. Mabere Marando na Profesa Abdallah Safari, Bw. Komu alisema Dkt. Slaa analipwa sh. mil.7.1 ambazo zimejumuisha mshahara na marupurupu yote.
"Dkt. Slaa analipwa posho yake binafsi ambayo inaweza kuitwa mshahara sh. 1,725,000 wakati mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi, Katibu wa CHADEMA analipwa mafuta ya kuja ofisini na kurudi nyumbani lita 30 kwa siku, sawa na lita 900 kwa mwezi, bei ya kila lita moja sh. 2,000" alisema Bw. Komu.
Alisema wakati Dkt. Slaa analipwa kiwango hicho mbunge analipwa lita 1,000 kwa mwezi kwa bei ya kila lita moja sh. 2,500 bei ambayo haipo lakini bunge linaridhia kulipa.
Bw. Komu anaendelea kusema kuwa ingekuwa sahihi kusema kuwa Dkt. Slaa ananufaika sawa na mbunge kama angekuwa analipwa zaidi mbali ya sh. mil. 7,174,000 anazogharimiwa na chama.
"Mbunge akikaa katika kikao cha Kamati ya Bunge au akihudhuria mkutano wa bunge analipwa posho ya sh. 70,000; sh. 30,000 posho ya mafuta na sh. 80,000 posho ya kujikimu akiwa Dodoma, fedha hizi zinalipwa bila kujali kama mbunge huyu amekuja na gari lake Dar es Salaam na amekwenda nalo Dodoma," alisema Bw. Komu.
Alisema mbunge anapewa mkopo wa sh. mil. 90 ambazo anatakiwa kulipa nusu ya fedha hizo, mzigo unaobaki unabebwa na serikali na pia serikali hiyo hiyo inamdhamini kukopa sh. mil. 200 kutoka vyombo vya fedha.
Bw. Komu alisema viongozi wakuu wa CHADEMA wakiwa katika makazi yao hawalipwi posho zozote kwa kazi wanazofanya na wakiwa nje ya makazi yao kama ziara mikoani, hulipwa sh. 40,000 kwa siku kwa ajili ya chakula na malazi.
Akizungumzia ununuzi wa Fuso, Bw. Komu aliwataka Watanzania kufahamu kuwa CHADEMA ndiyo walioomba kuuziwa magari hayo ambayo CCM inayaita chakavu.
Alisema magari hayo hayawezi kufananishwa na magari mengine ya Fuso yanayotembea mitaani, hiyo ni mitambo maalumu yenye vipaza sauti vyenye thamani ya sh. mil. 222 na jenereta tatu ambazo kila mmoja ina thamani ya sh.mil. 47.
Bw. Komu alisema kila gari lina bodi maalumu yenye uwezo wa kubeba watu wasiopungua 12, jenereta moja kubwa, mafuta ya helkopta, jukwaa la kuhutubia na vifaa vya matangazo ambazo zote zimejengwa kwa sh. milioni 48.4.
Alisema CHADEMA imeweka wazi malipo ya viongozi wake, gharama za uchaguzi na vyanzo vyake vya mapato na jinsi inavyotumia mapato yake.
"Tunasisitiza kuwa CCM ni chama cha mafisadi kwa kuwa viongozi wake ni mafisadi, wanafiki na wasio wakweli, wamekiri wenyewe katika kile wanachokiita kujivua gamba katika siku 90 wanachama na mafisadi, CHADEMA tunataka kuona hilo linafanyika bila kisingizio," alisema Bw. Komu.
Akizungumza na Majira mjini Sumbawanga Dkt. Slaa alikataa kuzungumzia madai hayo, akisema 'hakuna hoja wala jipya katika kauli ya Nape...lakini pia hana muda wa kujibizana naye, si saizi yake.
"Nilitegemea atazungumza jipya, nilitegemea kusikia ufisadi wa CHADEMA na Dokta Slaa, sasa naona kaishia kuzungumzia mshahara wa Dokta Slaa tu, jambo ambalo tumeshalitolea ufafanuzi, aende akasome kwa nini liko hivyo," alisema Dkt. Slaa kwa ufupi.
Naye Bw. Marando alisema Mnauye hana hadhi ya kuinyoshea kidole CHADEMA kwa kuwa si mtu makini mwenye agenda ya wananchi kwani wana ushahidi wa kutosha kuwa ni mmoja wa watu walionufaika na fedha za wizi wa EPA kupitia Jetu Patel ambaye alitoa maelezo yake mbele ya Kamati ya Rais.
"Alitumia fedha hizo kusaka uongozi ndani ya CCM, hivi sasa analipwa mshahara wa ukuu wa wilaya na huku analipwa na CCM na kutumia fedha za Serikali kufanya kazi za CCM," alisema Bw. Marando.
Bw. Marando alisema Nape Mnauye baada ya kushindwa kupata nafasi ya katika kura za maoni kugombea ubunge Jimbo la Ubungo kupitia CCM aliomba agombee kupitia CHADEMA akakataliwa kwa kuwa hakuwa na sifa za kumzidi John Mnyika ambaye ni mbunge wa CHADEMA katika jimbo hilo.
Alisema Nape Mnauye alikuwa mmoja wa wasisi wa CCJ na iweje leo awe na ubavu wa kuonyoshea kidole CHADEMA.
"Yeye ndiye aliyetumwa CCM kuiwakilisha katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA 2010 ambaye alisema Chadema inakwenda vizuri kama taasisi na kwa hoja, leo inakuwaje?" alisema Bw. Marando.
Alisema Chadema ndiyo maana inaona Nape ni vuvuzela anayecheza ngoma asiyoijua, mnafiki mzushi na mtu asiye na msimamo.
Bw. Marando alisema Chadema wanataka majibu ya msingi kama vile sababu za kufilisika kwa serikali, mchakato wa katiba mpya na kupanda kwa gharama ya maisha