Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema wakati wa mchakato wa chama kurejesha imani kwa wananchi hali ilikuwa ngumu kwake hadi kufikia kutishiwa maisha na watu wasiojulikana.
Mbali ya watu hao kumpigia simu za vitisho nyakati za usiku, pia walikuwa wakimchafua kupitia mitandao ya kijamii lakini anamshukuru Mwenyezi Mungu alivuka salama na chama kimevuka salama.
"Tulipoanza kuzunguka kujenga chama nilitukanwa sana. Watu waliwekeza kunichafua. Watu hao niliokuwa nawanyooshea kidole hawakufurahishwa na hatua ile hivyo wakaweka mkakati wa kutaka kunifukuzisha ndani ya chama na ilifika hatua wakawa wananichafua katika mitandao ya kijamii.
Nikaamua kujitoa huko mpaka leo hii nimeamua kujitoa katika mitandao na kubaki katika twitter pekee kwa kuwa unaweza kutambua mtumiaji," alisema Nape.
Akizungumza katika mahojiano maalumu nyumbani kwake mkoani Dodoma, Nape alisema watu hao walifikia mbali zaidi na kudai yeye si mtoto wa Mzee Moses Nnauye.
Chanzo: Mwananchi